Vita kati ya majangili na askari wa hifadhi za wanyama pori

Aisee, noma. Sema hii ya wachinjaji nyama machinjioni nilishaisikia kuna mtu alinambia kaa mbali kabisa na hao jamaa, kuchezea damu, visu na mapanga kwao washazoea sasa wewe peleka mwili wako
 
Dunia hii kuna watu wanafikirisha sana aisee
 
Adui hana alama, hakuna adui mvivu.
 
Kuna zee (jangili) moja lilitaka kunifyeka panga hadharan baada kujua natembea na binti yake ila niliponea chupu chupu baada ya kuchanganya vyema mbaliga zangu sitoisahau hyo siku. Dah Hawa watu wanaroho ngumu sana asee huwa hawaoni ajabu kumwaga damu ya mtu
 
Bora ukutane na talibani nakuwatukana dini yao hadharani hata kumla mke wake kuliko kukutana na magame reserve
 
Mimi ni mzaliwa wa Mloka ni hatua chache kuingia pori la hifadhi. Sasa nilipomaliza chuo nikachagua sehemu ya kufanyia kazi ni Selous. Kabla ya kuingia mafunzoni tulikuwa tunafanyakazi hizi za magendo. Sasa unapata mtanziko wapi.
 
Mimi ni mzaliwa wa Mloka ni hatua chache kuingia pori la hifadhi. Sasa nilipomaliza chuo nikachagua sehemu ya kufanyia kazi ni Selous. Kabla ya kuingia mafunzoni tulikuwa tunafanyakazi hizi za magendo. Sasa unapata mtanziko wapi.
Mkuu Rufiji sasa umeliweka sawa..Kijiji cha Mloka nakifahamu na nilisha fika hapo, kimepakana na selous kwa kambi ya Mtemere, hata askari na wafanyakazi wa hotel huenda kunywa na wengine kupata mademu hapo, nakumbuka kulikuwa na mgogoro kati ya Selous na kijiji hicho baada ya mmoja wa wanakijiji kufungwa kwa kosa la kuiba mafuta katika kambi ya Mtemere.

Kuna askari alikuwa anaitwa Twaha...aliwahi sababisha nyumba moja hapo Mloka kuchomwa moto na wanakijiji kwa mgogoro huu, yeye alikwenda hapo kunywa kisha akaenda kulala kwa demu wake, wanakijiji wakachoma nyumba ya huyo demu wake ili Twaha afie ndani, uzuri alipata taarifa mapema na kutoroka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…