James Comey
JF-Expert Member
- May 14, 2017
- 8,759
- 14,831
Atapeli wazee sokoni Manzese.
Jamaa huyu ni mwalimu( Tapeli mzoefu)
Kakodi taksi toka muhimbili mpaka Manzese sokoni pale Bakhresa. Kufika pale kaagiza mikungu ya ndizi ya elfu 30000 kisha anakwambia hebu nipe elfu tano hapo nichukue kabichi utaunganisha ktk bili yangu. Anaenda kwa muuza kabichi hapohapo pembeni yako anachukua kabichi za elfu kumi kisha anachukua elfu mbili achukue vitunguu. Jamaa alitapeli meza kama tano akajipatia kama elfu hamsini mkononi akawaacha kila mtu na mzigo wake akasepa...sasa bada ya kujua wamepigwa wakamuendea dereva taksi...awaonyeshe bosi wake...hapo ndo walichoka yaani yule jamaa kamkodi toka muhimbili mpaka manzese na pale anasubiri pesa yake.
Nb
Baada ya malalamiko kuwafikia matapeli wa manzese wenzake. Wakamtafuta siku alipopata pesa akaenda kuwalipa wote kasoro dereva teksi.
Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo