Mbowe uliwatuhumu wabunge wa CCM kuhongwa lakini hukutoa details zaidi ila leo hii unatuhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Zitto ulisema wabunge wa upinzani kwa idadi yenu mnaweza kuanzisha mchakato wa kumvua madaraka mh.sana ila ukaishia hapo lakini jana umelalamika kutaka kukamatwa tena utakapotoka nje ya viwanja vya Bunge.
Na wewe askofu Gwajima ulimtuhumu Dr.Mihogo kuhusiana na mzigo wa huko Afrika kusini ila ukaishia hapo lakini leo umetajwa katika orodha ya watuhumiwa wanaohusika na madawa ya kulevya.
Kauli kwamba kile kivuko sasa ni mali ya jeshi na mnaohojiji mjue hivyo sio ya kuachwa ipite hivi bali inapaswa kuhojiwa na inabidi mpambane kama Tundu Lissu kama kweli mnataka kushika dola.
Hivyo wakati nyinyi mkiwa softy katika misimamo yenu,wenzenu wanafanya hayo wanayoyafanya tena kwa kuwanika hadharani.
Nachowashauri ili kuheshimiana na kila mtu aonye uchungu wa siasa chafu na kutuhumiana kwa style hii,
Wenzenu wakimwaga ugali,na nyinyi mwageni mboga kama alivyofanya Msukuma jana.
Acheni kulalamika tumieni power yenu na ikiwezekana hata kashifa za Escrow hasa waliochota mabilioni kupitia benk ya stanbic kama mnawajua muwataje ndani ya Bunge ambao mna kinga ya kutoshitakiwa na maazimio ya Bunge kuhusu hii kashifa muyafufue upya..