Miaka ya 2000 mwanzoni tuliwahi kulizwa na wazee wa kazi.
Mzee alikuwa ana duka la kuuza baiskeli na spea zake. Basi siku ya siku jamaa wakaja wakamkuta mzee wakamwomba kama anazo shilingi moja moja awatafutie watazinunua 1 kwa sh 20, mzee akazisaka mule dukani akapata kadhaa, maana kipindi hicho zilishaacha kutumika.
Wakazinunua akapata kama 15,000/-, basi wakamwambia awakusanyie watakuwa siku fulani, walipokuja walikuta kakusanya nyingi kidogo, wakanunua, alipata kama 250,000/-.
Mzee akaambiwa akusanye zaidi maana kuna wazungu ambao wanazihitaji sana, wanataka mzigo mkubwa, kwamba kuna vito wanatumia kutengenezea.
Basi kwenye kutafuta mzee akakutana na mtu ambaye alisema anazo ila anauza kwa bei ya sh 10 kila moja maana dili limeshajulikana kwamba anauza kwa 20. Akanunua mzigo wa almost 900,000/-, maana kuna shamba aliuza kuongezea hela. Hapo alitegemea faida mara 2.
Jamaa hawakurudi tena, ikaja baadae kugundulika wale jamaa waliomuuzia mzigo wa mwisho ndiyo hao hao walionunua kwake mwanzoni.