Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Kuwa muwazi, hizi semina zimefanyika hoteli gani? Mie nilipita Flomi hotel kulipangwa semina/warsha kumbi 3 gharama za ngos 3 hatahivyo matukio yote matatu hayakufanyika ingawa washiriki walifika hadi kwenye kumbi husika. Huo ni ushuhuda wa kutii amri halali ya SERIKALI
Nimestushwa kusikia Taasisi kadhaa za Umma wakiwemo watumishi wa OR-TAMISEMI NA wizara nyingine wakiendelea na vikao katika maeneo kadhaaa morogoro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa muwazi, hizi semina zimefanyika hoteli gani? Mie nilipita Flomi hotel kulipangwa semina/warsha kumbi 3 gharama za ngos 3 hatahivyo matukio yote matatu hayakufanyika ingawa washiriki walifika hadi kwenye kumbi husika. Huo ni ushuhuda wa kutii amri halali ya SERIKALI

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda ni ramli chonganishi na uchochezi
 
Shemeji kakudanganya.

Sent from my Nokia 6.1 Plus using Tapatalk
 
Ni tegemeo letu sisi Wakristo pia kwamba tutapewa miongozo chanya ya namna ya kuenenda na ibada bila kuruhusu mikusanyiko ya waumini.

Makanisa ya Kenya yamefanya hivyo, Mufti wa Waislamu Tanzania ameshatoa maelekezo kwa waumini wa Kiislamu na sasa tunawasubiri mitume wetu kama Mwamposya, Kakobe, Rwakatare, Gwajima, Mwingira, Gamanywa, Lusekelo na maaskofu wa TEC na CCT.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
johnthebaptist, Tanzania dini ziko nyingi tu!

Sio hizo mbili tu zenye kupimana ubavu kila uchao kutaka kuonekana mmoja ndie yuko sahihi zaidi hata ktk kutoa matamko kuhusu Corona.

Kwakuwa ni dini tofauti kila mtu atatoa tamko kwa wakati wake, hawawezi wote kutoa kwa sekunde moja, labda kama serikali ingeamua ibada za mikusanyiko kwa ujumla zisitishwe kwa muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom