and 300
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 26,398
- 36,406
A390 vs A220
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
@ Mama Sabrina sijui ndiyo huu?Habari mchanganyiko
Nimeonaa nimecheka
Kuna huu pia binamuWeka linki ya uzi unaochekesha RRONDO
Asante binam ngoja nisome nicheke
Hapana ni mwingine
Enjoy tu kwa kweliAsante binam ngoja nisome nicheke
[emoji23][emoji23]pole sana mkuu....sipati picha abiria wenzio wapo kwenye makoti wakikuangalia wew na kikaptura walikuwa wanakufikiriajeYakwangu sio mara ya kwanza ila ni kioja balaa,ni mwaka 1997 December 22 kutoka Dar kwenda Amsterdam na KLM. Miezi hiyo kwa kawaida Dar ni joto sana so nilivaa kaptura ya jeans na Tshirt na nikisafiri sipendi kubeba mizigo ya mikononi kwani ni msahaulifu,hivyo mizigo yangu yote niliipitisha ipimwe ili nisibaki na kitu mkononi.Safari ilikuwa nzuri mpaka tunafika,sasa karibu tunatua Amsterdam rubani anatutangazia hali ya hewa nasikia outside at ground level is -5 C,sikuwaza wala kushtuka sana coz kwa wakti huo ndani ya ndege ilkuwa pako poa sana.Ile tumefika wenzangu wote wanafungua mikoba yao na kutupia makoti marefu even air hostess mimi nabung'aa macho tu,tukashuka kwenye ndege kwenda ndani ya basi ili tuende terminal watu wote wananishangaa,nikaanza kuwa mweupe ule wa unga,mpaka tunafika lounge,mdomo hauwezi funguka.Bahati nzuri wenyeji wangu kama walihisi manake waliomba ruhusa nikaletewa koti refu la sufi,gloves na Kofia mzula.Nilikuwa kama mfu nusu kuongea siwezi,vidole vya mikono vimekakamaa balaa mabegi nayaona yanapita ila siwezi kuyachukua,pale Amsterdam kuna sehemu wenyeji wanawaona arrival kwenye kioo,so waliniona the way nilivyoganda wakaomba waingie kunisaidia mizigo.Mpaka naingia kwenye gari siwezi kuongea,hadi tunafika nyumbani heating system ilisaidia baada ya masaa mawili ndo niliweza kunyanyua mdomo.
Siwezi kusahau kioja hiki kwani wakati natoka Dar nilikuwa "Bontown" ila kule nilikuwa zoba (kila mjanja ana mjanja wake)
Merry Christmas and Happy New Year to you too palMerry Christmas [emoji319] and Happy New Year.
Ndege gani hiyo mkuu?Nairobi to Somalia (Mogadishu ) huku mnawaza kutunguliwa
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.
Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.
Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.
Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.
Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
Fastjet ishajifia long time na inadaiwa 6bn ( milioni 6000) tshsJambo sana ndugu zangu.Kuna mtu anae jua gharama za kusafiri kwa fast jet from Dar to mwanza.Msaada please,