Vita kati ya majangili na askari wa hifadhi za wanyama pori

Vita kati ya majangili na askari wa hifadhi za wanyama pori

Bora Ukutane na Majambazi kuliko kukutana na Jangili huyu ameshazoea kuziona damu.

Ni sawa na Bora ukutane na Muuzaji Bucha ya nyama kuliko kukutana na Mtu wa machinjioni ya mifugo hawa nao wana roho ngumu kuna jamaa angu aliwahi kuchomwa kisu mguuni kikatokea chini kwenye sori ya kiatu
Aisee, noma. Sema hii ya wachinjaji nyama machinjioni nilishaisikia kuna mtu alinambia kaa mbali kabisa na hao jamaa, kuchezea damu, visu na mapanga kwao washazoea sasa wewe peleka mwili wako
 
Binafsi, nawapongeza sana Askari wa wanyamapori, ni jasiri mno!
Majangiri ni watu hatari sana! Hakuna tofauti na wale wanaojiita wapigania haki wa msituni wa hit & run.
Wamekomaa mno kuliko ngozi ya mamba.
Imagine, wanaweza kukaa hata miaka 5 msituni bila kuoga?
Dunia hii kuna watu wanafikirisha sana aisee
 
Kuna kitu wengi wanakosea hapa. Hakuna anayesema ujangili ni mzuri au kuwatetea. Tatizo ni pale hao askari wanyamapori wanapofanya unyama wa hali ya juu kwa watu ambao hata hawakustahili. Wengine unakuta ni hawa watu local na duni kabisa ambao wanatumia mapori kujikimu kutokana na ukali wa maisha na hawana silaha za hatari. Halafu wenhi wanakiuka sheria kwa kujichulia sheria mikononi.
Adui hana alama, hakuna adui mvivu.
 
Kuna zee (jangili) moja lilitaka kunifyeka panga hadharan baada kujua natembea na binti yake ila niliponea chupu chupu baada ya kuchanganya vyema mbaliga zangu sitoisahau hyo siku. Dah Hawa watu wanaroho ngumu sana asee huwa hawaoni ajabu kumwaga damu ya mtu
 
Bora ukutane na talibani nakuwatukana dini yao hadharani hata kumla mke wake kuliko kukutana na magame reserve
 
Mkuu Rufiji napata tabu kidogo na hii hadithi yako...unasema umekulia Selous kisha unasema ulikuwa kwenye mafunzo kwa vitendo ni confusion...upi ukweli pili katika pori la selous sehemu inapita reli ni Matabwe ambayo iko Western zone na Kisaki ambayo iko eastern zone, na sehemu ambayo unaweza pata mto wako vua samaki ni mto Rufiji... kwa ukaribu uliosema mlipowaona hao wavuvi itakuwa ni mto Rufiji ambao upo Matambwe katika kituo cha Mtemere na huko hakuna treni.... Uko kwenye mafunzo ya vitendo ni mawindo gani mlikuwa mnatafuta....kwa hadithi yako huenda mlikuwa doria...sasa doria gani mnatafuta mawindo......
Mimi ni mzaliwa wa Mloka ni hatua chache kuingia pori la hifadhi. Sasa nilipomaliza chuo nikachagua sehemu ya kufanyia kazi ni Selous. Kabla ya kuingia mafunzoni tulikuwa tunafanyakazi hizi za magendo. Sasa unapata mtanziko wapi.
 
Mimi ni mzaliwa wa Mloka ni hatua chache kuingia pori la hifadhi. Sasa nilipomaliza chuo nikachagua sehemu ya kufanyia kazi ni Selous. Kabla ya kuingia mafunzoni tulikuwa tunafanyakazi hizi za magendo. Sasa unapata mtanziko wapi.
Mkuu Rufiji sasa umeliweka sawa..Kijiji cha Mloka nakifahamu na nilisha fika hapo, kimepakana na selous kwa kambi ya Mtemere, hata askari na wafanyakazi wa hotel huenda kunywa na wengine kupata mademu hapo, nakumbuka kulikuwa na mgogoro kati ya Selous na kijiji hicho baada ya mmoja wa wanakijiji kufungwa kwa kosa la kuiba mafuta katika kambi ya Mtemere.

Kuna askari alikuwa anaitwa Twaha...aliwahi sababisha nyumba moja hapo Mloka kuchomwa moto na wanakijiji kwa mgogoro huu, yeye alikwenda hapo kunywa kisha akaenda kulala kwa demu wake, wanakijiji wakachoma nyumba ya huyo demu wake ili Twaha afie ndani, uzuri alipata taarifa mapema na kutoroka!
 
Back
Top Bottom