Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka saa 12 asubuhi (ndege ndo inapaa) mimi nikajipa kama dakika 20 kutoka home Tabata mpaka Airport, nikidhani ni kama Mabasi ya Mkoani pale Ubungo stendi duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichokaje. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege.

**NEW DEVELOPMENT
Mwezi Juni 2015 nilipata safari ya kwenda CAMEROON (kwa hisani ya Watu wamarekani USAID) sasa tukiwa huko tukalipwa posho kwa hela ya huko Central African Franc sasa nikazibana nije kubadilishia Bongo nafika bongo Bureau De Change zote hawabadilishi hizi pesa yaani nmepagawa sijui nikazitupe Coco maana....

****MPYA ya 2016
Mwezi Januari nilienda NEW DELHI duuh pale airport hakuna sijui kutangaza wala nini ni KIMYA KIMYA tu ukisubiri matangazo utastukia ndege ishakuacha.

HAKIKA USHAMBA MZIGO!
Umenikumbisha vile niliacha mafuta yangu hapo JNIA kisa yamezidi mils 100, tulikiwa kundi la watu kama 10, tulipita kila airport kulitokea kiroja.

Tukiwa bongo hapa haikuwa shida sana japo kubabaika kulikuwa kwingi,tumefika Dubai jamaa kapapaswa kadakwa na wembe mfukoni mambo hayakuwa magumu sana tukatoka japo tulipoteza muda.

Tumeingia Beijin jamaa yuleyule kadakwa na dawa ya meno Colgate kubwa,hapo ikawa shida tena....simu nyingi na maelezo karibia nusu saa hapo.

Tukatoka beijin kwenda jimbo moja na Kunming,hapo tena akadakwa na LUNDO LA NYEMBE...sijui alitaka izifanyie nini walahi hapo ndio wakamkalisha chini kabisa na tulikaa takribani saaa zima ndio jamaa akaachiliwa na tulikuwa tunaunganisha ndege kwenda wilaya ya Xuanbana_sina uhakika na spelling, sasa kule walimkagua hadi mapumbu,wakati wa kurudi hakukutokea tatizo.

mie niingia online nikasoma vitu vyote visivyoruhusiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole yake huyo mjuba. Next time atajipanga
 
Back
Top Bottom