Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Mtanzania akiwa kwenye mkusanyiko usio wa lazima


Wabongo ambao majina yao hajakujulikana wakiwa kwenye mkusanyiko usio wa lazima

Kama kawaida ya watanzania bila kujali hali za maisha ni watu mfano wa kenge ambae kusikia kwake ni mpaka atoke damu masikioni kwa kupigo.Mwendelezo wa kukosa usikivu umetokea pia katika vita dhidi ya Corona.

Wakati ambao serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti kuenea kwa Corona,hatua hizo zimeonekana kupuuzwa mapema kabisa.

Serikali imeagiza tuchukue hatua kubwa 2,kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na usafi wa mara kwa mara hususani kunawa mikono kwa sabuni.

Mikusanyiko isiyo ya lazima imepuuzwa kabisa na watu wanaendelea na maisha kama vile hakuna kitu kimetokea. Wiki hii nilikuwa na safari ya kikazi,safari ambayo ilikuwa inanilazimu kula bar. Kwa uoga ba tahadhali nilikuwa nalazimika kuagiza chakula kwa boda. Ajabu ni kwamba hapa Mwanza maeneo ya bata watu wanajumuika kama kawaida wakila maisha. Clubs zimeendelea kama kawaida. Kutembeleana na kuchepukiana ni kama kawa.

Hata viongozi wa umma wameendelea kukusanya waru kama kawaida licha ya wao wenyewe kutoa tahadhari. Kiufupi hapo tumefeli. Kwa kushindwa kulimudu hili hata kufungwa kwa mashule na vyuo kunaonekana kama ni bure tu ya kuhamisha mkusanyiko sehemu B na kuupeleka sehmu A. Mwisho wa siku mwanafunzi analetewa virus na baba aliyeenda bar weekend kula kinywaji au mjomba alikuja kumsalimia mwanafunzi katika likizo ya Corona.

Watu wametoa excuse kwamba hatuna budi kutoka kujitafutia kiipato na mlo watanzania wanyonge. Lakini mbona mnakusanyika maeneo mengi isivyo na ulazima?

Kunawa mikono
Hapa pia kuna vituko vyake,imekuwa kama fasheni tu. Leo katika pitapita nimekutana na sehemu 3 unanawa maji bila sabuni. Ofisi zingine unapita tu sanitaiza imeisha zaidi ya siku 2.

Jamani watanzania idadi inazidi kuongezeka badala ya kupungua. Nini hatima yetu dhidi ya corona? Mnataka mpaka polisi wawekwe mitaani kutuzuia kutoka?
 
Wanabodi,
Tumeona hali inavyozidi kutisha kutokana na ugonjwa huu wa Corona. Nchi zenye uchumi mkubwa duniani zimechukua hatua za kupunguza mikusanyiko na hata kulazimu wananchi watulie majumbani kuepusha kusambaa kwa ugonjwa huu.....

Kwa hapa tulipofikia, ni wakati sasa Serikali kuchukua hatua ya kupunguza mikusanyiko.
Kama tunavyoona kwa majiji makubwa hapa Nchini, Wamachinga ndio wafanyabiashara wanaosababisha kikusanyiko barabarani, watu wanagusana na kupishama kwa shida.

Jana nimepita mtaa wa Congo Kariakoo, kiukweli hapapitiki, njia zimebana. Hii inamaanisha kwamba, mtu mmoja au machinga mmoja akiwa na ugonjwa huu, basi ni asilimia kubwa watapataa maambukizi.

Nashauri Serikali, hatua ya kwanza ni kuwaondoa Wamachinga wote Mjini, wabaki wenye maduka tu. Vilevile hata katika kufanya manunuzi dukani kuwekwe utaratibu wa kuachiana nafasi ukiwa upo dukani.

Tuchukue hatua sasa.
 
Ugonjwa ushaingia lakini ukiangalia jinsi mikusanyiko ya watu katika maeneo mbali mbali unaingiwa na hofu kuwa hali itakuwaje hili gonjwa likijipenyeza katika mikusanyiko hiyo

Hapa nataka wambia viongozi wetu wa kiroho kuwa hali imekuwa mbaya kuna ubaya gani endapo makanisa na misikiti ikafungwa kwa kipindi hiki cha mpito, waumini wakasalia majumbani kwao wakiendelea na ibada

Viongozi wetu mnaweza jiongeza nyie msisubilie serikali ikataze ndio muache mnaweza jiongeza nyie wenyewe siyo mpaka serikali itamke.
 
Kwenye ibada ndipo kulipo na solution angalia walikofunga ibada maambukizi yalivyo makubwa
Tusiende mbali apa tu Rwanda maambukizi yamefika watu 70 uko paka saivi

MUNGU ndio atakuwa suluhu kwetu watanzania
 
Dini biashara, hakuna biashara bila watu. Kiongozi mmoja akadiriki kusema makanisa yakifungwa watu watakufa.
 
dini
misibani
harusi
mtaa wa congo

angalau waanze kuweka soft control japo naamini Corona sasa imeshatoosha itaanza kupungua na baadaye kidogo miezi kama miwili ijayo haitakuwa tishio.
 
Hao watu wanaoenda huko makanisani ina maana wao hawajasikia kwamba kuna ugonjwa? Au wao hawana akili mpaka watangaziwe kwamba kanisa limefungwa
 
Hao watu wanaoenda huko makanisani ina maana wao hawajasikia kwamba kuna ugonjwa? Au wao hawana akili mpaka watangaziwe kwamba kanisa limefungwa
Kiongozi mumini anamsikia sana kiongozi wake uoni watu wanambia kanyageni mafuta fanyeni hivi nk, wanafanya kwaiyo kiongozi akisema mkija humu kwenye ibada hampati corona wanamini kwaiyo inaitajika busara itumike kuna vitu vingine mungu naye anakushangaa, hili la corona halitaji ujanja ujanja inabidi masharti yafuatwe

Ona italy ndio alipo papa na tunajua uwezo wa kiimani wa papa je kwashindwa hata oteshwa dawa nini ila wanakufa watu kama nini kwaiyo tuwe makini
 

Mimi nna mwaka wa pili sasa sijakanyaga kanisani lengo likiwa ni kujiepusha na mikusanyiko inayoweza kupelekea maambukizi. Kuna mambo mtu unatakiwa ujiongeze mwenyewe sio mpaka usubiri matangazo
 
Unafunga kanisa na msikiti wakati watu wanaenda sokoni, kazini, wanapanda daladala, baa wanaenda, si bora uache tu hzo nyumba za ibada watu wakatubu

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia uko sokoni na kwingineko nani anaweza kusema wakatii jibu ni serikali hakuna mtu anayeweza kusema soko nk vikafugwa, ila uku kwenye imani viongozi wa imani wakisema hata serikali haiwezi waingilia kwaiyo panapowekezana pashughulikiwe
 
Sadaka sadaka sadaka.....mambo ya fwedha!

Everyday is Saturday..................... 😎
 
Kwenye ibada ndipo kulipo na solution angalia walikofunga ibada maambukizi yalivyo makubwa
Tusiende mbali apa tu Rwanda maambukizi yamefika watu 70 uko paka saivi

MUNGU ndio atakuwa suluhu kwetu watanzania
Ghana ilikua na kesi 6 za maambukizi ya korona. Raisi akaitisha kikao na wachungaji pamoja na masheikh kwa ajili ya kuomba, siku zilizofuata waathirika waliongezeka hadi kufikia kesi 62 za maambukizi

Raisi hakuchoka akawataka wananchi wote wafunge na kusali, na siku zilizofuata ilifikia kesi 132 za maambukizi

Hapo ndipo watu wakajua kua Sky daddy is not a doctor

Bible & Quran has mentally destroyed the black race
 
According to you your right
😁😁😁
 
tetesi ni kuwa tabata kimanga kuna proven cases.

ajabu leo kimanga kuna gulio na watu wanapishana kama mtaa wa congo.

je serekali inajali watu wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…