Me I and my self
JF-Expert Member
- Sep 16, 2016
- 4,077
- 8,828
Mkuu 2000Walipotea wapi; si ajabu unasikia hadithi tu; ni kweli tulipoteza wanajeshi karibu 2000 (sina namba kamili) ambayo ni kama batallion moja, na nimekuambia kuwa katika hatua za kwanza za vita Kuna karibu Batallion nzima iliyopotea kwa sababu ya uamuzi mbovu wa kamanda mmoja.
Vile vile vita ya Lukaya iliua waganda na walibya wengi sana lakini pia watanzania walikufa. Sasa unaposema mimi nina utaahira (lugha za matusi zinazozuiwa hapa JF) sema ukweli wako. Mimi nilikuwa karibu sana na taarifa za mapambano yale kuanzia mwezi Octoba mwaka 1979 kabla hata Rais hajatangaza vita yenyewe kwa vile nilikuwa kwenye Brigedi ya Magharibi ambayo ndiyo iliingia vitani kwanza.
Vita iliendelea kwa miezi saba katika mazingira magumu kama niliyosema hapo, hivyo ni kweli watu walikufa. Huwezi kupigana vita ya ardhini bila askari wako kufa. Jeshi la Uganda halikuasi bali lilielemewa nguvu na jeshi la Tanzania licha ya kuwa walikuwa wanasaidiwa na askari wengi sana kutoka Libya.
Unaposema kuwa watu wetu walielemewa sana ila baada ya hapo jeshi la Uganda likaasi ndipo tukapata unafuu- ni wazi hujui vita nini- ile siyo ngoma ya mdundiko ndugu yangu, ni kazi ya kurushiana risasi za moto, sema pia ni askari wangapi wa Uganda waliokufa kama hutapatwa na ugonjwa wa moyo iwapo unaliangalia jeshi la Tanzania wakati huo katika negative lens;
Jeshi la Uganda lilikuwa kubwa sana, Amini alikuwa anawekeza sana katika jeshi kuliko sehemu nyingine yoyote, ila sasa JWTZ ilikuwa inawafuta kama sisimizi ndipo wakafikia kukata tamaa ya kuendelea na vita ile.
Ni Battalion mbili hizo.
Na makadirio huenda tulipoteza Battalion 3