Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Hivi kweli sisi Watanzania ni wakudanganywa kila mara! Tatizo la ukame na njaa linawekwa kapuni kwa kujadili madawa ya kulevya! Sikumbuki ni kashfa gani iliikumba serikalini, awamu IV mara fikra na mawazo yakahamishwa hadi Loliondo kwa Babu, vyombo vya habari vyote vikaacha kujadili issue muhimu na kugeukia kikombe cha Babu. Viongozi kadhaa walionekana wakinywa kikombe cha Babu kwanza ....alafu misururu ya Watanzania wagonjwa ikafuata, mjadala muhimu wa kitaifa ukasahaulika. Wadanganyika bwana, kweli ni Wadanganyika!
 
"Makonda hana ushahidi anakurupuka tu na kutaja watu awachafue ili apate umaarufu"

"Makonda ana ushahidi wa kila kitu juu ya anaowatuhumu, ndiyo maana akajiamini na kuwataja"

Hivi ni nani anayejua kama Makonda hana ushahidi wa kile anachokiongea juu ya wafanyabiashara na watumiaji wa madawa ya kulevya? Hebu aweke ushahidi wake hapa kuonesha yule RC anakurupuka.

Hivi nani anajua Makonda anao ushahidi juu ya yale anayoyaongea? Auweke basi tuuone . TUACHE KUDHANI

Ifike mahali watanzania tupunguze kujifanya tunajua kwa mambo ambayo hayapo ndani ya uwezo wetu. Si kila jambo la kulipigia domo na kulidhania tu kisa mawazo yako yamekwambia. Sote hatujui kama Makonda ana ushahidi au hana, hebu tusijifanye wavuvi wazuri wakati hata kushika nyavu hatujui.

Si kisa tu umemsikia fulani anaongea na ukaamini, ukumbuke hao wasemao si malaika useme wanaongea kila kilicho sahihi na wakijitetea kweli wanamaanisha. Au fulani kataja majina usikurupuke haraka tu na kusema kaongopa, kwani ulikuwemo mawazoni mwake?
Eti Fulani kakana hivyo ni ukweli,ukumbuke pia hakuna Mwizi anayekubali nimeiba atakana na hata akibanwa sana huweza sema niliazima bila ya ruhusa na sikuiba. Pia Aliyetuhumu fulani kaiba anamaanisha kuwa ni kweli, huenda ushahidi huko mbele ukamzidia nguvu akasema nilimwona tu akipita eneo ambalo lilikumbwa na wizi.

Jamani wadau wote tunajua ni jinsi kuna baadhi ya wenzetu walipotea kisa madawa ya kulevya, mmojawapo ni mwenzangu niliyesoma naye shule moja ya msingi na wengine waliingizwa bila ya kujua kwa kutiliwa madawa kwenye sigara, kinywaji na vitu vingine ili wawe wateja wazuri wauzaji wawaingie pesa. Asilimia kubwa tunayachukia, tunahitaji nchi iondokane na kadhia hii. Hebu sasa tutulieni si kutia chumvi au sukari pishi ambalo wala hatujui lilianzwa vipi kutayarishwa hadi kufikia hapo. Ukiwa unapinga madawa ya kulevya basi simamia msimamo wako tu, chukua nafasi kwenye ngazi ya familia kulipiga vita. Laiti kama kila mmoja akilipiga vita sehemu ya uwezo wake, tutafika mbali sana kuliko kuendelea kuropoka tu.

Kama Makonda kweli amekosea basi ashtakiwe, apandishwe kizimbani. Sisi hatujawa sehemu ya mahakama tuanze kuhukumu watu mapema namna hiyo. Kama Mtu katuhumiwa pia msichukue nafasi ya kuhukumu, waachieni wenye kazi yao. Nyinyi bakini na zenu, maswala ya kichama hebu tuyaweke kando kwanza kwenye masuala tusiyoyajua.
NI HAYO TU.

Hassan O Mambosasa,
www.maridhawa.com

Morogoro,
Tanzania.
 
Vita ya madawa ya kulevya ni kubwa kuliko tunavyofikiria.

Ukisikia mumeo, mkeo, hawara'ko, kaka'ko, dada'ko, mama'ko, baba'ko, babuyo, bibiyo, boss wako, rafiki yako, jirani yako, jamaa yako, mchungaji wako, sheikh wako au wewe mwenyewe unaitwa kuhojiwa usistuke.

Ni vita kubwa sana ambayo inagusa kila mmoja wetu kwa namna moja nyingine.

Tupambane kutokomeza unga, ni safari ndefu na ngumu.

Nchi imeanza kutikisika na ndiyo mwanzo.

Wapenda mema tushirikiane kwenye hili la sivyo sisi sote tutaingia kwenye janga tukitaka tusitake.

Tukiyawachia haya, utafika wakati tutawekewa madawa ya kulevya mpaka kwenye pipi, biskuti ili mradi tuwe wateja na watu waendeleze ushetani wao.

Tuungane bila kujali nani ni nani.
Unayosema ni ukweli mtupu. Ninasikitika jinsi watanzania wengi tunapolichukulia kishabiki. Lakini ni muhimu sana kutumia mbinu sahihi kwa vita hii ili ushindi upatikane. Kila vita ina mbinu zake ili kuhakikisha unapata ushindi.

Watanzania ushabiki wa vyama vya siasa, vilabu vya mpira, ukanda , ukabia au udini hautatusaidia kwa namna yoyote kutatua matatizo yetu.
 
M makonda siku zote namfahamu kama kada msanii, lakini kwa usanii Wa awamu hiii! Kaniacha na maswali.

Hivi jamani tuweni wakweli, makonda anaweza je kusema anaoushahidi na uchunguzi umefanyika huku majina aliyonayo hayajakamilika, unataja mtu jina moja kweli! Na mengine yametajwa ma A.K.A!

Narudia tena, makonda ni msanii lakini nauona mwisho wake uko karibu kuliko pua na mdomo.

Huwezi kudanganya watu zaidi y million 48 ukabaki salama
 
Halafu ameandika tukaratasi.eti Nyandu Tozzy mara Philemone Mbowe,ajabu kina watu na akili zao wanaunga mkono
 
M makonda siku zote namfahamu kama kada msanii, lakini kwa usanii Wa awamu hiii! Kaniacha na maswali.

Hivi jamani tuweni wakweli, makonda anaweza je kusema anaoushahidi na uchunguzi umefanyika huku majina aliyonayo hayajakamilika, unataja mtu jina moja kweli! Na mengine yametajwa ma A.K.A!

Narudia tena, makonda ni msanii lakini nauona mwisho wake uko karibu kuliko pua na mdomo.

Huwezi kudanganya watu zaidi y million 48 ukabaki salama
Jina maalufu ndio raisi kumpata mtu.Mfano vijiweni unakaa na mtu muda mrefu jina lake halisi hulifaham unalijua la kijiweni tu na wauza ngada wengi wanaficha majina yao halisi
 
Jina maalufu ndio raisi kumpata mtu.Mfano vijiweni unakaa na mtu muda mrefu jina lake halisi hulifaham unalijua la kijiweni tu na wauza ngada wengi wanaficha majina yao halisi
"maalufu" ?
 
Eti "Watuhumiwa tunawajua kuliko wanavyojijua", kumbe hata majina yao halisi hawayajui.....mtu kwenye list anaitwa mmiliki wa Sea cliff.....what if hiyo Sea Cliff ikiwa inamilikiwa na share holder zaidi ya mmoja?? Makonda akishtakiwa mahakamani atajibu alikuwa anamlenga mmiliki yupi? Dogo ni mkurupukaji kuzidi hata bao la kwanza
 
M makonda siku zote namfahamu kama kada msanii, lakini kwa usanii Wa awamu hiii! Kaniacha na maswali.

Hivi jamani tuweni wakweli, makonda anaweza je kusema anaoushahidi na uchunguzi umefanyika huku majina aliyonayo hayajakamilika, unataja mtu jina moja kweli! Na mengine yametajwa ma A.K.A!

Narudia tena, makonda ni msanii lakini nauona mwisho wake uko karibu kuliko pua na mdomo.

Huwezi kudanganya watu zaidi y million 48 ukabaki salama
Jamani mbona Logic ni ndogo sana mweee! Hiyo ni Biashara ya kulevya labda nikuulize kwanini wewe unajiita H.T.P ?!?!?! hebu jibu hilo kwanza. The same na madawa ya kulevya si mnajua kuwa ni biashara haramu jamani au ilihalalishwa lini. Mtu anaweza kuwa maarufu kwa a.k.a kuliko hata hilo jina lake! Ndio uchunguzi sasa utaanzia hapo. Sasa kwa mfano wewe umenikosea sin nitataja H.T.P kanikasea si ndi uchunguzi unaanzia hapa. je kwa kutamka H.T.P nimekosea si ndio uluvyojiregistyer. jamani tufanye mambo ya msingi ninge furahi saaaana kama ningeona sukuhu inatolewa kwa kuonyesha uchungu wa madawa ya kulevya kuliko uchungu mnaouna wa Makonda kushughuklikia madawa ya kulevya! Shame on Us ( Tanzanians) . Ingekuwa kungine huyo ni Shujaaa, poor us sasa hivi eti ni kinyume chakle Mungu wangu!
 
Halafu utashangaa mtu kalike huu utumbo wako.

Kama RC kapewa taarifa akapewa jina la A.K.A kwanini asitake time na timu yake wawachunguze hao watu ili wawajue japo majina yao kamili afu ndo wawatafute? Kiherehere cha nini.. Kweli Shame on us Tanzanians who keep on electing incapable leaders....

No wonder kwamaalezo ya Kamanda Sirro waliofika ni wanne tu.

Vita ya Madawa ya kulevya sio kama ya, wezi wa kuku.. Ni vita kama ya Ugaidi.. You need to be very smart. Ndio maana ukifuatilia operation GERANIMO EKIA ( kumuua Osama) utajifunza mengi lakini pia namna CIA inavyodeal na drug trafficing...
 
go go Makonda wananchi tupo nyuma yako
Labda wewe MWANANCHI wa nchi ya kukurupuka ndo upo nyuma yake! Wenye nchi yao ndo tunaomdai ushahidi na jinsi anavyoliharibu pambano hili kwa mbinu zake za kimakusudi. Boss wa mkoa kwa karatasi ile isiyo na utambulisho utadhani ni ya mwanafunzi wa kidato cha pili aliyefeli.
A.k.a badala ya majina halisi yenye kutaja umri, kabila na mahali anapoishi na anapopatikana, wajihi wake na hata biashara yake. Namsikitia sana kwa kukubali kuicheza kete hii kwani Haikumpasa.
 
Ndugu mkuu Wa mkoa Wa mkoa Wa dar es salaam naiukubali kwa kazi yako ya kupinga na kupiga vita madawa ya kulevya jambo ambalo limewafanya watanzania wengi wenye nia ya pamoja katika kupiga vita madawa ya kulevya ambayo yapunguza nguvu kazi ya taifa la jamhuri ya muungano Wa Tanzania jambo ulilofanya linaonekana ni la kijasiri na laweza kupunguza mateja mitaani ila kichwa cha maelezo haya ninayoandika nilikuwa nazilungumzia busara na uthibitisho ...ndungu mkuu Wa mkoa wewe tunafahamu fika wewe ni mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Wa dar es salaam ila jambo kama ulilolifanya kwa uwezo wangu Wa kuwa RAIA Wa nchi hii pamoja na katiba ya nchi hii sijaafiki ulichokifanya kumwita kiongozi mbele ya hadhara eti kisa umemhisi ni mtuhumiwa anaehusika na drug abuse sasa ninachojua Mimi kama mwananchi Wa kawaida ni kwamba siku zote unapomhisi mtu unatakiwa kulitumia jeshi la polisi kupeleka orodha ya uliyowahisi ni washukiwa then polis ndiyo wenye dhamana ya kuwaandikia samansi na mwisho Wa siku watuhumiwa wanafika kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano sasa mtukufu mkuu Wa mkoa ulichokifanya ni sheria namba ngapi na ya mwaka gani kama imefanyiwa marekebisho ni mwaka gani kaka ???? Ninao Uhuru Wa kutoa maoni yangu kukosoa kitu au kupongeza serikali bila kubugudhiwa na mtu yeyote ...

Si vyema kuwataja watu hadharani kwamba ni washukiwa na madawa yakulevya bila ushahidi au kidhibitisho tambua kwamba cheo ulichonacho ni dhamana tu ndugu mkuu Wa mkoa ..jambo hili limenifurahisha sana kwa upande mmoja na kwa upande mwingine umekera na kunifanya niamini yale maneno wanayozungumza Wa mtaani kwamba Tanzania viongozi hwafuati sheria katika uongozi wao ...na ule usemi usemao "dictatorship`` sitaki kuamini hilo ila kwa mtindo huu itanifanya niamini kwamba hii misemo ....

Mheshimiwa naunga mkono kazi yako na ujasiri bila kusahau ushujaa wako usio na busara katika kapambana na madawa ya kulevya Tanzania

###tanzania without drug abuse is possible

Naomba kuwasilisha
 
Chama ni watu, bila watu hakuna chama. Iwe ni Cuf, Chadema au CCM au chama chochote kile, ikumbukwe watu ndio wanaounda chama. Na unaposikia chama ni kichafu maana yake watu wake wanaokiunda ni wachafu. Hivyo basi hata katika suala hili la madawa ya kulevya, Kama wanaCCM watabainika ndio wahusika wakubwa, basi ni dhahiri kuwa chama kimechafuka na kimeumbuka. Hii ni fact na si siasa.

chama hakiwezi kuchafuka ila mtu na caree yake ndio anachafuka bwana. mbona mambo yanaeleweka???
 
Back
Top Bottom