#COVID19 Vita dhidi ya COVID-19 Angola imetuumbua, Balozi awajibike?

#COVID19 Vita dhidi ya COVID-19 Angola imetuumbua, Balozi awajibike?

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,377
Ndugu zangu tunazidi kuumbuka kuhusu janga la Corona.

Hadi niandikapo uzi huu, msimamo wa Serikali ya Rais Magufuli (si ya wananchi wa Tanzania) ni kwamba hakuna COVID-19 isipokuwa "changamoto ya upumuaji" hivyo basi ni dhambi ya mauti kutamka kuwa kuna "korona" Tanzania hata kama tunapukutika kama nzige wa jangwani waliopuliziwa dawa.

Vijana wetu wa Namungo FC waliondoka hapa nchini (kusiko na korono) kwenda kucheza nchini Angola (Champions Legue). Wamepimwa na kukutwa na ugonjwa huo ambapo ni wachezaji watatu na kiongozi mmoja wamekutwa na Corona. Mchezo wao umefutwa maana timu pinzani hawako tayari kurisk maisha yao. Wamehifadhiwa "jela".

Angola imeitangazia dunia kuwa Tanzania kuna COVID-19 mbele ya Balozi wetu nchini humo. Sasa wanne hao wanarejea nyumbani. Je, ndio wagonjwa wa kwanza hivyo tuwatenge na kuchunguza waliokutana nao kama yule mama wa Arusha mwaka Jana? Au watakapokanyaga ardhi tu ya Tanzania ugonjwa utakauka?

Kwa nini Balozi hakuziambia mamlaka za Angola kuwa majibu yao si sahihi maana hatuna Corona? Je, wanne hao hawatuletei Corona? Nawaza tu nikielekea kumzika Brigadier Mbena!
 
Acha uongo, sio kwamba timu ya angola hawakua tayari kurisk maisha yao ila mamlaka za angola ndio zikezuia hizi team kukutana. Ukisikiliza mahojiano na azam jamaa wanasema wenyeji wao waliwaambia kua serikali yao imekataa hata kuwapelekea msosi tuu.
Uongo upi na ukweli hapo uko wapi.

Wagonjwa wanne, walipogoma kiingia mjengo wa karantini ilibidi timu yetu ifungiwe kwenye bus lao.
 
Tanzania imekuwa kichekesho mbele ya Dunia. Aiseee ingekuwa Hii kitu sio dunia nzima hapo sawa.

Tuache jaman familia zinapoteza wapendwa kwa ajabu sana anafariki mme baada ya siku 2 unasikia mke nae amefariki bila aibu wanasema mstuko. Swali ina maana siku hizi mtu kufiwa na mme au mke ndio kumeanza mpk waongozane? ama ndio walipendena saaaaana?
 
Sijafurahishwa kabisa na unyanyasaji walio fanyiwa hao wachezaji na viongozi wa Namungo Fc. Ni vyema mamlaka zetu nazo zikajipanga ili kuja kulipa kisasi kwa kuwafanyia fitna za kutosha hao kenge iwapo watakuja Nchini mwetu kucheza mechi ya aina yoyote ile. Yaani waliwageuza Watanzania wenzetu kama mbwa vile. Nimekasirika sana!😟

Ila siungi mkono pia ishu ya serikali kupotezea uwepo wa huu ugonjwa. Ni bora hata kile kituo chao cha kupimia sampuli za huo ugonjwa kinge endelea kutumika hasa kwa wale Watanzania wote wanao safiri nje ya nchi ili kuondokana na aina hii ya manyanyaso kwa Watanzania.
 
Too soon to talk about this, ungesubiri CAF watakapokaa kwenye kamati zake na kuamua hatma ya hizo timu ndio uje na huu uzi, inawezekana ni figisu za mpira wa Afrika walizofanyiwa Namungo FC ndio sababu ya mchezo kufutwa.
 
Acha uongo, sio kwamba timu ya Angola hawakuwa tayari kurisk maisha yao ila mamlaka za angola ndio zikezuia hizi team kukutana.

Ukisikiliza mahojiano na Azam jamaa wanasema wenyeji wao waliwaambia kuwa Serikali yao imekataa hata kuwapelekea msosi tuu.
Jeshi!
 
Sijafurahishwa kabisa na unyanyasaji walio fanyiwa hao wachezaji na viongozi wa Namungo Fc. Ni vyema mamlaka zetu nazo zikajipanga ili kuja kulipa kisasi kwa kuwafanyia fitna za kutosha hao kenge iwapo watakuja Nchini mwetu kucheza mechi ya aina yoyote ile. Yaani waliwageuza Watanzania wenzetu kama mbwa vile!! Nimekasirika sana!!😟

Ila siungi mkono pia ishu ya serikali kupotezea uwepo wa huu ugonjwa. Ni bora hata kile kituo chao cha kupimia sampuli za huo ugonjwa kinge endelea kutumika hasa kwa wale Watanzania wote wanao safiri nje ya nchi ili kuondokana na aina hii ya manyanyaso kwa Watanzania.
Kipimo kinaendelea kufanya kazi. Watu wanapimwa maana ni kati ya requirements za kusafiri nje ya nchi. Tatizo ni kuwa majibu yanaelekea kama vile ni ya kupangwa ili kuonyesha kuwa hakuna huo ugomjwa Bongo!
 
Inawezekana Balozi hakupangwa mapema kwa majibu kwa vile, huku kwetu ni propaganda hivyo Balozi zetu nyingi hazijashirikishwa katika "kuelezea nini kinaendelea Tanzania na COVID-19"

Tena Serikali ijifunze kwa hili lilotokea Angola,kwani yawezekana Mabalozi wetu wengi hawajaandaliwa kutoa majibu kwa Nchi wazotuwakilisha!
 
Yaan kwa namna Yoyote ile Angola hawajawatetendea Haki wachezaji wetu na ikibd serikali inabd iliingilie Kat hiki

Ule ni uvunjifu wa Haki za kibinadamu

NB Mimi sio kijni wa Rumumba
 
Angola na Tanzania picha haziendi tokea zamani au na hili nalo hamlijui.
Picha zimesimama tokea zamani ipi? Angola na Tanzania ni "nchi marafiki" hata vyama vya ukombozi vya nchi hizo MPLA na TANU/CCM ni damu damu na wote ni wanachama wa SADEC na AU tokea enzi za OAU. Wapigania uhuru kadhaa wa Angola enzi hizo walikuwa hosted Tanzania.
 
Back
Top Bottom