Ndugu zangu tunazidi kuumbuka kuhusu janga la Corona.
Hadi niandikapo uzi huu, msimamo wa Serikali ya Rais Magufuli (si ya wananchi wa Tanzania) ni kwamba hakuna COVID-19 isipokuwa "changamoto ya upumuaji" hivyo basi ni dhambi ya mauti kutamka kuwa kuna "korona" Tanzania hata kama tunapukutika kama nzige wa jangwani waliopuliziwa dawa.
Vijana wetu wa Namungo FC waliondoka hapa nchini (kusiko na korono) kwenda kucheza nchini Angola (Champions Legue). Wamepimwa na kukutwa na ugonjwa huo ambapo ni wachezaji watatu na kiongozi mmoja wamekutwa na Corona. Mchezo wao umefutwa maana timu pinzani hawako tayari kurisk maisha yao. Wamehifadhiwa "jela".
Angola imeitangazia dunia kuwa Tanzania kuna COVID-19 mbele ya Balozi wetu nchini humo. Sasa wanne hao wanarejea nyumbani. Je, ndio wagonjwa wa kwanza hivyo tuwatenge na kuchunguza waliokutana nao kama yule mama wa Arusha mwaka Jana? Au watakapokanyaga ardhi tu ya Tanzania ugonjwa utakauka?
Kwa nini Balozi hakuziambia mamlaka za Angola kuwa majibu yao si sahihi maana hatuna Corona? Je, wanne hao hawatuletei Corona? Nawaza tu nikielekea kumzika Brigadier Mbena!