Vita Vya Iran na Marekani: Nani Kasalimu Amri Iran au Marekani?

Vita Vya Iran na Marekani: Nani Kasalimu Amri Iran au Marekani?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
"Naamka napita mitandaoni kwanza kabisa habari muhimu naikuta Aljazira wanatangaza wanasema Marekani na Irani wamekubaliana kumaliza vita. Basi mimi kwanza nikaitizama kile cha habari... Kwani vita hivi alianza nani? Na nani kila siku alikuwa anasema atampigia nani?. Ukweli ni kuwa Marekani na Israeli wameshambulia Irani siku 107 zilizopita, miezi mitatu ilizopita, na Marekani akisikika mara kwa mara akisema kuwa ataimaliza Irani na kuirudisha... kwenye stone age yaani kule kwa zamani kabisa.

"Marekani anajiondoa kwenye vita kwa sababu hajaweza kupata ushindi ambao yeye aliutegemea". Anataja kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano yatafanyika Geneva, mahali ambapo kuna kiti kikubwa kilichovunjika mguu mmoja kuwakilisha mapambano dhidi ya cluster bombs (mabomu ya vishada) yaliyotumiwa na Israel dhidi ya Iran, Gaza, na Lebanon,.

Kuhusu suala la nyuklia, anasema: "Kitu kikubwa ambacho ndicho ambacho Wayahudi wanasema kuwa kinawafanya wao wachopuliwe ni Irani kurutubisha uranium... lakini mshangao katika haya mapatano, Wamarekani wamekubali, wameridhia Wairani kuendelea na enrichment ya uranium lakini sio kwa kiwango cha kutengeneza bomu. Hili ni jambo la kustaajabisha sana na nadhani limewavunja nguvu sana Wayahudi"



View: https://youtu.be/AhnrdT3-bk4?si=Tw9mmyNc3Y_C_L3h
 
As long as vita vimekwisha yote heri, tunaomba visiibuke tena.
 
..Marekani na Iran wameanza kushambuliana tena.

..Iran kashambulia meli ya mizigo kwa drone.

..Marekani kashambulia ndani ya Iran anakodai drones zinahifadhiwa.
 
..Marekani na Iran wameanza kushambuliana tena.

..Iran kashambulia meli ya mizigo kwa drone.

..Marekani kashambulia ndani ya Iran anakodai drones zinahifadhiwa.
JokaKuu,
Marekani na Israel walidhani itakuwa vita vya kuingia na kutoka.

Tunaelekea mwezi wa nne.
Iran imesimama na imejitolea kwa lolote.

Marekani ndiyo inayojitazama.
 
Back
Top Bottom