ITR
JF-Expert Member
- Sep 22, 2022
- 7,637
- 20,676
Vita iliyo anzishwa na Netanyau kwa lengo la kumuangusha Ayatollah imekuwa kinyume chake na inaenda kumnufaisha kisiasa.
Nadhani ulimwengu wa kimagharibi utakuwa umeshangazwa,kufadhaishwa na kutamaushwa sana na raia wa Iran kwa kuungana na serikali yao hali yakuwa wamekuwa wakiamimisha watu duniani kupitia vyombo vyao vya habari kuwa raia wa Iran wameichoka serikali yao ya kidini kwa sababu inawakandamiza.
Lakini raia wa Iran wameonesha dunia kuwa mikwaruzano ya kisiasa ndani ya nchi yao haina mahusiano na msilahi ya kitaifa.
Na mikwaruzano ya kisiasa huwa ipo kila nchi duniani zikiwemo hiyo Israel na Marekani ambao walitaka kutumia mikwaruzano ya kisiasa ya ndani ya Iran kuiangusha serikali yake.
Hata Netanyau ndani ya nchi yake hatakiwi na raia wengu na huwa wana andamana kumpinga.
Kiukweli tukiachana na ushabiki Israel na Marekani walifanya kitu cha kipumbavu sana kuishambulia Iran wakati wakifanya mazungumzo, kitendo hicho kitawanyongonyeza wanasiasa wenye msimamo wa wastani ndani ya Iran walio kuwa wanapendelea mazungumzo na Marekani.
Malengo ya hii vita yalikuwa ni kwenda kuharibu vinu vya nukilia, kubadilisha utawala na kwenda kuirazimisha Iran kusaini makubaliano ya amani na Israel kama walivyo fanya kwa Misri na Jordan lakini yote yamegonga mwamba.
Kiufupi Netanyau raia wa Iran wamemdhalilisha sana Netanyau, nadhani sasa hivi akiona video zake za kuwaambia wairan kuwa amekuja kuwakomboa atakuwa ana tamani ardhi immeze.
Lakini pamoja na hayo yote Iran na penyewe kuna mapungufu makubwa na uzembe mwingi.
Taasisi zake za kijasusi zimejaa uzembe na utovu wa uwajibikaji ,kitendo cha hujuma dhidi ya mifumo ya ulinzi, mauaji ya viongozi na wanasayansi imeridhihirisha hilo.
Inatakiwa kufumua taasisi zake za kijasusi na kuzifanya kuwa na weledi unao takiwa tofauti na hapo maadui zake ipo siku watafanikisha wanacho kitaka kwa sababu kwa sasa wameenda kujipanga upya na watarudi na mbinu mpya.
Iran inatakiwa kuimarisha jeshi lake la anga,unajuwa unapo kuwa na jeshi zuri la anga hata ikitokea mifumo ya ulinzi imepofushwa , jeshi la anga lina uwezo mkubwa wa kililinda anga hasa dhidi ya adui anaye tegemea kukushambulia kwa kutumia ndege kama Israel.
Iran ingekuwa na jeshi la anga levo ya Pakistan tu hata hilo anga la Iraq lingekuwa chungu sana kwa ndege za Israel.
Cha mwisho Iran ifanye kila namna imiliki silaha za nyuklia ili ijihakikishie usalama wa milele tofauti na hapo hatokuwa salama ,sasa hivi wamemshindwa ila wataenda kujipanga upya hata kama ni miaka 20 na kurudi kujaribu kufanya kilicho washinda sasa hivi.