Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Dege la jeshi balaa halina mikanda wala viti, mtapanda na mbuzi, matairi, makorokoro kibao, sasa inapokaribia kutua lazima utazaa tu km ni mja mzito! linashuka ghafla fyuuu! kama mara tano hivi! na kushuka lazima ujiachie km unarushwa hivi na kudakwa! raia wanakomaje!

Lkn wajeda wao aaah!peace tu
 
baada ya gradu yangu chuo.Tukarudi mkoa na maza. Fastjet ndo imeanza.Nı mara yetu ya kwanza wote.
1. Mama anataka kukaa akakuta juu ya siti sehemu ya mizgo kuna mtu kashaweka wake.Akatia,"wee kondaa,we kondaa wéeh,hebu njoo kwanza"

2. Nikajaribu kwenda choóni japo sijabanwa alimradi tu nione pakoje

3.Facebuk page yangu iliomba poo. Mara checkin in at JKİ Airport. Mara nitupie picha alimradi kila mtu ajue.

4. Tulivofika madreva tax wakaanza kututukana eti "hamna lolote nyie mtakuwa fastjet tu" hapo kisa ni baada ya wao wanatugombania sie hatuna time tunaenda kwny daladala.

5. Jioni napokea simu toka kwa mjomba: "ah mjomba nimeamini ushamba mzigo wa mwiba".Nkamuuliza kwanini? Akasema,"leo sina raha. mama yako kutwa nzima anantambia kwny simu kisa kapanda ndege"
Nimecheka sana aisee...yani unakuja na ndege unaenda kupanda daladala[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
day 1 nili enjoy sanaaaa yani sanaaaa

baada ya hapo safari zilizofata ni hofu tupu as ..sipendi wakati inapoanza kuruka na wakati wa kutua. Pia hali ya hewa ikiwa mbaya safar inakuwa hovyo.

kioja changu kilikuwa kwenye pasport jamani.. nilipata ile ya muda as ilikuwa ya karatasi huyo mbio stationary kuifanyia lamination eti isiharibike. Walahi kama sio yule binti wa stationery sijui huko airport ingekuwaje ..looo!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom