Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Mtu mweusi kubaguliwa na watu weupe ni sahihi kabisa, leo nimeenda mjini watu ni wamevaa barakoa za vitenge ambazo hazizuii maambukizi(according to makamu wa waziri wa Afya) na hata hawajali!
 
Kwa nchi masikini hata maamuzi huwa ni duni sana.

Ugonjwa unachukuliwa kawaida ila haujaanzia kwetu bali umeanza China na baada ya mwezi ukaenea nchi nyingi duniani
Madhara yake tumeyaona tuliopo nje na athari zake zote

Watu wamekufa sana ila na kila siku wanajiongeza na kuona kesho wafanye nini. Suala la kufunga biashara na lockdowns zimefanyika na nchi zingine sasa wameamua kuachia kidogo kidogo.

Hospital zote nchini ziwe na sehemu za kuwaweka wagonjwa wa Corona tofauti maana mtawafungia mpaka store
Mkileta ubishi mtaanza kupalilia mashamba kwa kuzika watu ná mortuary zitajaa wafu.


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ninaumia sana, ninapo ona watu wanakaa magengeni mitaani wanapiga story, wengine wanalandalanda tu, mtaani, wengine wabishi kila kitu wanataka uthibitisho kana kwamba corona inasingiziwa kumaliza watu, waTz hatukuzoea kufa kwa mtutu, au mass, kulingana na historia yetu, nafikiri imetufanya tuwe na mizaha sana, basi wajinga wachache watatufanya tupigane na corona miaka nenda rudi, tushauliane mala ya ngapi ndio tuelewane!

watu hawajali,watu hawana wasiwasi, bora wanao tegemea kipato kila leo, haikwepeki, lakini mtu yupo tu,anadhulula, corona sio mchezo, tutakwisha wote hapa mjini.
 
Habari wadau..

Shule na vyuo vimefungwa kuepusha mikusanyiko.

Kanisani na misikitini wameruhusu mikusanyiko iendelee.. hii inamaanisha nini
 
Back
Top Bottom