Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Naona kama wewe unaquestion uwezo wa jeshi la Tanzania wakati huo, na unaelekea kuamini tu kuwa JWTZ walikuwa ni wanyonge. Leo hii sijui muundo wa JWTZ, lakini wakati wa Nyerere JWTZ ilikuwa ni pamoja na JTK, Polisi, Magereza, na Mgambo kama majeshi ya akiba. Kulikuwa na sera ya kuwa jukumu ulinzi wa taifa letu ni raia wote na kila askari katika eneo lolote alikuwa ni mlinzi wa taifa. Hicho kitabu ulichosoma inawezekana kilikuwa kinaripoti namba za wale active soldiers wa TPDF na kusahau kuwa TPDF ilikuwa na reserve soldiesr wengi sana; baada ya vita kuanza wale reserve soldiers wote walikuwa activated na jeshi kuonekana kubwa sana. Katika yote ya Nyerere nadhani sifa yake kubwa ni ile ya kujenga mioyo ya uzalendo kwa wananchi.Sawaa lkn kuna kitabu kimoja kinasema Jeshi letu mpk 1978 kilikuwa na askari wasiozidii 20000 au 30000 lkn ndani ya miezi 6 hivi askari waliongezeka mpk 100000 au 150000....hapa tunajumuisha mgambo, askari polisi, uhamiaji, TISS na wengneo....
Kuhusu iyoo idadi (379) kuna makaburi Bunazi kyaka na Kaboya......
Nataman kujuaa waliokufa wengine walizikwa wapii au walitelekezwa uwanja wa vita, achana na wale waliogeuzwa chakula cha Mamba Kagera ambao tunaaambiwa walikuwa platoon 3 mpk 6 zilizomiminiwa Mizinga na Askari wa amini wakitaka kuvuka mpaka kuingia Uganda kwa mitumbwiii
Sent using Jamii Forums mobile app