Visa vyangu vya mapenzi: Harakati za kusaka mume

Visa vyangu vya mapenzi: Harakati za kusaka mume

😄😄😄
Nani kaelewa hiliTangazo...?
Mimi sijaelewa kwa mara yakwanza naomba unieeleweshe my dear japo kidogo . Maana ukweli ni huu mengi ni uongo na ukweli anataka mume sasa akisema anahela si atapata wengi mario
 
Mimi sijaelewa kwa mara yakwanza naomba unieeleweshe my dear japo kidogo . Maana ukweli ni huu mengi ni uongo na ukweli anataka mume sasa akisema anahela si atapata wengi mario
Kwanini nidanganye, nimeweka statement ya niko vizuri ili uweze kukaa katika viatu vyangu! Sababu sio uongo…. Sina mpango wa kupata mtu humu ila ninapenda kujua mawazo ya wengi kuhusu ‘dating’ ndani ya bongo.. Sijagoma kwenda sababu sina hela, nimegoma sababu sikupanga kwenda na sijaelewa kabisa hii situation huyo kaka alioniweka
 
Jamani eeh, dada yenu niko singo na niko kwenye haraki za kutafuta mpenzi! Ninajiweza niko sawa kifedha na la hasha navutia kwa kudra za mwenyezi Mungu ila usumbufu naouona ni bab kubwa. Ntakuwa nahadithia hapa muwe mnanipa ushauri wa kumchagua. Wanaume hawa wote ni wabongo kasoro baadhi. Mpaka natamani kuhama mkoa mwingine kutafuta mwenza wa maisha ila sasa kazi hizi jamani doh

Mwanaume wa kwanza: Agel
Agel ni mkristo mzuri tu tulisoma wote chuo huko Dom ye akapata scholarship kwenda majuu akabaki huko,Agel hajawahi hata kuniongelesha tulivokuwa chuo ila tulikutana mtandaoni siku moja akaulizia niko vipi anaona mihangaiko yangu na anapenda sana navojishughukisha ( me nauza nguo na vitu vya ndani ) basi bwana ye anaishi majuu na ana cheo kweli kweli, kupewa cheo nchi za watu sio rahisi cv imeshiba, ni executive fortune 500 company huko yeye ni mambo ya first class na kuendeshwa na dereva, ana hadi chef wa kumpikia .

Katika majadiliano siku moja akaniambia me Chenko nakuelewa mwenzako. Nikashangaaa nikamuliza why? Akasema wewe mpambanaji nimekupenda sana na nimekuwa nakupenda toka chuo basi tu ulikua mkimya mnoo… basi mtoto nikaona yes nimepata fortune 500 husband.

Ila katika maongezi jamaa nikawa simuelew elewi, kwanza ni mkali mlalamisha usipopokea simu anaandika message ndefu barua, tuko masaa 10 nyuma sasa ni ngumu kweli mawasiliano me nimelala yeye ndo anaenda kazini, pili kila saa ananisifia uko vizuri sana kifedha nakuadmire sijawahi pata mwanamke alie kama mimi, kidogo sikupenda hii statement… halafu kila saa anataka nimwoneshe napokaaa nyumba nimpe tour eh jamani, (hata ye alitaka kunipa tour nyumba ake nkasema ya nini jamani siku ukiniliaka si ntapaona?), gari naloendesha anataka address ya nyumbani kwangu kabisa , halafu maongezi yake mhhh mara ananimiss anataka kuhug sijui hajaona mwanamke miezi 6 toka kaachwa dah hasa nikawa nakuwa uncomfortable.. (hatujaonana miaka 12) huko nikawa nakausha basi akanialika niende majuu tupate our first date angalau, mhh nikasita kidogo sababu sijawahi fika marekani na anaishi new york kabisa ila nikapiga moyo konde sababu ni mualiko wacha tuone , nikatafuta visa nikapata.. khaaa kaka si ananiambia nijilipie ticket? Ye atagharamia kila kitu cha malazi nikifika.

Huyu Agel sijamuelewa yani unanifuata wewe una hamu kuniona wewe unanitongoza wewe unanisumbua nije tuwe na first date wewe afu nijilipie ticket? Akaniambia im sure unaweza kulipia haina shida kwako, doh statement imenikata mbaya…Hela ninayo ila sina shida ya kwenda marekani saa hiii, ndo kwanza nina safari ya china mwezi ujao kuchukua mzigo. Kanidissapoint, nimwache au nimwambie tukutane dubai afu nimsikilizie?


Nina experience na wanawake Kama wewe wa 5, you just raise your hand and give up, hamuwezi ishi na mwanaume, keep your strength and finances!
 
Kwanini nidanganye, nimeweka statement ya niko vizuri ili uweze kukaa katika viatu vyangu! Sababu sio uongo…. Sina mpango wa kupata mtu humu ila ninapenda kujua mawazo ya wengi kuhusu ‘dating’ ndani ya bongo.. Sijagoma kwenda sababu sina hela, nimegoma sababu sikupanga kwenda na sijaelewa kabisa hii situation huyo kaka alioniweka
Wewe unatakaje tuanzie hapo
 
Kwa maelezo yako nakushauri tafuta kiben ten (marioo) vinginevyo sioni ndoa hapo
 
 
Tafuta wafanyabiashara wenzio wa hapo kariakoo, distance utaiweza mama? afu huyo jamaa kwa story uliyotoa hamuendani, yeye ana mtazamo wa kimagharibi, wewe mwafrika mweusi typical
Umeniwahi na hii comment.

Bi. Dada alihisi keshayatoa maisha kupata mmarekani na mmarekani kajua kapata mmarekani mwenzie independent.
 
Huna experience na mimi. Hunijui na hujawahi experience a financially stable woman na ukamuacha. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Mkogo hivi wote, watu wa hovyo Kabisa, Hakuna mtu financial stable ana kuja kupiga kelele huku Jamii forum na kutangaza ujinga Kama huu, mtakutana na watu mnaofanana nao!

Yanga Bingwa - Hu ndo mfano wa maneno ya mtu Mwenye pesa!
 
Back
Top Bottom