Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Visa vya matapeli na watoto wa mjini

[emoji23][emoji23][emoji23] najua umewagusa wengi humu
Mimi bingwa wa kutapeli wanaume wa mitandaoni wanitumie nauli.

Kama ni utapeli basi na mimi nipo kwenye hilo kundi najiuliza nini sababu mbna kazi ninayo pesaa ninazo lakini natapeli hela za nauli?

Basi najikuta na kesho naendelea tu kutapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia mjini shule, shamba darasa. Jiulize hao waliotunga huo usemi walikuwa na maana gani ama walikutana na masahabu gani!

Akili ya binadamu ni kitu cha kushangaza mno. Kina uwezo wa ajabu hasa pale mtu anapokutana na changamoto mbalimbali. Huko vijijini akili nyingi zimelala kutokana na kukosa changamoto za kimaisha.

Kijijini hata kama huna kazi huna pesa utaishi tu... Sio mjini! Mjini tangu kunapambazuka mpaka kunakuchwa kila kitu ni shekeli. Hakuna cha bure mjini. Lakini vilevile mjini kila mtu anatamani kuishi maisha fulani lakini changamoto ya elimu kipato na ajira ndio kikwazo.

Hivyo basi kuweza kukabiliana na changamoto hizo watu kila uchao hubuni mbinu mpya za kuingiza kipato. Kuanzia utapeli, wizi, ujambazi, kukaba, kurubuni nknk. Kila mmoja wetu hawezi kukosa kisa cha hawa jamaa wanaoishi kwa ujanja ujanja. Nitaaza mimi kwa kusimulia vichache

Kisa cha kwanza
Huyu jamaa yeye hakuwa na kazi maalum. Ila muda wote ni msafi akionekana kama afisa fulani hivi. Siku moja akawa kakosa nauli kabisa ya kurudi nyumbani kwake Tabata na yuko kijitonyama.

Alichofanya ni kuwarubuni wale jamaa wa magari ya majitaka kuwa anataka huduma hiyo Tabata... Wakapatana bei akaenda nao mpaka mtaa wa pili kufika kwake.

Akashuka huku akiwaelekeza uchochoro mmoja kuwa ndio kwake... Akaingia hapo akatokea upande wa pili akasepa mazima.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kisa cha pili.
Ni wale jamaa wanaorubuni watoto kuwanunulia chakula ama chochote. Ataenda na mtoto hapo mahali ataagiza kama ni bidhaa ama chakula.... Kisha atasepa na kumuacha bond mtoto wa watu..

Karibu nawe kabla sijaendelea na visa vingine

Jr[emoji769]
kuna wale wapo kariakoo karibu na shule ya uhuru wakiwauzia watu sabuni badala ya simu yenyewe.na mabosi zao ndio wenye maduka wakiwazamini simu hizo kisha jioni kuleta hesabu.na wenye maduka ya vitu vya nyumbani hapo kkoo ndio wanao ongoza kuhuza miche ya sabuni kwa matapeli.[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna wale wapo kariakoo karibu na shule ya uhuru wakiwauzia watu sabuni badala ya simu yenyewe.na mabosi zao ndio wenye maduka wakiwazamini simu hizo kisha jioni kuleta hesabu.na wenye maduka ya vitu vya nyumbani hapo kkoo ndio wanao ongoza kuhuza miche ya sabuni kwa matapeli.[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuu

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom