Unauziwa nguo usiku, kesho ukirudi lile eneo wamepanga viazi
Niliwahi fanya ujinga huu kigoma ujiji, sijisifii lakini kila siku nimekuwa nikijutia kitendo nilichokifanya na nina imani hata huyo niliyemfanyia atakuwa amenisamehe.
Ilikuwa Kigoma, mpaka siku ya tukio nilikuwa nimeshakaa siku 21 nalala msikitini, mpango wangu ulikuwa kuvuka kuingia nchi jirani, lakini kutokana na mambo yalivyokuwa tofauti najikuta nagika kigoma nina shilingi hamsini tu, muda ulikuwa ni ule wa salat magharib, sipendi kuelezea sana ila nilikomaa mui huo ka hizo siku 21 mapanga na kupangua, cna ndugu zaidi ya Utanzania wangu, hiyo siku nakumbuka...nitaendelea
Ilikuwa ni jumanne ktk pitapita zangu nikaona tangazo la mganga wa kienyeji kubwa kwamba ndio kiboko huyo mama na anuani zake pale, nikafuata maelekezo mpaka ujiji nikaulizauliza nikaelekezwa nikafika, wakati mimi naingia kulikuwa kuna jamaa na wakezake wawili walikuwa ndani kwa huyo maman a muda huo ndio walikuwaw akiondoka, nikasubiri mpaka wametokomea ndipo nami nikabisha hodi na nikakaribishwa ndani, nikamsalimu yule bi mkubwa kisha nikatulia tuli sikusema shida yangu, yule bibi akaseti mitambo yake pale kisha akaanza yeye kunichana mimi matatizo yangu na tangu siku naamua kutokomea huko, yaani hakuacha kitu ikumbukwe mimi sikwenda huko kuinjoy maisha hapana, nilikuwa na targets zangu ambazo hatanikiamua kuzianika hapa mnaweza kunielewa tofauti ila kifupi ni ktk kupambana nitoboe ninakotaka kwenda..bibi akaongeaaaa sana na mwisho nikaona naniwekea usiku nikamuuliza kama tayari matatizo yangu yote ushayajua unanisaidiaje? Akasema yeye atanisaidia kwa elfu arobaini, Dah, nikasema huyu bibi mwehu nini? Ina maana kashindwa kujua kama hapa sina hata kumi? Nikamwambia fanya dawa ila moyoni nilishavurugwa kwa tabia ile ya kutaka pesa wakati mfukoni sina mia nyekundu, Yule mama alinyanyuka akaingia ndani kuongeza dawa huku nyuma mimi nikabeba simu yake Nokia ya tochi na kwenye ungo kulikuwa na shilingi elfu hamsini ambazo nahisi wale niliopishana nao ndio walizitoa, nikabeba kisha nikamuandikia ujumbe ktk kipande cha gazeni "nikifanikiwa nitarudi, ahsante kwa msaada wako" nikaondoka, nikavaa lemba langu (Kama wapalestina) nilikuwa na kijiti nikakiweka mdomoni kisha nikanuia ninavyojua huku natokomea kule chini ziwani....ni story ndefu ila mwisho wa siku yule bibi alikuja ziwani akinitafuta na akaja kuniuliza kijana hujamuona kijana flani anarangi hivi na nywele zake ndefu kazibana kwa nyuma? Ananiuliza mimi na mtu anayemuulizia ni Mimi...nikamwambia sijamuona mama huku natafuna kile kjiti na napiga dua zote mnazo zijua na msizo zijua ili yule aondoke niendelee na safari, karata ilikuwa upande wangu ile ibilisi nikaiepuka ila sasa mbele ya safari boti ( mtumbwi wenye engine mbili) ulizama jirani na hifadhi ya gombe....naomba niishie hapa kwa sababu nazojua mwenyewe