Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Kuna baadhi vyama mpaka leo havieleweki vinasimamia maslahi ya nani, kuna wawakilishi wao walikuwa wanapiga sana kelele juu ya madawa ya kulevya leo mtu anasimamia wao wanakuja juu kutetea hao wahusika kila siku mapovu yanawatoka juu ya mapapa wa madawa hamjui kuwa viongozi wenu pia ni wahusika wakuu wa madawa nani asiye urafiki wa Lowassa na Rostam, rostam na familia yake ni mmoja wa wahusika wakuu.
Je nani hajui kuhusu GWAJIMA ambaye ndiye alkua mlez wa CHADEMA nani hajui juu ya haya.

Naona humu tunashabikia tunapiga kelele juu ya kitu ambacho hatukijui, msifuate upepo nyie bendera.
Nani na Nani wametajwa leo?
 
Jana usiku nikitokea lindi. Nilikuwa Na drive nikafika mbagala mida ya saa nne hivi Usiku, nilikuwa nimechoka nikaona kabla ya kusonga mbele nipumzike kidogo nipatie japo supu ya kongoro maana nikisema niendelee mpaka Mbezi nitakuta kila sehemu imeshafungwa na nitalala njaa,

Wakati nasubiri Supu ikawa ni saa tano hivi, jamaa walinichelewesha. Nikaagiza Coca ya pili, kabla sijaanza hata kunywa nikaona watu wanaanza kukimbia, kucheki naona Askari Kama nane hivi na Machine gun na mabomu, Mimi sikukimbia niliona kuna Kama watu 8 hivi nao walikuwa wamekomaa,

Pembeni yangu walikaa wazee fulani hivi wa makamo Kati ya 60-70 miaka kwa kuwatizama. Mara nikamuona Askari mmoja Kati ya wale nane, ni dogo tu. Kati ya 19-24 miaka hivi, akawafata wale wazee, nikasikia kaeni chini kaeni chini, mzee mmojawapo akataka kuhoji. Mara Afande akampa Rungu la begani mzee chini. Duh iliniuma sana, Mimi kuona hivyo nikanyanyuka nikaambaa zangu mpaka ktk gari nikaondoka zangu,

Kichwani najiuliza maswali Mia pamoja na hasira, infact hata njaa ilinipotea. Hivi Haya ndiyo maisha yetu Siku hizi, hatuheshimu tena hata wazee wetu wengine ni babu zetu.

Swali langu kwa Mh Makonda, hivi tangu umeweka hii amri ya kufungua bara saa kumi na kufunga saa tano usiku, ni faida gani umeshapata mpaka sasa hivi?. Hizi halmashauri zimeongeza kipato kwa kiwango gani?

Tahadhari, Mh. Makonda, ungekuwa unajua jinsi watu wanavyonyanyaswa na kudhalilishwa na polisi huku mitaani tangu uweke hiyo amri Nina Imani ungesitisha kwanza na ufanye tathmini ili uipange upya, Huku mitaani chuki ni kubwa sana kwako wakati wewe binafsi hunufaiki na chochote juu ya hii Amri,

Askari polisi wadogo wanapiga na kudhalilishaa watu wazima, na ole wake mtu akose elfu 50 au 30 ya kumpa polisi ili aachiwe, basi atapigwa Kama mwizi, Mh Makonda, Japokuwa siyo ww unayewapiga hawa raia wema wasio na hatia, tena walipa kodi wazuri, lakini Kaa Ukijua, Mitaani watu wana Chuki kubwa mno mno na wewe. Tafakari haraka na uchukue hatua, hii siyo Dafur, hii ni Tanzania yenye amani tele, tena ipo kabla hata Hujazaliwa na Mimi pia. Tutakufawa wote lakini Tanzania bado itabaki, Tumia busara na Hekima kuwaongoza Watu, ili Upate kibali machoni pa Mungu, kudhalilisha wazee ni Laana, hakika Hutabaki Salama!
 
Kupitia Clouds TV Makonda anamtaja Mbowe kuwa anahusika na madawa ya kulevya. Jee haya ni mapambano ya madawa ya kulevya au kuna hidden agenda?

Watanzania sijui lini mtakuja kujitambua, wasipotajwa shida, wakitajwa shida!! Mbona husemi kwa nini Gwajima Na Idd Azan wametajwa!? Wapumbafu tuko wengi nchi hii, na dawa yetu ni mkono wa chuma ili tunyoke!!!!
 
Mboweeeeeeeeeeee! Gooooooooooooo!

Yaani mpaka kichekesho, mlidhani akitajwa mboww ndio wapinzani watashtuka? Kama anafanya hiyo biashara kamata weka ndani na afungwe miaka ya kutosha kwani atakiacha chama na watu wasafi. Hakuna mtu yuko tayari kumtetea mtu anayefanya biashara ya kuumiza nguvu kazi ya taifa. Kwa hilo asibaki yoyote wala hofu kwa yoyote.
 
nchi hii ilishaoza kwenye uongozi ..... tusubiri miujiza ya mungu
 
Back
Top Bottom