Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Watu hawapo tayari kusaidia mtu kwenye mambo ya msingi. Wata pretend kukusaidia kwenye yale wanajua hayana maana ila ukiwa na real problem ndio utaona pretense yao ikijidhihirisha.
 
Ad majorem,
Sawa nimekulewa!
Hata muda huu ninavyo andika hii comment yangu Jimbo la Moshi wako kwenye shamrashamra za kumsimika Baba Askofu Minde, wako nyomi ya watu.

Hawaogopi ili hali Da' Isabela mwampamba yuko tu hapo Arusha jirani na Moshi
 
Juzi Machi 17 na jana Machi 18 serikali kupitia waziri Mkuu mh. Kassim Majaliwa imetangaza kuzifunga shule zote na vyuo Kuanzia awali mpaka Elimu ya juu.

Mpaka sasa wanafunzi na wanachuo wote wanatakiwa waondoke kurudi nyumbani kwao. Hili ni jambo jema sana ili kukabiliana na tishio la kuenea kwa corona.

Pamoja na juhudi hizo, serikali katika tamko lake imesahau kuelezea kinagaubaga kuhusu wafanyakazi wa taasisi hizo yaani walimu, wakufunzi, wahadhili, wahudumu na wafanyakazi wengine.

Je, wao hawaambukizwi au hawawezi kusambaza corona kama hivi sasa ambapo wanaendelea kwenda kazini? Kwanini serikali isiruhusu nao wakae makwao ili kuepusha huu msongamano huko kazini?

Mpaka sasa ni mvurugano tu maana wengine wanahofu kwenda huku mabosi wao wakisisitiza ni lazima waende kazini. Serikali tafadhali toeni tamko kuhusu hili.
 
Utaratibu unaotumikaga wanafunzi wakiwa wamefunga wapaswa kutumika na sasa ili ratiba ziende sambamba.
 
Kwa wake walimu walio shule za vijijini mbona na wao wamefunga tayari hakuna hata mmoja aliyebaki karibia wote nao wameenda likizo makwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimestushwa kusikia Taasisi kadhaa za Umma wakiwemo watumishi wa OR-TAMISEMI NA wizara nyingine wakiendelea na vikao katika maeneo kadhaaa morogoro.

Vikao vya kiutendaji vikipigwa marufuku ujue tumeshafika pabaya Sana...
 
Uzuri ni kwamba makanisa mfano katoliki wameshaweka taratibu za kufuatwa kipindi hiki cha corona.

Italia pale, wamekufa mapadre wengi sana kuanzia corona ilipoingia nchini mwao, huo huo ukaribu kati ya waumini na viongozi ndio umesababisha hivyo vifo.

La muhimu ni kuvumilia muda wa mwezi mmoja tu ili wataalam wautazame mwenendo wa hiki kirusi.
 
Soko hili Lina mkisanyiko mkubwa sana wa watu kuliko hata uwanja wa taifa, Serikali itupie jicho kufanya jitihada za kupunguza population eneo hilo,

Inawezekana yakatafutwa maeneo mengine wafanya biashara wakapelekwa sehemu mbalimbali na biashara zitafanyika tu kuliko watu wote kukusanyika kariakoo peke yake.

Tupambane na Corona kiukweli, Corona inaambukiza kwa njia za majimaji, na kwa joto la dar muda mwingi watu wanavuja jasho, sasa atokee mtu ana Corona pale kariakoo(mtaa wa Congo), atawaambukiza watu wangapi kwa siku, na hao watakaoambukiza watakaoambukiza wangapi?

#Corona ni hatari #

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi kubwa ni kujikabidhi kwa Mungu mambo mengi hayakwepeki kwa mfumo wa maisha yetu watanzania
 
Kuna Mapungufu makubwa katika Elimu afya inayotolewa kwa jamii juu ya COVID-19. Huenda Ni matokeo ya kila mtu kuwa mtaalamu wa afya. Inasikitisha kuona Kuna watu mnaamini kuwa ugonjwa huu, unaweza kuambukiza kwa jasho. Ndugu Bin Chuma Ugonjwa unaosababishwa na virus vya Corona hauambukizi kwa kila majimaji yatokayo mwilini Bali maji maji yenye viini vya Corona( Infected air droplets) yanayotoka kwenye mgumo wa upumuaji hasa pale mtu anapopiga chafya.
Tujifunze kwa wenzetu. Mfano Obama alipoulizwa kuhusu Corona, aliwashauri Wamarekani wazingatie ushauri unaotolewa na WATAALAMU wa afya hasa WHO na CDC.
Jurgen Klopp, Wakati flani aliulizwa kutoa comments zake kuhusu Corona, alijibu kuwa, yeye ni layman, Hana anachoweza kusema zaidi akashauri watu wazingatie ushauri wa wataalam wa afya.
Na sisi tunaweza kujifunza kwa Hawa wenzetu, Kwan kujifunza sio vibaya. Kinyume chake tukiruhusu kila mtu aongee yake, tutasababisha taharuki na hofu kubwa katika jamii. Mambo mengine yatasimama kabla ya Muda wake.
 
Ni kweli kujikabidhi kwa mungu lakini serikali ina jukumu kubwa kuhakikisha watu wake wanakuwa salama kama walivyozuia mkisanyiko mingine, basi wafanye jitihada za kupunguza watu maeneo ya kariakoo.

Ikumbukwe soko la kariakoo linabeba watu wa mataifa mbalimbali ya jirani, na huko kuna maambukizi makubwa zaidi kuliko sisi, hivyo tusipokuwa makini tutaangamia sana kupitia kariakoo.

Ni kweli hili jambo linahitaji elimu kubwa kwa jamii jinsi ya kujikinga, njia moja wapo serikali imezuia mikusanyiko, sasa na kariakoo pia panamkusanyiko mkubwa sana wa watu

#Corona ni hatari)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…