Kuna mzungu ni Raia wa Armania nilikua nawasiliana nae kwenye mtandao2, tulikua na Biashara ya Madini (Almasi) akaniomba nimtumie picha za Mali nilizo nazo yani hayo mawe, nikamtumia picha nyingi sana zikiwa tofauti tofauti, kuna Rejection, kuna nyeupe sana yani Dee colour, kuna kubwa kuanzia carat 10 kuendelea, sasa ikafika mda ikabidi atue Bongo ili tufanye Biashara, akafika Dar akanijulisha nikamwambia panda ndege uje Mwanza, akaja bwana Mzungu yule nikampokea Airport, nikampeleka Hotel asbhi yake tukaamkia Biashara, nikaanza kumwaga Mali mezani, nilimimina kila aina ya Almasi kasoro pink2 ndio ckua nayo, walikua wawili wao mimi nipo peke yangu yani one man show, lkn lkn kila Mali akihama bei ananihama pungufu, yani mfano Mali ya dola elf5 yeye anatoa elf3 au mbili, mwisho nikaona hkna wanunuzi hpa nikamuuliza umekuja kununua kweli au unafanya window shop? Akasema kweli nimekuja kununua, nikamtupia tena carat 42 Dee colour manake ndio ilikua kipimo changu cha mwisho kwake, nikamwambia hii Mali nataka dola laki5 mzungu Akasema dola laki2 nikachukua Mali yangu nikaweka mfukoni nikamwambia kwaheri, lkn kumbe wakati nafanya nae biashara alikua na mawasiliano na jamaa wengine kumbe ni matapeli, walikuja kumtupia chupa zilizochongwa wao matapeli wanaziita (nyau) alipigwa mzungu Dola laki 4, yule mzungu nahisi alienda kujiua uko Armania
Sent using
Jamii Forums mobile app