Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Escrow ni account,sasa itakujaje? Shame!

Lugumi ni kampuni,itakujaje?

Walioweka hela nje kwani sheria inakataza?Fanya utafiti kabla ya kuja na wivu wa kike
 
Nauliza mbona alipotaja vidaaagaa nyie wenyewe mliongea anaogopa mapapa??
Ebu mwacheni makonda afanye kazi zake bwanaa.
Sasa kila mumoja anamshambulia. hivi tanzania tumelaaniwa kiasi hiki kweli??
Badala ya kuunga juhudi za kijana huyu aliyejitoa muhanga halafu ni kumsengenya jamaaanii??
Makonda Mungu anakuona na atakulipa kwa juhudi zako.
Soma wagalatia 9:6
 
Hahaha, hana wa kumlinda huko, hana maslahi....huku kwenye sembe kuna wadau wake. Kama alishawahi kwenda hata Nairobi kabla ya kuwa RC, sitashangaa kwenda mapumziko Dubai au Paris
Pole sana kama haya ndio unayoyaona muhimu kuliko watoto wa kitanzania wanaoumia na madawa ya kulevya.
 
Mkuu wa mkoa unaendelea kulisaidia taifa kuondokana na biashara ya madawa ya kulevya.

Na umeonyesha ujasiri na ukomavu pale ulipotaja majina yao kwenye vyombo vya habari, na kuwataka uliwataja kufika polisi.

Inamaanisha unaweza kujenga taifa likaondokana na biashara ya madawa ya kulevya ambazo kila mtu anajua madhara yake.

Lengo letu ni taifa lisonge mbele siyo tu kwa kumaliza hii vita ya madawa ya kulevya.

Kwa kuwa umekuwa jasiri wa kutaja majina na tunakupa hongera.

*SIYO MADAWA YA KULEVYA PEKEE YAKE YANORUDISHA NYUMA MAENDELEO YA TAIFA HATA WALIOTUIBIA FEDHA ZA TAIFA LETU WAMETURUDISHA NYUMA*

NAOMBA:-
TUNAKUOMBA UWATAJE MAJINA NA WAJE KITUONI WARUDISHE FEDHA.

1.LUGUMI
2.ESCROW
3.WALIOFICHA FEDHA NJE YA NCHI MAJINA YAPO.

TUNAKUOMBA KUPITIA TV NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI WAITE KITUONI KWA KAMANDA SIRO.
Amalizie kwanza kuwata wauza unga aanze na lizone
 
Serikali lazima isemwe.......

Mahakama lazima isemwe .....

Rais kachaguliwa na wananchi na wabunge wamechaguliwa na wananchi hivyo bunge kumsema Rais( Serikali) ni wajibu wake.......

Msituletee porojo za kichama kimoja na Mawazo mgando ya kupiga mapambio kwa kila kitu......

Kama rais na serikali Yake hawataki kusemwa dawa ni kujiuzulu tu......
 
Mtu unaitwa kwa ajili ya mahojiano juu ya Dawa za kulevya .Kabla hujaenda kuitikia wito kujua kama unatuhumiwa kuuza ,kutumia au kuna taarifa za mtu au watu zinahitajika kutoka kwako unakimbilia kuanza kutoa matamko ya kukanusha kujihusisha na biashara ya Dawa za kulevya.

Hii ni Dalili Tosha kwamba mmeguswa .
Wengine wanasema ooo sijui wao wasukuma ,sijui wanamuunga mkono Rais so what ?

Nendeni mkasikilize mlichoitiwa mtakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusema kulipuka kwenu kunaongeza mashaka .
Mara oohh naonewa wivu sijui mbona nani hajatajwa huku ni kuweweseka tulieni mshughulikiwe.

Wengine wameitwa wao wanataka kulifanya hili jambo ni la Taasisi zao au madhehebu yao .Na baadhi ya wanachama au waumini wanataka kulibeba jambo hili wakiwa blind /Less informed.

Vyombo vya Dola vinawajua hawa viongozi wenu kuliko nyie mnavyowajua.

Makonda haya Mayowe usiyasikilize endelea kukomaa nao .
Usigeuke nyuma utageuka kuwa jiwe .

Ukitupa Jiwe gizani ukasikia mayowe ujue jiwe limelenga kwenyewe.

Ninajua Makonda hajakurupuka anazo taarifa za uhakika juu ya hawa anaowaita .
 
Kwetu sisi wenye umri mkubwa kidogo hoja ya wabunge kuita watu bungeni ati kwa kisingizio cha kudhalilishwa hakikuanza leo. Mwanzoni wa miaka ya 2000 kuna Mhariri aliwahi kuitwa kwa sababu gazeti lake lilichapisha 'habari za kudhalilisha wabunge'.

Kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja wabunge hususani wa upinzani wamekuwa wakipigania kile kinachoitwa 'udikteta' wa raisi, kwamba hataki kukosolewa. wamesema kila aina ya lugha chafu hadi kufikia 'kupanga njama za mauaji' kwa kisingizio cha unabii lakini haya yote yanaonekana ni demokrasia.

Zitto Kabwe akijenga hoja amesema 'kila muhimili una wivu' sasa kama ni hivyo kwanini hakuna heshima kwa Raisi (mhimili wa dola)? Kila kukicha mmewatukana wakuu wa mikoa,wilaya kuwa ni vibaraka je huu si udhalilishaji?

Kama Makonda eti kwa tuhuma za kusema 'wabunge wanachekesha, wanasinzia' amedhalilisha bunge na wabunge kiasi cha kutoa hoja afutwe kazi basi hatuna uhalali wa kumtetea Lema na Mkewe kwa kumdhalilisha Raisi Dr.Magufuli na RC Gambo tena kwa ushahidi.

wakiwajibika Makonda na Mnyeti basi Lema,Lissu,Mke wa Lema na wengineo hawatapona kwani hukumu hiyo ya wabunge inatengeneza 'rejeo' la mhimili mmoja kutoingilia mhimili mwingine kuwa ni kosa.

Leo wanaojiita wanademokrasia' wanatumia kanuni za bunge kuwaminya wakosoaji wa wabunge, Leo mbunge anaongopa eti kapigiwa simu huku anayemshitaki hayupo bungeni? ni wapi sasa tuna uhalali wa kudai 'natural justice'

Hoja hii ya wabunge sasa inahalalisha ni haki na sahihi kabisa kwa Dola kuwachukulia hatua wabunge wote wanaokosoa na kumdhihaki Raisi nje ya bunge.
Kweli kabisa maana kwa maana hiyo humanisha kuwa wao hawakosei na hawapaswi kusemwa maana wao wanaita n udhalilishaji
 
ulikuwa na hoja kama yangu.Umenena kweli tupu.
Naona wabunge wanalalamikia kuhusu heshima yao wengi wao wa upande upinzani lakini wanasahau kwa namna wanavyo ongea bila hata breki juu ya rais ambaye naye anastahili heshima sawa na wao wanavyostahili.
Ukitaka kuheshimiwa jiheshimu na waheshimu wengine na si kutaka heshima upande wako tu bila kujali heshima ya wengine.
 
Dawa zipi ulizowakuta nazo?
Au ni ule msokoto wa bange alobambikiwa mwana wa sepetu.
 
Mkuu wa mkoa unaendelea kulisaidia taifa kuondokana na biashara ya madawa ya kulevya.

Na umeonyesha ujasiri na ukomavu pale ulipotaja majina yao kwenye vyombo vya habari, na kuwataka uliwataja kufika polisi.

Inamaanisha unaweza kujenga taifa likaondokana na biashara ya madawa ya kulevya ambazo kila mtu anajua madhara yake.

Lengo letu ni taifa lisonge mbele siyo tu kwa kumaliza hii vita ya madawa ya kulevya.

Kwa kuwa umekuwa jasiri wa kutaja majina na tunakupa hongera.

*SIYO MADAWA YA KULEVYA PEKEE YAKE YANORUDISHA NYUMA MAENDELEO YA TAIFA HATA WALIOTUIBIA FEDHA ZA TAIFA LETU WAMETURUDISHA NYUMA*

NAOMBA:-
TUNAKUOMBA UWATAJE MAJINA NA WAJE KITUONI WARUDISHE FEDHA.

1.LUGUMI
2.ESCROW
3.WALIOFICHA FEDHA NJE YA NCHI MAJINA YAPO.

TUNAKUOMBA KUPITIA TV NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI WAITE KITUONI KWA KAMANDA SIRO.

Mtu mzima akishikwa pabaya panapouma kilio chetu muda mwingine unaweza ukacheka japo mwenzio analia kwa uchungu. Duu, haya bwana. Poleni
 
Serikali lazima isemwe.......

Mahakama lazima isemwe .....

Rais kachaguliwa na wananchi na wabunge wamechaguliwa na wananchi hivyo bunge kumsema Rais( Serikali) ni wajibu wake.......

Msituletee porojo za kichama kimoja na Mawazo mgando ya kupiga mapambio kwa kila kitu......

Kama rais na serikali Yake hawataki kusemwa dawa ni kujiuzulu tu......
Mkuu kw hiyo wabunge wasisemwe? wasikosolewe? wauze mihadarati? wafanye watakalo? kama ambavyo tunamkosoa raisi lazima kila mtu akosolewe, sasa kwa hili la wabunge kuwanyamazisha wanaowakosoa inahalalisha dola kunyamazisha wanaikosoa. Haya, Kwa msingi huu Lema na Mkewe hawatapona kwa kuukosoa mhimili wa dola kama Makonda atakuwa na hatia kwa kuwakosoa wabunge.
 
Awaite kwani yeye anamamlaka gani?
Ni nani katika nchi hii, vita hii ya ufisadi inawatu wake ambao wanalindana tu

Yeyote yule anayeonyesha Ukakamavu, Uzalendo, Ujasiri wa kupangusa makamasi kwenye uso wa nchi hii, (Kwa Vitendo), tutahakikisha anakuwa Kiongozi na kumpa mamlaka zaidi. Tanzania lazima isafishwe. Wanaompinga Kiongozi huyu na harakati zake, iwe kisheria au kimaadili au hata maneno ya fedheha kwenye mitandaoni basi hawalitakii jema Taifa letu. At least, for once, lets do something good for our country. Tutafute umaharufu wa nchi yetu, sio umaharufu wa watu binafsi au klabu za mpira. Tanzania comes first. Tanzania oyee.
 
Tundu lissu amesema rais ni wa hovyo na ni mropokaji..lakini wao wangeitwa hivyo wangesema wanadhalilishwa..kweli wacha magufuli awanyooshe vya kutosha
 
Mkuu kw hiyo wabunge wasisemwe? wasikosolewe? wauze mihadarati? wafanye watakalo? kama ambavyo tunamkosoa raisi lazima kila mtu akosolewe, sasa kwa hili la wabunge kuwanyamazisha wanaowakosoa inahalalisha dola kunyamazisha wanaikosoa. Haya, Kwa msingi huu Lema na Mkewe hawatapona kwa kuukosoa mhimili wa dola kama Makonda atakuwa na hatia kwa kuwakosoa wabunge.
Mbona tuliwasema juzi hapo baada ya kuhongwa mil 10? Kwani walifanyaje?....
 
Back
Top Bottom