Visa vya Uchawi na Ushirikina Mkoani Kigoma Mwisho wa Reli

Umenielewa sasa[emoji16][emoji16][emoji23]
 
Kuna jamaa fulani wawili wa kigoma walikuwa na mazoea ya kutaniana na mshkaji fulani hivi mtu wa pwani

Unajua utani huwa unayemtania akichukia ndiyo utani umemuingia
Jamaa alikuwa anawaweza wakigoma

Kumbe hawa jamaa walikuwa wamechukia kweli na hawataki tena utani
Siku moja kaja maskani tumekaa kapata dili kaenda kupiga karudi amekaa
Anasema anaskia kizunguzungu
Anasema mtu unaweza kufa hivi hivi kimasihara akatuambia ameishiwa nguvu anaomba akae chini kaomba maji kaomba apelekwe nyumbani kafia njiani

Kumbe jana yake walitoka kutaniana sana na washikaji walimaindi sana mpaka kuwatahadharisha watu wamwambie asicheze nao hawataki lawama baadae

Tangu pale wale jamaa nilikuwa nawaangalia tofauti sana why warahisishe uhai wa mtu kiasi kile
Walianza kuogopwa sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wana uchawi wao unaitwa "Kidono"

Ni zindiko kali sana hilo, hata ukatwe mapanga, au risasi haiingii


Yaan mganga anachukua mwanawe, anamfanyia ilo zindiko

Kisha nakuambia wee umkatekate ..utakata weee lkn wapi


Sasa ndio ukiridhika anakufanyia wew
 
Kigoma ukikuta mtu kafa njiani, kafa amekaa au kapiga magoti ,usimwondoe hapo.


Ukimwondoa ndo anakufa jumlajumla.


Unapaswa, uite mganga chapchap, amurudishe hapohapo.
 
Kuna Mmama mmoja aliua Mtoto wa jirani

Yaan hao majiran walikua na ugonv, sasa mtoto wa jiran X akiwa anacheza nawenzake mpira, mpira ukaenda kwa nyumba ya jiran Y, alivyoufata tu..akakauka palepale na kufa



Familia X wakaamua kulipiza kisasi.. Yule mama Y, siku anakufa, Alikua anazaa watoto wanageuka kua watu wazima wale wote alowaua, kisha wanayeyuka

Alikufa kwa mateso sanaaa
 
Ukiishi kidole, USICHANGANYE UCHA MUNGU NA UGANGA.

KAMA NI WAMUNGU SALI SANAA..KAMA NI WA MGANGA KAGANGIKE SANAA
 
Traffic huwa wahawakamati vijana bodaboda na probox wa ujiji,na huwa hawaendi ujiji wanaishiaga maweni tu.maana ujiji wabembe ni balaa,lakini kigoma wachawi ni watongwe wa ilagala na watu wa njia za maji) kama wanavyoita hao huku mwamgongo kalya mpaka ufipa.ila waha sio wachawi nao wanaogopa sana watongwe,wabembe na warundi.
 
Kuna yule alikuwa Mkuu wa Mkoa toka Sumbawanga ambaye amefariki miezi michache iliyopita,alipimana ubavu kichawi na wazee wa Ujiji ngoma ikawa droo wakaanza kuheshimiana
Bro inaonekana ulikuwa mwamzi kwenye hili pambano
 
Huwezi kupewa kidono kama huna kinkuti.hizi dawa huenda sambamba lakini ni za wakongomani(wabembe)
 
Hiko kisa cha kwanza ni utopolo ntupu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hivi ulivyoongea ni vitu vya kibaiolojia kabisa ila kusema sijui mtu kuwafuata usiku amevaa pensi huu ni uongo maana hii habari ingetangazwa vyombo vya habari
 
Jamii yoyote iliyojaa waislam Hayo Mambo Ni kawaida
Itakuwa unapotosha kwa makusudu mazima au kwa kukosea ila Kama unaamini uchawi upo Basi unaweza kuwa na wasaa wa kuchunguza mikoa iliyo kwenye top ten ya wachawi inakaliwa na wenyeji wengi wa dini ipi hii itakusaidia na itatusaidia kwenye kuondoa upandikizi ulioukusudia
 
Hilo ni la kweli na kabla sijaivunja miiko yake ilishawahi kutokea wababe wakashindwa kunichana kwa kisu......majarbio ya hilo zindiko wanakufanyia wewe mwenyewe kwa kupigwa mapanga mwilini
 
😁😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…