Kwetu sisi wenye umri mkubwa kidogo hoja ya wabunge kuita watu bungeni ati kwa kisingizio cha kudhalilishwa hakikuanza leo. Mwanzoni wa miaka ya 2000 kuna Mhariri aliwahi kuitwa kwa sababu gazeti lake lilichapisha 'habari za kudhalilisha wabunge'.
Kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja wabunge hususani wa upinzani wamekuwa wakipigania kile kinachoitwa 'udikteta' wa raisi, kwamba hataki kukosolewa. wamesema kila aina ya lugha chafu hadi kufikia 'kupanga njama za mauaji' kwa kisingizio cha unabii lakini haya yote yanaonekana ni demokrasia.
Zitto Kabwe akijenga hoja amesema 'kila muhimili una wivu' sasa kama ni hivyo kwanini hakuna heshima kwa Raisi (mhimili wa dola)? Kila kukicha mmewatukana wakuu wa mikoa,wilaya kuwa ni vibaraka je huu si udhalilishaji?
Kama Makonda eti kwa tuhuma za kusema 'wabunge wanachekesha, wanasinzia' amedhalilisha bunge na wabunge kiasi cha kutoa hoja afutwe kazi basi hatuna uhalali wa kumtetea Lema na Mkewe kwa kumdhalilisha Raisi Dr.Magufuli na RC Gambo tena kwa ushahidi.
wakiwajibika Makonda na Mnyeti basi Lema,Lissu,Mke wa Lema na wengineo hawatapona kwani hukumu hiyo ya wabunge inatengeneza 'rejeo' la mhimili mmoja kutoingilia mhimili mwingine kuwa ni kosa.
Leo wanaojiita wanademokrasia' wanatumia kanuni za bunge kuwaminya wakosoaji wa wabunge, Leo mbunge anaongopa eti kapigiwa simu huku anayemshitaki hayupo bungeni? ni wapi sasa tuna uhalali wa kudai 'natural justice'
Hoja hii ya wabunge sasa inahalalisha ni haki na sahihi kabisa kwa Dola kuwachukulia hatua wabunge wote wanaokosoa na kumdhihaki Raisi nje ya bunge.