Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Usijali Mungu anatulinda sana sisi watanzania maana anajua kuwa serikali yetu imelala

Na ndio maana kila siku tuna wagonjwa 13 juzi ndio walifika 19 mmoja kafa 5 wamepona tumerudi palepale wagonjwa 13 kwa hiyo usijali we endelea na mambo yako tu hayo mambo ya corona muachie bi ummy Mwalimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa nikitafakari hawa viongozi wa madhehebu yetu ya ibada, kwa huu milipuko wa ugonjwa wa Corona (Covid-19) wamekuwa wakiendelea na ibada na swala kama kawaida huku wakijua ni hatari kubwa kwa afya za waumini wao na mikusanyiko hiyo inaweza kuwa chanzo Kikubwa cha ongezeko la maambukizi kwa waumini.

Tunajua kuwa Serikali bado haijapiga marufuku mikusanyiko ya ibada, lakini katika kusaidia juhudi za serikali kukabiliana na hili kanga, kwanini wasinge sitisha ibada na swala hadi hili janga litakapokwisha?

Kuna haja gani ya kuwa na mikusanyiko kwa kipindi Hiki? Pongezi ziende kwa baadhi ya viongozi waliofunga Misikiti, Mungu awabariki kwa kujali maisha ya watu.
 
Mungu aendelea waalifunga miskiti kwa uzalendo wao. Uzalendo ni hali ya mtu kupenda maisha ya watu kuliko pesa,mali yake
 
Mikusanyiko ibadani inaweza kuhatarisha maisha ya waumini.
Kwetu Tanzania pick ya corona inakuja,kwa uzembe unaoendelea Mungu atunusuru
 
Kuna kufanya jambo huku ukiwa unaamini hivyo katika unachofanya na kuna kufanya jambo ili tu uonekane na hauko nyuma na wewe unafanya hilo jambo.

Sasa afrika tunataka tu tuonekane kuwa nasi hatuko nyuma kwenye mapambano dhidi ya korona,Italy Spain na America wote hao tunaambiwa walidharau hawakuchukua hatua za kuzuia corona isiingie kwao ndio maana et corona imeingia na kuleta athari.
 
Mwananchi jali maisha yako binafsi na familia yako,huko msikitini,kanisani sijui wanasiasa hawajali chochote khs wewe na ustawi wako.
 
Leo Waziri wa Afya ametangaza virusi hatari vya Corona kuwepo nchini mwetu. Mgonjwa mmoja amethibitishwa kwa vipimo vinavyofanywa kwenye maabara moja tu hapa nchini kwetu.

Maana yake kuna uwezekano wa kuwepo wengine wenye virusi hivyo ambao hawajabahatika kufanyiwa vipimo hivyo au ni carriers.

Cha ajabu, baada ya tangazo hilo, kiongozi wa chama kimoja kikubwa cha siasa katangaza kufanyika mikutano ha hadhara nchi nzima kila siku bila kikomo kuanzia wiki ijayo hadi Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Tusifanye mzaha na virusi hivi vya Corona. Na vikiendelea kuwepo hata Uchaguzi mkuu wa mwaka huu lazima tutauahirisha.

----
Serikali ipige marufuku machinga mjini



-----
Misongamano kwenye usafiri wa umma idhibitiwe


----
Maeneo ya kufunga na mambo ya kuzuia ili kuepusha coronavirus Dar es Salaam
Mbona Bashite anawakusanya watu bila kukemewa?
 
Vita dhidi ya corona haina chama wala dini wala ukabila. Kuna uwezekano hata ibada za siku kuu za Pasaka mwaka huu hazitakuwepo.

Huko Italy na Vatican, wananchi wote wako under house quaranteen (hawatoki nje ya nyumba zao) isipokuwa watoa huduma wa hospitalini tu na polisi. Sisi tunataka kufanya maandamano na mikutano ya hadhara isiyo na kikomo kila siku kama ile ya UKUTA ya 2017! Hata jumuiya za kimataifa zitatushangaa!
Mbona nyie CCM huwa mnaingiwa na kiwewe na mikutano ya Chadema? Si siku zote mnasema Chadema haipo tena?
 
Serikali ichukue hatua za haraka kuzuia jumuia za wakristo majumbani ili kudhibiti usambaaji wa Corona. Familia zetu nyingi si wakweli zinaweza kuwa na mgonjwa ndani na zitamficha eti kuogopa lawama ya kumtenga ndugu, wiki iliyopita familia huko Kenya ilifiwa na ndugu yao huko marekani cha ajabu wanafamilia walikuwa wakitaka maiti iletwe ili wamzike ndugu yao! Hapa zipo familia zinazoficha wagonjwa majumbani na inawezekana hata baadhi ya nyumba wanakokutana wanajumuia wamo bila kujulikana kwa wanakikundi wengine wa jumuia husika, kwa Corona kitendo hicho kinaweza kusababisha kusambaa Corona mitaani.
 
Serikali ichukue hatua za haraka kuzuia jumuia za wakristo majumbani ili kudhibiti usambaaji wa Corona. Familia zetu nyingi si wakweli zinaweza kuwa na mgonjwa ndani na zitamficha eti kuogopa lawama ya kumtenga ndugu, wiki iliyopita familia huko Kenya ilifiwa na ndugu yao huko marekani cha ajabu wanafamilia walikuwa wakitaka maiti iletwe ili wamzike ndugu yao! Hapa zipo familia zinazoficha wagonjwa majumbani na inawezekana hata baadhi ya nyumba wanakokutana wanajumuia wamo bila kujulikana kwa wanakikundi wengine wa jumuia husika, kwa Corona kitendo hicho kinaweza kusababisha kusambaa Corona mitaani.
Watanzania bado hawajachukulia serious huu ugonjwa nakushauri tu jiwekee Isolation mwenyewe usisubiri mtu akutangazie, kama unajijali fanya maamuzi mwenyewe,
#This too shall pass#

The best Medicine of Corona is to Stay Home.
 
Waeleze viongozi wakuu aka makada wa CCM waache kukusanyika.

Wanasahau hilo hasa kama diwani wa upinzani kahamia CCM NK. Mliona kule CHATO!!!!!!!!
 
Katika kupambana na corona, Tanzania tumekuwa tofauti sana na wenzetu kiasi kwamba unajiuliza kama ile dhana ya dunia ni kijiji ina-apply katika nchi yetu.

Tumekuwa very selective katika kuamua ni aina gani ya mikusanyiko ipigwe marufuku na ipi iachwe wakati ukweli unabaki mikusanyiko ni mikusanyiko bila kujali nature ya mikusanyiko hiyo.

Kwa mfano,tunajidanganya sana kwa kujifanya wacha Mungu kwa kutozuia mikusanyiko katika nyumba za ibada kwa imani eti tusioogope huu ugonjwa mpaka tukashindwa kwenda kumuomba Mungu wakati unaweza kumuomba Mungu hata nyumbani kwako na akakusikiliza hasa katika kipindi hiki cha hili janga.

Sasa, wakati tumeacha kudhibiti baadhi ya mikusanyiko huku idadi ya wagonjwa ikiongezeka,ni jambo la kushangaza kuona tumeshindwa hata kuzuia mikusanyiko kwenye mabaa ambapo watu wanajazana na huku wakinywa kwa pamoja katika meza moja kanakwamba hatuna tishio la corona.

Kwa hakika tunashangaza sana, ila muda si mrefu tutavuna tunachopanda kama Taifa.
 
Back
Top Bottom