Nilikuwa katika mazingira ya jeshi la akiba wakati huo, na siyo kweli kuwa Jeshi la Uganda lilikuwa liko vizuri sana kuliko la Tanzania.
Wale askari wetu waliokufa wengi kwa kipindi kimoja ni wale waliotumwa na Brigadia Yousufu Himid ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa Brigade Commander wa Brigedi ya Magharibi kabla ya kuondolewa (kwa kosa hilo) na nafasi yake kukaimiwa na Kanali Kotta - baba yake na Faraja Kotta.
Brigedia huyo aliituma battalion kadhaa zivuke mto kwa mitumbwi kuingia hilo enelo llililokuwa limetekwa baada ya daraja kuvunjwa. Kwa vile upande ule uliokuwa umetekwa ni high tactical ground ndiyo maana askari wa Tanzania waligundulika na kuuwawa kwa vile walikuwa wanajiandaa kuvuka na bunduki tu, bila ya kuwa na silaha kubwa. Askari wetu wa kwanza kuingia Uganda kukomboa ile sehemu iliyokuwa imetekwa na kusaidia ujenzi wa daraja la muda walipitia Rwanda.
Ni vivyo hivyo pia kwa kupitia Rwanda ilikuwa ni rahisi wao kuingia ndani zaidi ya uganda kwa upande wa Magharibi, hivyo hata mashambulizi makubwa ya kuingia Kampala yalitokea huko Magharibi, na ni kweli askari wetu wengine walishafika mbali karibu na Sudan kabla ya kuja kushambulia Uganda.
Kikosi Kikikubwa cha Idi Amini ni kile kilichokuwa kinaitwa Simba Batallion kilichokuwa na makazi yake pale Masaka ambacho baadaye kilikuja kusaidiwa na askari wa Libya wakati wa yale mapambano ya Lukaya. Kikosi kile cha Simba Batallion kilizingirwa pia na majeshi ya Tanzania kutokea Magharibi kikiongoizwa na Brigadier Imran Kombe na Major General Marwa, ndipo Amini alipotuma wale askari wa Libya waje kusaidia na kufanya mapambano ya Lukaya kuwa makali sana lakini mwishowe Simba Batallion na askari wa Libya wakasalimu Amri na kuiacha Baracks ya Masaka mikononi mwa Imran Kombe. Ukishaondoa hiyo Simba batallion na Askari wa Libya, sehemu kubwa ya jeshi la Amin lilikuwa ni "maharage ya Mbeya tu"
View attachment 1478112
Rangi ya nyekundu ndiyo iliyokuwa ruti ya kwanza kuingilia Uganda, halafu ruti ya kijani ndiyo ilikuwa ruti ya pili baada eneo la kaskazini mwa mto Kagera kusafishwa na daraja la muda kujengwa