Kipimo kinaendelea kufanya kazi. Watu wanapimwa maana ni kati ya requirements za kusafiri nje ya nchi. Tatizo ni kuwa majibu yanaelekea kama vile ni ya kupangwa ili kuonyesha kuwa hakuna huo ugomjwa Bongo!
MENGI yanaweza kuzungumzwa kuhusiana na kadhia hiyo, na wazungumzaji hawaachi kujipambanua na itikadi yake ya kisiasa. Lakini serikali ilishaweka utaratibu wa kupimwa Corona kwa wasafiri wote wanaokwenda nje ya nchi, na wanaobainika kukutwa na maambukizo hukataliwa kusafiri.
Nadhani ili kuukata mzizi wa fitna, tungevuta subira, angalau kwa wiki mbili, muda ambao unatosha kuwafuatilia wachezaji na viongozi wanaodaiwa kukutwa na maambukizo ya virusi vya kama watakuwa na corona, ili tuwe na uhakika wa yale tunayoyajadili, kwani endapo washukiwa hao wataonekana ni timamu kiafya hata baada ya muda huo, tutajua kwamba ni kweli walifanyiwa njama na figisu kwa malengo wanayoyajua wenyewe.
Hata hivyo Mamlaka ya Afya na serikaliilishatahadharisha kuwa kila mtu ana wajibu wa kujilinda, kuchukua tahadhari na kufuata kanuni zote za afya ili kujikinga na janga hili, huku tukimtanguliza MwenyeziMungu!
Lakini kuna baadhi ya watu, ama kwa kufuata mkumbo, kutumika kwa maslahi ya nje, kutojiamini, kushibishwa fikra potofu ama kwa sababu zote hizo, wanadhani uhai wa mtu ni mali ya serikali ama Chama fulani!
Haijakatazwa mtu binafsi, familia na ama ukoo kujifungia ndani ('lock down'), kwa muda wowote anavyoona inafaa kwake au kwao!, bila kuathirika.
Lakini kudhani kuwa suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii haiwezi kupatikana kutokana na fikra, ubunifu na kwa kuzingatia mazingira yetu, ni dalili kuwa bado tunakubali kutawaliwa kifikra na tungali utumwani, tena utumwa mbaya kabisa na wakujitakia.
Matukio ya watu kufariki dunia yalikuwepo na yataendelea kuwepo, hata baada ya kupita kwa janga hili la sasa, kwani Imeandikwa 'Kila nafsi lazima itaonja umauti'.