Kenya wametangaza kufunga mpaka na Tanzania, wameruhusu bidhaa ziendelee kuingia kwa kuwa wanazo nyingi ziingiazo Tanzania lakini hawataki madereva wa kitanzania kuingia Kenya. Huu ni ujinga uliopitiliza kwa upande wa Kenya, wamejivika kitanzi wenyewe kwa kuwa biashara zao za vyakula vilivyosindikwa zitadoda. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amefanya yake, anastahili pongezi, lakini mpaka huo ufungwe tu.
Kenya na Msumbiji wakiamua wao kufunga mipaka yao, tuwajibu kwa kufunga mipaka yetu pia, kwa nchi kama Zambia, Malawi,Burundi, Rwanda na Uganda wakileta zao isiwe shida, tusiwafungie mpaka ila tuwasogezee mizigo yao kwenye bandali kavu huko huko kwenye mikoa inayopakana nao ila waje wachukue mizigo hiyo pale mpakani kwa gharama zaidi kwa kuletewa mizigo yao mpakani,.... Kama wanamwaga ugali, tumwage mboga tu!.
DRC ni chimbo tofauti, namna bora ya kufanga nao biashara ni kulitumia ziwa Tanganyika ipasavyo kwa kuzijengea uwezo bandali za Kigoma Kipili na Kirando ili kuziunganisha na Kalemie upande wa DRC.