OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wabongo ambao majina yao hajakujulikana wakiwa kwenye mkusanyiko usio wa lazima
Kama kawaida ya watanzania bila kujali hali za maisha ni watu mfano wa kenge ambae kusikia kwake ni mpaka atoke damu masikioni kwa kupigo.Mwendelezo wa kukosa usikivu umetokea pia katika vita dhidi ya Corona.
Wakati ambao serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti kuenea kwa Corona,hatua hizo zimeonekana kupuuzwa mapema kabisa.
Serikali imeagiza tuchukue hatua kubwa 2,kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na usafi wa mara kwa mara hususani kunawa mikono kwa sabuni.
Mikusanyiko isiyo ya lazima imepuuzwa kabisa na watu wanaendelea na maisha kama vile hakuna kitu kimetokea. Wiki hii nilikuwa na safari ya kikazi,safari ambayo ilikuwa inanilazimu kula bar. Kwa uoga ba tahadhali nilikuwa nalazimika kuagiza chakula kwa boda. Ajabu ni kwamba hapa Mwanza maeneo ya bata watu wanajumuika kama kawaida wakila maisha. Clubs zimeendelea kama kawaida. Kutembeleana na kuchepukiana ni kama kawa.
Hata viongozi wa umma wameendelea kukusanya waru kama kawaida licha ya wao wenyewe kutoa tahadhari. Kiufupi hapo tumefeli. Kwa kushindwa kulimudu hili hata kufungwa kwa mashule na vyuo kunaonekana kama ni bure tu ya kuhamisha mkusanyiko sehemu B na kuupeleka sehmu A. Mwisho wa siku mwanafunzi analetewa virus na baba aliyeenda bar weekend kula kinywaji au mjomba alikuja kumsalimia mwanafunzi katika likizo ya Corona.
Watu wametoa excuse kwamba hatuna budi kutoka kujitafutia kiipato na mlo watanzania wanyonge. Lakini mbona mnakusanyika maeneo mengi isivyo na ulazima?
Kunawa mikono
Hapa pia kuna vituko vyake,imekuwa kama fasheni tu. Leo katika pitapita nimekutana na sehemu 3 unanawa maji bila sabuni. Ofisi zingine unapita tu sanitaiza imeisha zaidi ya siku 2.
Jamani watanzania idadi inazidi kuongezeka badala ya kupungua. Nini hatima yetu dhidi ya corona? Mnataka mpaka polisi wawekwe mitaani kutuzuia kutoka?