Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Moja kwa moja kwenye mada, obvious siioni mantiki ya kufunga shule tu na kuacha vyuo, maana vyuoni pia kuna mkusanyiko mkubwa sana wa watu.. Na kama mambo za mabweni yapo kama kawaida..
Vyuo kama vya ualimu, kilimo, afya na kozi mbalimbali wanachuo wamelundikana vyuoni.

Ombi langu kwa serikali ni kwamba fungeni mpaka vyuo kwa huu mda wa mwezi mmoja hapo nitaona mantiki ya hili suala.
Ila kwa ujumla tu, tuendelee kumwomba ALLAH atuepushe na hili janga.
INSHAALLAH
 
I think the first step is to take precautions of or kids below 18.

Nyie wazee mna akili zenu bananeni huko wee kwenye mapantoni na madaladala ila mkirudi majumbani moja kwa moja kuoga na sabuni yenye sanitation.

Kwanza mmezeeka hata mkifa Taifa halina hasara sana...ha ha ha
 
Naomba uzi huu usiungwe...

Natambua hatua ambazo Serikali Inachukua kuepusha kuenea kwa maambukizi ya Virusi wa Corona

Lakini Kuna ushaghalabaghala wa Usafiri wa daladala Dar naona Serikali haisemi chochote na mle tunasafiri watu kibao wana Mafua na wanapiga chafya za hatari...So inakuwaje?

Hivi ukifunga shule, halaf utaratibu wa hovyo wa usafiri wa Umma Dar ukaachwa uendelee kama ulivyo si Serikali inakuwa inajitaabisha tu?

Naona serikali kama imejigusagusa tu lakini inashindwa kuchukua hatua madhubuti kwa ujumla wake..

Na hata sijasikia waseme chochote kuhusu kufunga Viwanja vya Ndege...

IT SHOULD BE A TOTAL LOCKDOWN ...wanahofia kukosa mapato? We cannot prioritize money over lives, Come on guys!
Kwani kuhusu usafiri wa umma unatakaje? Serikali imnunulie kila mwananchi usafiri wake au?
 
Baada ya Corona kuingizwa Arusha na mrembo na tajiri mwenye shule za binafsi, sasa muda wowote itaingia Dar kupitia wasanii wa Bongo Fleva wanaotoka kupiga Show ulaya.

Ili kuzuia hatua zifuatazo zichukuliwe leo hii:

1. Harusi zote zisitishwe

2. Misiba wahudhurie ndugu tu, wasizidi 20.

3. DART-mwendokasi upigwe marufuku

4. Machinga wote waliozagaa mjini kwa tamko la JIWE waondoshwe na kurudishwa makwao.

5. Mabasi yaendayo nje ya nchi yasitshe safari.

6. JKT WARUDISHWE NYUMBANI.

7. MAHABUSU WOTE NA WALE WALIOPO VITUONI WAPEWE DHAMANA

8. KWARESMA NA NJIA YA MSALABA IPIGWE MARUFUKU

9. BEACH ZOTE ZA UMMA zipigwe marufuku.

10. Betting offices zifungwe

11. Wale makahaba wote wa Sinza, Buguruni walipwe fedha/ruzuku, ili wakae nyumbani.

12. Kupanda daldala iwe LEVEL SEAT, NA KUINGIA KWA FOLENI/MSTARI na kila mtu alipe kwa tigo pesa.

13.Traffic akikukamata hakuna kumpa leseni, wataeneza ugonjwa.

14. Gest houses zote zifungwe na zibaki hoteli tu.

15. CCM LUMUMBA vile vijiwe vya kahawa vifungwe vyote
Umeshau vivuko vya Ferry kigamboni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM imesitisha shughuli zote za chama ambazo zinahusisha mikusanyiko ya watu wengi.

Mh Polepole amewaomba viongozi wote wa dini kumuomba mwenyezi Mungu atuepushie balaa hilo.

Source ITV habari

My take; Chadema waige mfano wa CCM kwa kuweka siasa pembeni kwa sasa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Vyuoni wapo watu wazima wanaojua hata matumizi ya kondomu wanajua namna ya kuishi kwa tahadhari.
Mkuu, huu ugonjwa hauna mtu mzima wala mtu mdogo.. Kwani muathirika was Corona unaweza kumjua kwa macho..?
Maana kuna watu wameambukizwa hyo corona na hawajijui..
That is serious issue, so serikali iliangalie hili
 
Back
Top Bottom