Kwa ugonjwa huu wa Corona mikusanyiko ya na misongamano ni kichocheo kikubwa cha maambukizi, ukiangalia hali ya hewa ya baadhi ya Maeneo ya nchi hasa ukanda wa pwani, mahsusi Dar as salaam.
Vituo vya mabasi vya Kimara mwisho, Ubungo, Ferry, Kariakoo Mbagala, utaona hilo ni bomu linalo Subiri kulipuka, nilipita Kariakoo misongamano ni mkubwa sana, inazidi hata baadhi ya mikusanyiko inayokuwepo wakati wa kuangalia ligi kuu ya mpira.
Kwanini serikali inashindwa kupiga Marufuku machinga kariakoo na wauza bidhaa barabarani kwa sababu wanasababisha misongamano isiyo ya lazima, wamepanga bidhaa zao chini na kusabisha Barabara kuwa nyembamba.
Hivi hatuoni mitaa ya nchi ya wenzetu kwa sasa walivyochukua hatua thabiti, mabasi na madaladala yanajaza kupita kipimo, tumeambiwa ugonjwa huu unaambukiza kwa chafya, kugusana na kupitia jasho
Machinga wanaouza vitu kwenye magari kwenye mataa wanasika kila kitu unaponunua kitu kwa machinga hatujui bidhaa hizo watu Wangapi wanakuwa wameshika! kwa kuangalia au kurudisha wakiwa na nia ya kununua, Machinga wanakuwa wametokwa na majasho kwa kushinda juani na hali ya hewa ilivyo Mungu saidia
Tunalipa pesa kama nauli na tunapokea chenji, tunapeleka nyumbani bidhaa na chenji fikiria kama kuna maambukizi, kesho yake pia tunakwenda kazini, yaani mzunguko ni mkubwa sana
Nafikiri ni busara tuchukue hatua sasa, Ulaya na Marekani ni Marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 10 kukaa pamoja.
sisi tuna nini hadi tupuuze hayo, piga picha kama Machinga wataondolewa barabarani Kariakoo kutaonekana vipi naomba wahusika wachukue hatua haraka, kuna huduma za lazima kama wauza chakula nk wanaweza kubaki lakini siyo machinga wauza viatu nguo nk. Itabidi waondoke kutusitiri
Machinga wakiondolewa hata usafiri wa wala daladala na mabasi ya mwendo kasi utakuwa na ahueni
Sent using
Jamii Forums mobile app