NGOJA NIWAPE MKASA MMOJA
kuna boss wangu juzi nimemtapeli kazi aliyoniandikia pamoja na 50000 ya lodge.
Alikuwa ananitongoza nikakubali nikamwambia aniandalie document flani ambazo nilitakiwa nikaguliwe kazini kwa kuwa alijua atapata mzigo akaniandalia hizo document.
Siku ya kuzifata akaniambia yupo pale Madengo bar ya Dodoma wengi wanaifahamu. Basi nikaenda pale nikaagiza savvana kama mbili na Kitimoto rost nikazifukia nikala nikashiba.
Nikamwambia document zikwapi akasemaa hizi hapa kwenye bahasha nikazichukua nikaweka kwenye mkoba nikatulia.
Akasema tutafute lodge tukalale mm nikamwambia kwa sababu wewe ni mheshimiwa watu wakikuona itakuwa shida unatengeneza skendo nipe hela mm nikachukue chumba pale Simba hotel alafu nakupigia simu unakuja.
Akawa amenipa elfu 50000 ya chumba mm nikachukua pikpik ndruuuuki mpaka Geto kwangu.
Nilivyofik ninatumia sms usinitafute mm nipo nyumbani.
Hapa nilipo nawaza siku nikipata shida ya kikazi yeye ndiye boss wa hicho kitengo atanisaidia?
Maana alimpigia simu mpaka kiongozi wa ofisi yetu kumwambia jinsi mfanyakazi wake nilivyomtapeli.
Sent using
Jamii Forums mobile app