Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Pole pole anasemaje maana siku hizi kawa msemaji wa kila tukio.
 
Dr Akili,

Mkuu huu ugonjwa huwezi kuujua hapo hapo
Wengi wanasafiri wakiwa wazima kabisa kumbe wanao
Lakini tahadhari pia ni muhimu nafikiri angekuwa anajua anao asingekanyaga huko
Simtetei ila huu ugonjwa mpaka kujitokeza hata siku kadhaa inachukua


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Katika watu tunaoweza kuwasahau ni wafungwa na mahabusu waliopo gerezani. Kuna haja ya kupunguza msongamano hasa kwa mahabusu.

Serikali iangalie namna ya kuweka masharti rafiki ya dhamana ili tupunguze msongamano.
 
Hivi wao walikuwa wanafanya mikusanyiko bado maana vyama vingine wao wakikusanyika ni mabomu na kukamatwa

Huku ndiko kunufaika na kuwa na Dola aliko kuzungumzia Katibu wa CCM Chama Tawala..🙄
 
Gereza Na Umasikini Huwezi Kuvicheka Vitu Hivi Viwili Ndio Maana Tunakomaa Watoke Wenzetu
 
Ku stop review means ratiba itavurugika May hakutakua na pepa itawawia vigumu sana ku arange mtihani hapo kati ndio mana wanakomaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona serikali imeahirisha mitihani ya form six ilikua may pia, vyuo na kadhalika. Yaani ratiba ya mitihani ndio iweke maisha ya watanzania hatarini kiasi hicho? Kwani hiyo mitihani haiwezi kufanyika wakati mwingine?

Hoo sio hoja kabisa. Maisha na afya ya watanzania kwanza, mitihani na masomo yatakuja baadae.

Itakuaje iwapo watakutana darasani halafu mmoja ametoka kukutana na muathirika wa corona bila kujua?
 
Mkuu Phillipo tatizo sio muda gani mtu anaanza kuugua baada ya maambukizo. Na wala hakuna njia ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa kwa wale wasiojua kwamba alikutana na nani.

Hoja hapa nadhani ni kitendo cha mtu kujichanganya na mgonjwa mwenye maambukizo halafu asitoe taarifa mapema.

Ni vyema kutoa taarifa mapema pale unapojua kwamba umejichanganya na mtu mwenye maambukizo, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati kuokoa maisha ya wengine.
 
Nilikuwa katika harakati zangu ghafla nikatokezea eneo la Ubungo riverside nimekuta jamaa kawakusanya watu wanaangalia mazingaombwe licha ya mikusanyiko siyo na maana kuzuiwa.

Rai yangu Watanzania tuwe waelewa na tusiache kuelimishana juu ya hili kwa sababu Serikali inaweza kuwa na nia njema kabisa ila tukaikwamisha kwa upuuzi wetu.

Nilijaribu kuongea na raia wachache wakanielewa,tusiache kukumbushana kila wakati ili kukwepa gharama zinaziweza kuepukika.

Serikali kusimamisha shughuli zake zote hizo siyo jambo dogo tulitilie uzito kwani ni kwa faida yetu.
 
Jana kariakoo kuna jamaa wanasalimiana kwa kushikana mikono wanasema Mlinzi ni Allah Pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…