Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Ndege Alhamdulillah nimeanza kuzipanda tangu nikiwa sijazaliwa. Nikiwa mdogo likizo nakabidhiwa tu kwa wahudumu hapo safari Mwanza tu Dsm basi napokelea dsm na nikirudi Mwanza the same,kitu kilikua kinanichanganya utotoni ni kufungua ac hapo ilikua lazima niombe usaidizi.Sema kuna kitu nimekinotice hususani kwa ndege za ndani,unakuta muhudumu anaongea kiingereza na kifaransa sasa wanasahau si kila msafiri kasoma mtu anaweza shinda kuelewa maelekezo kwa lugha tu zinazotumika,ndege za ndani watumie na Kiswahili
 
Yakwangu sio mara ya kwanza ila ni kioja balaa,ni mwaka 1997 December 22 kutoka Dar kwenda Amsterdam na KLM. Miezi hiyo kwa kawaida Dar ni joto sana so nilivaa kaptura ya jeans na Tshirt na nikisafiri sipendi kubeba mizigo ya mikononi kwani ni msahaulifu,hivyo mizigo yangu yote niliipitisha ipimwe ili nisibaki na kitu mkononi.Safari ilikuwa nzuri mpaka tunafika,sasa karibu tunatua Amsterdam rubani anatutangazia hali ya hewa nasikia outside at ground level is -5 C,sikuwaza wala kushtuka sana coz kwa wakti huo ndani ya ndege ilkuwa pako poa sana.Ile tumefika wenzangu wote wanafungua mikoba yao na kutupia makoti marefu even air hostess mimi nabung'aa macho tu,tukashuka kwenye ndege kwenda ndani ya basi ili tuende terminal watu wote wananishangaa,nikaanza kuwa mweupe ule wa unga,mpaka tunafika lounge,mdomo hauwezi funguka.Bahati nzuri wenyeji wangu kama walihisi manake waliomba ruhusa nikaletewa koti refu la sufi,gloves na Kofia mzula.Nilikuwa kama mfu nusu kuongea siwezi,vidole vya mikono vimekakamaa balaa mabegi nayaona yanapita ila siwezi kuyachukua,pale Amsterdam kuna sehemu wenyeji wanawaona arrival kwenye kioo,so waliniona the way nilivyoganda wakaomba waingie kunisaidia mizigo.Mpaka naingia kwenye gari siwezi kuongea,hadi tunafika nyumbani heating system ilisaidia baada ya masaa mawili ndo niliweza kunyanyua mdomo.
Siwezi kusahau kioja hiki kwani wakati natoka Dar nilikuwa "Bontown" ila kule nilikuwa zoba (kila mjanja ana mjanja wake)
[emoji23][emoji23]pole sana mkuu....sipati picha abiria wenzio wapo kwenye makoti wakikuangalia wew na kikaptura walikuwa wanakufikiriaje
 
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
sasa tukiwa huko tukalipwa posho kwa hela ya huko Central African Franc sasa nikazibana nije kubadilishia Bongo nafika bongo Bureau De Change zote hawabadilishi hizi pesa yaani nmepagawa sijui nikazitupe Coco maana....
[emoji23]Kata tiketi ukazibadili
 
Back
Top Bottom