Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Atapeli wazee sokoni Manzese.

Jamaa huyu ni mwalimu( Tapeli mzoefu)

Kakodi taksi toka muhimbili mpaka Manzese sokoni pale Bakhresa. Kufika pale kaagiza mikungu ya ndizi ya elfu 30000 kisha anakwambia hebu nipe elfu tano hapo nichukue kabichi utaunganisha ktk bili yangu. Anaenda kwa muuza kabichi hapohapo pembeni yako anachukua kabichi za elfu kumi kisha anachukua elfu mbili achukue vitunguu. Jamaa alitapeli meza kama tano akajipatia kama elfu hamsini mkononi akawaacha kila mtu na mzigo wake akasepa...sasa bada ya kujua wamepigwa wakamuendea dereva taksi...awaonyeshe bosi wake...hapo ndo walichoka yaani yule jamaa kamkodi toka muhimbili mpaka manzese na pale anasubiri pesa yake.

Nb

Baada ya malalamiko kuwafikia matapeli wa manzese wenzake. Wakamtafuta siku alipopata pesa akaenda kuwalipa wote kasoro dereva teksi.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Jamaa Asafiri mpaka Morogoro kumendea mzigo.

Tapeli wa mazense kanunua mabegi sawa baada yakupewa mchingo wa pesa ndefu.

Kuna mtu alikuwa anaenda Mwanza ana begi kubwa moja. Jamaa akanunua mabegi kama yale mawili. Akakata tiketi gari lilelile akapata pata siti ya karibu naye akaweka like begi pambeni kidogo ya yule jamaa wa mwanza alipoweka. Gari kufika Moro jamaa akashuka akashuka na begi la msukuma. Akapanda gari akarudi Dar...
Ndani akakuta vitenge vya waksi doti kama hamsini. Fedha kama laki tatu na khanga na nguo nguo nyingine.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Nakumbuka enzi hizo za Jakaya vyuma havijakaza tulikuwa wadada wa 5 tunapeana dili za kuwanyoosha watu wazima ovyo mibaba ilokuwa inapenda kutongoza ovyo.
Teamwork ilikuwa na mmbulu,mnyarwanda,shombe la kizungu,kisomali na mchaga kila mtu alikuwa akikutana na danga anatupasia namba mmoja anajifanya kakosea kutuma hela afu ana tuma msg au kupiga simu uku analia lia katuma pesa kimakosa alikuwa anamtumia mama ake anaumwa basi muamala unarudi kama ilikuwa efu 5 inakuwa laki na wataendelea kuwasiliana na vizinga vinaendelea mtu anapigwa huku na huku ye hana habari ndo ukawa mchezo wetu.
siku ya siku kidogo yatutokee puani mimi nilikutana mkongo akawa anajifanya mfanyabishara mkubwa kumbe tapeli alijua ntababaika ili anile papuchu bure nikamlia vihela vyake nikampotezea nikampa rafiki yangu namba akatumia mbinu zote na rafiki yetu mwingine wakamtapeli mkongo hela ndefu wakamblock siku moja tunakutana na yule mkongo tukiwa wote wa3 akajua kabisa alichezewa mchezo nilikimbia mbio zote kati kati ya mji.
Mungu wangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Mangi ajifanya mjanja, apigwa laki sita.

Mangi anaduka hapo TipTop kamweka kijana. Sasa akaja jamaa mmoja dukani kwake akamwambia dogo ampimie bidhaa zikafika kama laki tatu. Sasa kumbe bosi yupo ktk mtu pembeni mchezo wote anauoana. Akaenda pale dukani akamwambia lipa kbsaa jamaa akamwambia twende utarudi na pesa...mmiliki wa duka akakubali akapanda guta wote wanaenda pamoja...kufika karibu na mabibo sokoni jamaa akasema anataka na mikungu ya ndizi...hivyo akawaelekeza waende nyumbani kwake akawaelekeza nyumba inayoneka mbele wamuulizie mama Jack...

Kumbe kile kitendo wale wanaenda kwa mama Jack yule jamaa akarudi pale dukani fasta kwa dogo...akamwambia amapimie tena mchele na maharage na mazagazaga kibao jumla laki sita dogo akaambiwa afanye fasta ili awawai ili bosi wake yule dogo wa dukani aunganishe arudi na pesa yote. Dogo akfanya kama alivyoelekezwa ili jamaa awai...
Mwisho wa siku bosi na mwendesha guta wamefika ktk ile nyumba wanaulzia mama Jack awape pesa yao wanaambiwa hakuna mtu kama huyo....Yule bosi anasema mpumbavu alitaka kunitapeli huyu...nilimstukia mshenzi sana hahaa...kurudi dukani sasa anakuta tobo la laki sita alichoka

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Atapeli wazee sokoni Manzese.

Jamaa huyu ni mwalimu( Tapeli mzoefu)

Kakodi taksi toka muhimbili mpaka Manzese sokoni pale Bakhresa. Kufika pale kaagiza mikungu ya ndizi ya elfu 30000 kisha anakwambia hebu nipe elfu tano hapo nichukue kabichi utaunganisha ktk bili yangu. Anaenda kwa muuza kabichi hapohapo pembeni yako anachukua kabichi za elfu kumi kisha anachukua elfu mbili achukue vitunguu. Jamaa alitapeli meza kama tano akajipatia kama elfu hamsini mkononi akawaacha kila mtu na mzigo wake akasepa...sasa bada ya kujua wamepigwa wakamuendea dereva taksi...awaonyeshe bosi wake...hapo ndo walichoka yaani yule jamaa kamkodi toka muhimbili mpaka manzese na pale anasubiri pesa yake.

Nb

Baada ya malalamiko kuwafikia matapeli wa manzese wenzake. Wakamtafuta siku alipopata pesa akaenda kuwalipa wote kasoro dereva teksi.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Jamani ina maana humu hatujawahi kukutana na visa hivi vya kitapeli?
Karata 3?
Madini bandia?
Mercury bandia?
Noti bandia?
Bidhaa bandia kama simu, Marathi, viatu nk?
Dili za kusambaza madawa ama chakula kambi za wakimbizi?
Bahati nasibu za mitandao? Nknk

Jr[emoji769]
 
Kama kisa hiki ni cha kweli basi una njaa kali sana.
NGOJA NIWAPE MKASA MMOJA

kuna boss wangu juzi nimemtapeli kazi aliyoniandikia pamoja na 50000 ya lodge.

Alikuwa ananitongoza nikakubali nikamwambia aniandalie document flani ambazo nilitakiwa nikaguliwe kazini kwa kuwa alijua atapata mzigo akaniandalia hizo document.

Siku ya kuzifata akaniambia yupo pale Madengo bar ya Dodoma wengi wanaifahamu. Basi nikaenda pale nikaagiza savvana kama mbili na Kitimoto rost nikazifukia nikala nikashiba.

Nikamwambia document zikwapi akasemaa hizi hapa kwenye bahasha nikazichukua nikaweka kwenye mkoba nikatulia.

Akasema tutafute lodge tukalale mm nikamwambia kwa sababu wewe ni mheshimiwa watu wakikuona itakuwa shida unatengeneza skendo nipe hela mm nikachukue chumba pale Simba hotel alafu nakupigia simu unakuja.

Akawa amenipa elfu 50000 ya chumba mm nikachukua pikpik ndruuuuki mpaka Geto kwangu.

Nilivyofik ninatumia sms usinitafute mm nipo nyumbani.

Hapa nilipo nawaza siku nikipata shida ya kikazi yeye ndiye boss wa hicho kitengo atanisaidia?

Maana alimpigia simu mpaka kiongozi wa ofisi yetu kumwambia jinsi mfanyakazi wake nilivyomtapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona penzi linafufuka upya.
Safi sana.
Hawara hana talaka
Kaanzisha mada ya utapeli ili atapeliwe tena na chamdeko wake.
Mshana itakua amemiss kutapeliwa na taratibu mambo yataenda kama yanavyopaswa kua.
The bold na Niffah wake nao siwaoni kabisa siku hizi sijui hata kulikoni.

Maendeleo hayana chama
 
Kaanzisha mada ya utapeli ili atapeliwe tena na chamdeko wake.
Mshana itakua amemiss kutapeliwa na taratibu mambo yataenda kama yanavyopaswa kua.
The bold na Niffah wake nao siwaoni kabisa siku hizi sijui hata kulikoni.

Maendeleo hayana chama
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
umenikumbusha mbali, hizo ndio ilikuwa zangu enzi hizo mpaka nilinunua fenicha za ndani kuanzia kitanda, godoro kabati makochi tv nk kwa pesa za kutumiwa nauli hahaha dah!
Mimi bingwa wa kutapeli wanaume wa mitandaoni wanitumie nauli.

Kama ni utapeli basi na mimi nipo kwenye hilo kundi najiuliza nini sababu mbna kazi ninayo pesaa ninazo lakini natapeli hela za nauli?

Basi najikuta na kesho naendelea tu kutapeli.
 
Back
Top Bottom