Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Kuna jamaa yangu mmoja alipigwa hii na malaya villa mwanza.

Katoka North mara, tuko tunacheck band pale, mara akapita mwanamke mmoja hata kama umekaa na Beyonce meza moja lazima ugeuke. Jamaa mate yakamtoka, akamvuta mezani. Mida ya saa 5 dem anataka akale, sasa namuambia msosi hapa si upo akasema anataka twende salma cone ndio kuna mishkaki mizuri. Basi, K zinanguvu, tukaondoka kuelekea salma cone. Njiani dem akasema anataka apite kwake abadili nguo ili awe huru. Kwake anasema anaishi Mkolani.. (Dah, hii route kwa watu wa mwanza nadhani mnanielewa). Nikamwambia mbona mbali sana.. Sasa sbb dem alikuwa mbele na jamaa ndio anadrive, naona alizidiwa nguvu akiweka gia mkono unagusa paja..

Mwana akasema twende tu, akipitia crdb ya Pale lapf safari ikaanza. Kufika mkolani, tukasimamishiwa lodge. Nikamuuliza ndio hapa, dem akasema ndio hapa, amekuja kwenye semina na amefikia hapa. Nikahisi hapa ipo namna. Sbb mtu kichwa kidogo kishasimama kikubwa hakifanyi kazi.

Tukarudi na kufika salma cone. Msosiz baadae tukaenda club hadi night kali jamaa yuko tungi.. Dem kama hajanywa vile na amegonga savanna kama 10.. (Nikahisi huyu ni mamba). Kufika lodge, nikawaacha.. Asubuhi saa 2 napigiwa sim namba ngeni... Kufika lodge, jamaa anasema Dem kasepa na Iphone, Note 5, na laki 4... Nilijikuta nacheka sana badala ya kusikitika.

Sasa kuuliza ilikuwaje, jamaa anasema alipoingia alipiga kimoja, wakaingia bafuni, dem akarudi chumbani na kuja bafuni, wakiwa mle dem akaanza mnyonyesha matiti.. Akaona kama mwili unazidi ishiwa nguvu... Akashtuka asubuhi yuko bafuni... Wale watu wa lodge wanasema dem alitoka saa 12 akidai anamfuatia mmewe dawa za moyo amezisahau bar...

Ikabidi twende kule lodge, kufika kule wanasema huyo mwanamke alichukua chumba tu hapo alilala na mtu, so muda ule alipokuja alibadili nguo na kutoka. Chumbani kukuta kaacha nguo tu zile za usiku uliopita.

Ukiona vitu visivyo vya kawaida nasi ujue hapi taa nyekundu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ivi 2013 kulikuwa na balimi ndogo? Mchai chai umezidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuuu baharia wa Pacific[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha tuu huo mkasa sijawahi kumsimulia mtu zaidi ya yule shoga angu aliejionea na humu maana niliona dunia imenielemea yani na mm nimetapeliwa duu kijingaaaa
Ishawahi kumkuta rafiki angu aisee...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nilicheka sanaa yani hatukuamini kama ndo tushaibiwa hivyooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo bahat mbayaaa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…