Dr Akili,
Mikutano ya hadhara kila siku bila kikomo. Ndio tamko lilivyo ama Dr umeongeza kidogo? Kati ya tamko la mikutano na taatifa ya kuwepo mgonjwa ni hipi ilitangulia? Mzaha ni pale mamlaka inapokosa vipimo vya uhakika adi kupelekea mgonjwa kujitangaza mwenyewe kwamba nimuathirika.
Mtu anaingia nchini kutokea nchi iliyo na taarifa za kuwepo kwa corona halafu mamlaka inamuacha anajichanganya na watu wengine, anachukua taxi adi hotelini anapumzika kwanza halafu ndio anajitambulisha. Halafu anakwenda kuchukuliwa hotelini na msafara utadhani ni mualikwa mahala flani, we unaona sio mzaa huu?
Huyu dada akipona inatakiwa atoe maelezo ya kina kwanini ameamua kuliingiza taifa katika janga zito. Kwa sababu maelezo yanaonyesha alijua kwamba afya yake haiko salama kutokana na kwamba nyumbani kwa mwenyeji wake anakotoka kulikuwa na mgonjwa wa maambukizi ya corona.