Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Hizo ni hatua za awali, na hatua za mwisho ni kubaki nyumbani hakuna kutoka nje, kwa sasa serikali imeshasema tusifanye safari na mikusanyiko isiyo na lazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyani Ngabu,
Kwenye lalamiko hili la huyu jamaa umejibu vizuri sana. Sisi ndiyo tunaofahamu mazingira ya hapa bongo na serikali imeshatoa tahadhari zote na options za kujikinga hata ikasema si lazima uende kazini kama unaweza kufanya kazi online while at home bado wanataka Serikali isimamie hata maisha yao binafsi ikiwemo kupanda daladala. Kweli?
 
Baada ya tangazo la PM kuhusu kuacha kukusanyika bila ulazima kama mbinu ya kujiepusha na kuenea kwa Corona, kuna haja watendaji kuja na orodha ya mikusanyiko isiyo ya lazima na ile ambayo ni ya lazima, vinginevyo taharuki kwa wananchi haiepukiki.

Mfano, je sherehe za harusi ni mkusanyiko wa lazima? Unaruhusiwa?

Je, mule kwenye hotel (Arusha) waliomozuiwa watu kuingia na kutoka hotelini hakuna watu waliokuwa na michepuko ambayo ni wake za watu? Itakuwaje?
 
Harusi ni mkusanyiko usio wa lazima kwa sababu hakuna sehemu inakutaka uhudhurie harusi kwa namna yoyote ile.
 
Mkuu samahani naona ingekuwa vyema kama ungesema serikali izuie mikusanyiko ya watu ila kwa hii kauli yako kuna watu watakushutumu kuwa mbona umezungumzia upande A na Upande B umeuacha?
 
Muda umefika kwa serikali kusitisha makundi ya maombezi kama ilivyositisha makundi mengine, makundi haya huambatana na watu kuanguka na kugalagala chini vinginevyo hao manabii na mitume watakusanya watu ili kuwaponya na kuwakinga na Corona.
Muda si mrefu nimetoka kuongea na muumini ametokea kwenye maombi anasema Mungu atawalinda. Wao hawana cha kuhofu kabisa. Sijui serikai imejipangaje kukabiliana na watu wenye imani kali kama hawa.
 
Vya kufunga ni vingi MBONA nyomi ni kila sehemu hakuepukiki,kuona wagonjwa mahospitalini,kwenye vivuko,masokoni,nyumba za ibada
Ndo maana Ulaya Wamefanya Total Lockdown...kila kitu kimefungiwa, hapa hatuwezi?
 
Harusi ni mkusanyiko usio wa lazima kwa sababu hakuna sehemu inakutaka uhudhurie harusi kwa namna yoyote ile.
Ndugu, marafiki na wanafamilia hawawezi kuacha kuhudhuria kwenye harusi ya mtu wao wa karibu, je huuoni ulazima wa watu hao kukusanyika?
 
Kama wenzetu Rwanda kupiga marufuku mikusanyiko yote katika nyumba za ibada makanisani na misikitini ...........

Tena itapendeza viongozi wa dini wakiungana na serikali yetu kuzuia mikusanyiko katika kipindi hiki chote cha sitofahamu ya ugojwa huu wa corona kama wenzetu wa rwanda

Kama swala la kuabudu kila mmoja abudu nyumbani kwake hivyo

Nawakilisha hoja kwa serikali na viongozi wa dini kuhusu hili swala

Sent using Jamii Forums mobile app
Yale mapagani tunaanza kuyajua sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu, marafiki na wanafamilia hawawezi kuacha kuhudhuria kwenye harusi ya mtu wao wa karibu, je huuoni ulazima wa watu hao kukusanyika?
Ndugu na marafiki wataweza kukuacha uzikwe na manispaa ukifa na Corona.
 
Jeshi lina kazi nyinga, Magereza tu mambo Safi, utakuwa unasikia mifupa inavujika tu kwaaaaa.
 
Back
Top Bottom