Jana usiku nikitokea lindi. Nilikuwa Na drive nikafika mbagala mida ya saa nne hivi Usiku, nilikuwa nimechoka nikaona kabla ya kusonga mbele nipumzike kidogo nipatie japo supu ya kongoro maana nikisema niendelee mpaka Mbezi nitakuta kila sehemu imeshafungwa na nitalala njaa,
Wakati nasubiri Supu ikawa ni saa tano hivi, jamaa walinichelewesha. Nikaagiza Coca ya pili, kabla sijaanza hata kunywa nikaona watu wanaanza kukimbia, kucheki naona Askari Kama nane hivi na Machine gun na mabomu, Mimi sikukimbia niliona kuna Kama watu 8 hivi nao walikuwa wamekomaa,
Pembeni yangu walikaa wazee fulani hivi wa makamo Kati ya 60-70 miaka kwa kuwatizama. Mara nikamuona Askari mmoja Kati ya wale nane, ni dogo tu. Kati ya 19-24 miaka hivi, akawafata wale wazee, nikasikia kaeni chini kaeni chini, mzee mmojawapo akataka kuhoji. Mara Afande akampa Rungu la begani mzee chini. Duh iliniuma sana, Mimi kuona hivyo nikanyanyuka nikaambaa zangu mpaka ktk gari nikaondoka zangu,
Kichwani najiuliza maswali Mia pamoja na hasira, infact hata njaa ilinipotea. Hivi Haya ndiyo maisha yetu Siku hizi, hatuheshimu tena hata wazee wetu wengine ni babu zetu.
Swali langu kwa Mh Makonda, hivi tangu umeweka hii amri ya kufungua bara saa kumi na kufunga saa tano usiku, ni faida gani umeshapata mpaka sasa hivi?. Hizi halmashauri zimeongeza kipato kwa kiwango gani?
Tahadhari, Mh. Makonda, ungekuwa unajua jinsi watu wanavyonyanyaswa na kudhalilishwa na polisi huku mitaani tangu uweke hiyo amri Nina Imani ungesitisha kwanza na ufanye tathmini ili uipange upya, Huku mitaani chuki ni kubwa sana kwako wakati wewe binafsi hunufaiki na chochote juu ya hii Amri,
Askari polisi wadogo wanapiga na kudhalilishaa watu wazima, na ole wake mtu akose elfu 50 au 30 ya kumpa polisi ili aachiwe, basi atapigwa Kama mwizi, Mh Makonda, Japokuwa siyo ww unayewapiga hawa raia wema wasio na hatia, tena walipa kodi wazuri, lakini Kaa Ukijua, Mitaani watu wana Chuki kubwa mno mno na wewe. Tafakari haraka na uchukue hatua, hii siyo Dafur, hii ni Tanzania yenye amani tele, tena ipo kabla hata Hujazaliwa na Mimi pia. Tutakufawa wote lakini Tanzania bado itabaki, Tumia busara na Hekima kuwaongoza Watu, ili Upate kibali machoni pa Mungu, kudhalilisha wazee ni Laana, hakika Hutabaki Salama!