Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Kwenye vita hii hayo maji hayaruhusiwi. Hata kuhudhuria ibada za kanisani na misikitini hairuhusiwi. Ni kubaki nyumbani tu. Simu za mkononi ni petri dish za corona. Ukinawa mikono halafu unashika simu yako (ambayo hujainawisha na huwezi kuinawisha) work done inakuwa zero! Hivyo baki nyumbani kwako tu.
Simu waweza isafisha Kwa sanitizer Na isipate madhara
 
Kwa nguvu kubwa ya tahadhar dhid ya corona nje na ndan ya nchi. Je sio wakat muafaka wa kutojaza kwenye mabas hasa MWENDOKASI? naona bado ni pomoni pomoni. Au sisi Tz tuna ka immunity flan!
Htr
Screenshot_20200316-160536_WhatsApp~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vita dhidi ya corona haina chama wala dini wala ukabila. Kuna uwezekano hata ibada za siku kuu za Pasaka mwaka huu hazitakuwepo. Huko Italy na Vatican, wananchi wote wako under house quaranteen (hawatoki nje ya nyumba zao) isipokuwa watoa huduma wa hospitalini tu na polisi. Sisi tunataka kufanya maandamano na mikutano ya hadhara isiyo na kikomo kila siku kama ile ya UKUTA ya 2017! Hata jumuiya za kimataifa zitatushangaa!
Huyu anayetembea na magari karibu mia hafanyi misongamano ?!. Mbona mkikaa akili inawarudisha Cdm tu ?!. Hukumbuki kuwa Mbowe ameongea kabla ya Ummy !! Kosa lake liko wapi ?!. Je na yule aliosema hasubuhi kuwa Tz hakuna Corona tumhukumu !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka picha mkuu uzi bila picha haunogi inaonekana ni uongo weka kapicha tuone
Mkuu unataka na picha ya mwendokas kujua kama inajazaga kupitiliza kweli? Nilidhan mambo ya picha yanaishia mkono wa Mdee
 
Waachwe wakafanyie hukohuko kwao wapukutike hiyo kanda ipigwe vizuizi kama Wuhan tu! Hakuna kutoka mtu.

Na habari njema ni kwamba waliokuwa wanaomba mdudu aje kaanzia hukohuko kwao!

Who cares!
 
Vita dhidi ya corona haina chama wala dini wala ukabila. Kuna uwezekano hata ibada za siku kuu za Pasaka mwaka huu hazitakuwepo. Huko Italy na Vatican, wananchi wote wako under house quaranteen (hawatoki nje ya nyumba zao) isipokuwa watoa huduma wa hospitalini tu na polisi. Sisi tunataka kufanya maandamano na mikutano ya hadhara isiyo na kikomo kila siku kama ile ya UKUTA ya 2017! Hata jumuiya za kimataifa zitatushangaa!
Kwa janga hili Mbowe asubiri kwanza lipite ndo tutakuja kwenye mikutano yao,Kwa sasa hivi Wawe wanarecod kwa sana clip za kampeni wanatupia hizi Hazina cha intelligence ya polisi zisiwe za uchochezi tu.Pia ccm imeshawafanyia kampeni tosha Kwa kutusomesha namba mwaka wa tano sasa ccm haina jipya nje ya ndege, sgr,stiglers
 
Mods nadhani ifike mahali turuhusiwe kutukana watu kama hawa,we boya nani alianza kufanya mkutano kati ya mbowe na ummy?
Vita dhidi ya corona haijaanza leo. JPM kaanza kabla ya hapo kutanganza vita hii na vyombo vyetu vya habari viliitikia vizuri na vimekuwa vikiitangaza. Mbowe alipaswa kuwa analijua suala hili. Halijaanzia kwa Ummy.
 
Corona is a real disaster and I mean a real Catastrophe but it is sooo overrated.
Na Hii ni kwa sababu ya fast flow of information through social media
Kama Vile JF. Some " wanatengeneza " fake news ili tu kuinstall Panick.

Naimagine UKIMWI ndo Ungekuja kipindi Hiki Cha Globalization.....
Sijui Ingekuwaje!

Taylor Swift - You Need To Calm Down!
 
Mipango itaendelea tu labda mzuie mawasiliano. Kama univesities lectures zinaendelea on line seuse mawasiliano ya Mwamba na wanachama 😂
Tangu lini hayo mawasiliano ya mtandaoni mliyasitisha? Si Mwamba kaona hayatoshi na ndipo kaagiza muingie mitaani kupambana na polisi na kusambaza corona?
 
Kwa taarifa tu ni kwamba mgonjwa ili aweze ku survive na Respiratory Distress Syndrome ya corona anahitaji mashine ya kupumulia (automatic ventilation machine) kwa muda wa wiki nne akiwa ICU. Nchi kama Italy yenye mashine za aina hizo zipatazo elfu tano imeshindwa kuwamudu wagonjwa hao wa corona. Imelazimika kuwapatia mashine hizo vijana tu wenye umri wa miaka isiyozidi 45 ambao uwezekano wa kupona ni mkubwa. Wazee wanaozidi umri wa miaka 45 imebidi waachwe tu wajifie zao.

Sisi ambao mashine hizo tunazo zisizozidi mia moja tutegemee nini kama mlipuko huo utafika kiwango cha Italy? Hivyo ni muhimu sana kwetu tukaudhibiti mapema ugonjwa huu kwa nguvu zetu zote ili usifike kiwango hicho. Tusifanye mzaha. Mikusanyiko ya watu tusiruhusu. Mbanano kwenye nyenzo za usafiri tusiruhusu. Safari zisizo za lazima tusiruhusu. Na kadhalika kama itakavyokuwa ikielekezwa na wizara ya afya. Na tumuombe Mwenyezi Mungu atuvushe kwenye janga hili.

Wanasiasa tusikubali watudanganye. Na uchaguzi mkuu wa mwaka huu usiwepo. Tutaufanya baada ya janga hili kutoweka hata kama ni baada ya miaka 10. Hata bunge la bajeti ya mwaka huu lifanyike kwa mtandao (video conference) ambayo pia itatuepusha na malipo ya posho ya vikao vya wabunge inayosemekana ni shilingi takribani laki nne kwa siku kwa kila mbunge mara siku 60 za vikao hivyo vya bunge la bajeti. Tuende kimtandao na hata kama corona itaisha tuendelee kimtandao. Tutaokoa pesa nyingi.
 
Cha muhimu ni kuwa Waziri mwenye dhamana na afya ya Watanzania leo amewataka Watanzania wote kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama wanavyopatiwa taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbali mbali. Aidha, kwa kuzingatia Kanuni ya 46 ya Sheria ya Afya ya Jamii, 2012 (Reg. 46 of the Public Health Regulation (Sanitisation and Hygiene Practices), 2012); waziri wa afya leo kaelekeza mambo yafuatayo:-

I. Watanzania wasiokuwa na safari za lazima, wanashauriwa kwa sasa kusitisha safari zao kwenye nchi zenye maambukizi

2. Amezitaka Taasisi zote zikiwemo Shule, Hoteli, Maduka ya Biashara, Nyumba za Kulala Wageni (Lodges/Guest Houses), Makanisa, Misikiti, Ofisi za Umma na za Binafsi, Vituo vya kutolea Huduma za Afya, taasisi za fedha, vyombo vya Usafiri, pamoja na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, viwanja vya mpira, na vituo vya abiria kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji tiririka na sabuni au maji yenye Klorini kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa mikono. Aidha kwa kadri itakavyowezekana, maeneo hayo yawekewe vifaa maalum vya kuwekea vitakasa mikono (Sanitizer Dispensers)

3. Kuweka maji yenye dawa ya Klorini au vitakasa mikono (hand sanitizers) katika mageti ya kuingilia hifadhini au mahotelini kwa ajili ya kusafisha mikono ya watalii na waongoza watalii wote.

4. Kuweka maji yenye dawa ya Klorini katika Vituo vya Mabasi ya abiria na Mwendokasi kwa ajili ya kusafisha mikono ya wasafiri.

5. Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana, kugusa pua, mdomo pamoja na macho kadri itakavyowezekana.

6. Hospitali zetu amezitaka zihakikishe kuwa ndugu/jamaa wanaokwenda kuona wagonjwa waliolazwa idadi yao isizidi wawili kwa kila mmgonjwa

7. Kutoa taarifa kwenye Ofisi za Afya au Vituo vya Kutolea Huduma za Afya endapo watamwona mtu mwenye dalili za ugonjwa wa COVID- 19

Imetolewa na: Ummy Mwalimu,Mb.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Dar es Salaam.
 
Dr Akili,
Mikutano ya hadhara kila siku bila kikomo. Ndio tamko lilivyo ama Dr umeongeza kidogo? Kati ya tamko la mikutano na taatifa ya kuwepo mgonjwa ni hipi ilitangulia? Mzaha ni pale mamlaka inapokosa vipimo vya uhakika adi kupelekea mgonjwa kujitangaza mwenyewe kwamba nimuathirika.

Mtu anaingia nchini kutokea nchi iliyo na taarifa za kuwepo kwa corona halafu mamlaka inamuacha anajichanganya na watu wengine, anachukua taxi adi hotelini anapumzika kwanza halafu ndio anajitambulisha. Halafu anakwenda kuchukuliwa hotelini na msafara utadhani ni mualikwa mahala flani, we unaona sio mzaa huu?

Huyu dada akipona inatakiwa atoe maelezo ya kina kwanini ameamua kuliingiza taifa katika janga zito. Kwa sababu maelezo yanaonyesha alijua kwamba afya yake haiko salama kutokana na kwamba nyumbani kwa mwenyeji wake anakotoka kulikuwa na mgonjwa wa maambukizi ya corona.
 
Ushauri:

Serikali ifungie night club au club zinazopiga disko ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona. Maana juzi Jumapili nilienda club moja hivi na kwa ule msongamano wa pale ni dhahiri kwamba kama kungekua na mtu hata mmoja ana ugojwa huo basi tungepata wote tuliokuwamo pale na tungerudi nyumbani na kuambukiza familia zetu vile vile.

Najua bado kuna sehemu mbalimbali za kudhibitiwa ila mimi nmeona nianze na hili maana halina ulazima sana na tunaweza kuacha kwenda kwa muda mpaka pale ufumbuzi utakapopatikana duniani (nchini).
 
Back
Top Bottom