Lazima watakuwa walitushanga kama keli tulifanya hivyo. Kosa nikurudia kosa.Vp tuliporuhusu ndege iliyoleta wachina, hizo jumuiya hazikutushangaa?
Sent using Jamii Forums mobile app
mtanzania bwana ni mtu mmoja wa propaganda sana, kipindi kile aliwaponda sana ndugu zetu waliopo China muda wote ni utani utani tu, lakini kama ndugu zetu waliopo China Bado wana survive basi huu ndio muda wakuwauliza wao wana survive vipi huko walipo.Vitu vingine ni vya kufikirika japokua vingine sijui ulikua serious ama?
Yaani mt
mtanzania bwana ni mtu mmoja wa propaganda sana, kipindi kile aliwaponda sana ndugu zetu waliopo China muda wote ni utani utani tu, lakini kama ndugu zetu waliopo China Bado wana survive basi huu ndio muda wakuwauliza wao wana survive vipi huko walipo.
Acha kutisha watu,Kwa tulipofika sasa, adui yetu Mkubwa si COVID-19 bali hofu. Watu wameingiwa na hofu kubwa, kila kitu kimesimama. Watu wamevaa Masks mpka kwenye Private cars Tena wakiwa peke yao. Lakin kwa mujibu wa Taratibu na ushauri Toka WHO, Masks zinatakiwa kuvaliwa endapo unazungumza na mtu mwenye kikohozi. Wengine tuendelee kunawa mikono kwa maji safi na sabuni. Pia, tukumbushe kufuta surfaces zote kwa kutumia Alcohol based Sanitisers. Uingiapo ofisini, safisha vitasa, mipango, meza, computer and everything utakachokigusa vifute kwa Sanitersa au Deltol. Otherwise, let's be cool and calm, this too shall pass.
Ndio hapo SasaMimi wananiudhi, walikataa wanafunzi wetu walioko China wasirudi Tanzania kuogopa Corona ila wanaachia watu kutoka nje freely....it doesn't make sense..
Kama umemsikia vizuri: huyo dada akiwa anajua ana virusi vya corona alitembelea Uingereza, Uswizi na Ubelgiji huko ulaya. Kote huko ulaya alikopita hawakuweza kumgundua. Kuna uwezekano akiwa huko Ubelgiji alimtembelea kamanda wetu wa huko na kumpa mkono na kumu hug. Mungu apishe mbali kama tetesi hizi ni za kweli.Dr Akili,
Mikutano ya hadhara kila siku bila kikomo. Ndio tamko lilivyo ama Dr umeongeza kidogo? Kati ya tamko la mikutano na taatifa ya kuwepo mgonjwa ni hipi ilitangulia? Mzaha ni pale mamlaka inapokosa vipimo vya uhakika adi kupelekea mgonjwa kujitangaza mwenyewe kwamba nimuathirika.
Mtu anaingia nchini kutokea nchi iliyo na taarifa za kuwepo kwa corona halafu mamlaka inamuacha anajichanganya na watu wengine, anachukua taxi adi hotelini anapumzika kwanza halafu ndio anajitambulisha. Halafu anakwenda kuchukuliwa hotelini na msafara utadhani ni mualikwa mahala flani, we unaona sio mzaa huu?
Huyu dada akipona inatakiwa atoe maelezo ya kina kwanini ameamua kuliingiza taifa katika janga zito. Kwa sababu maelezo yanaonyesha alijua kwamba afya yake haiko salama kutokana na kwamba nyumbani kwa mwenyeji wake anakotoka kulikuwa na mgonjwa wa maambukizi ya corona.
Unawaza pumba mkuu,Nisizunguke sana.
Stieglers gorge ina wafanyakazi wasiopungua 3,000 mpaka sasa na kuna mchanganyiko wa wageni wengi toka china na Misri.
Na huwa wanachukua likizo baada ya miezi mitatu wanaenda makwao na kurudi kwa sababu viza zao ni za miezi mitatu mitatu. Nina mashaka wanaweza kuwa wamerudi na virusi.
Tukumbuke wafanyakazi wa huu mradi wapo wanaolala site na wengine wanaingia na kutoka kila siku.
Kwa SGR vivyo hivyo inaje gwa na wageni na muingiliano na mkusanyiko wa raia ni mkubwa pia.
Serikali ikiwasikiliza baadhi watoa pumba kama hizi, tutajikuta tunarudi nyuma,Tuwaze kabla ya kutoa maoni. Corona sio mwisho wa kila kitu hivyo shughuli za kiuchumi lazima ziendelee lakini tutafute namna ya kudhibiti maambukizi. Sijui umewaza Nini kushauri Serikali isitishe mradi mkubwa Kama SGR kisa tu Kuna wachina na waarabu? Kwani Corona ipo kwa wachina na waarabu pekee?