Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Ndivyo ulivyosema hivyo kwenye post yako ya 106# ?? Umechanganyikiwa ?? 😜 😜 😜 😜
Nadhani sasa kweli "umechangikiwa" kweli kwa vile ndilo hali iliyokukaa kichwani sana. Siwezi kukufundisha namna ya kujenga na kutetea hoja zako, ila usitake kuwa mtu wa maneno ya mkatomkato usyoweza kutetea kwa ushahidi thabiti.
 
Ni kweli, kuna watu wengi walikufa ila hawawezi kufikia askari 5000 kwa sababu jeshi letu lilikuwa na brigedi tano tu kwa hiyo askari 5000 ingekuwa ni karibu robo tatu ya brigedi nzima. Kumbuka ni vita ambayo tulivamiwa kwa hiyo kuna raia wetu wengi waliokufa baada ya uvamizi kabla vita haijaaza. Namba za Nyerere zinaweza kuwasahihi zaidi kwa vile zinahusu askari wa jeshi ambao walikuwa na namba za kijeshi na zinaweza kuwa hazihusishi askari wa akiba kama mgambo na JKT.
Unajibu kisomi sana with facts n experience.✌✌ bravo kutupa shule sie vijana wa late 80's
 
Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (1953-1985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa nchi yetu, alikuwa kiungo pekee kati ya Chama (CCM), Serikali na Kanisa Katoliki.

Agosti 3, 1970 Mwalimu Nyerere, alimwita Ikulu Padri Rweyemamu katika mazungumzo maalum ambapo Nyerere alimuahidi Rweyemamu kuwa, hivi sasa Kanisa ndilo lililoshika hatamu za kuongoza dola naye atahakikisha hali inaendelea kuwa hivyo.

“Tanzania is not Catholic country, but Catholics is strong, I want to give the church a better chance here”.

Akiwa na maana kwamba:- japo “Tanzania si nchi ya Kikatoliki, lakini Ukatoliki una nguvu, hivyo nataka kulipa Kanisa nafasi ya pekee hapa nchini” (Msome, Bergen Uk. 335)
Hivi hizi mada za udini mnataka ziwapeleke wapi? Niwaambie kitu tumetawaliwa na waingereza na wajerumani kwa maana hiyo walikuwa kipa umbele chao ni kujenga mashule tofauti na waarabu.Kwa sababu hizo ndio maana wakristo walionekana wako juu kielimu kuliko waislamu.
Acheni mada za udini hazijengi zinabomoa.kama mnasema Nyerere alikuwa anajenga ukatoliki mbona alitaifisha mashule yao na hospitali kubwa kama Bugando? achene hizo wengine hapa JF mwaka 1979 walikuwa hawajaja dunia hii
 
Nadhani sasa kweli "umechangikiwa" kweli kwa vile ndilo hali iliyokukaa kichwani sana. Siwezi kukufundisha namna ya kujenga na kutetea hoja zako, ila usitake kuwa mtu wa maneno ya mkatomkato usyoweza kutetea kwa ushahidi thabiti.

Kwani nikuomba unifundishe kujenga hoja ?? wewe umejenga hiyo hoja na context hutaki kuleta , unanilaumu na kumwaga povu , mara huyo mtu tuna wasiliana naye mara umeleta hicho ulichowasiliana naye ni vichekesho vitupu

umeondoa kitu gani hapa

mara nimefuta link .
1592220531066.png

Kweli umechanganyikiwa au maji ya Dodoma yamekuzidi
 
Hivi hizi mada za udini mnataka ziwapeleke wapi? Niwaambie kitu tumetawaliwa na waingereza na wajerumani kwa maana hiyo walikuwa kipa umbele chao ni kujenga mashule tofauti na waarabu.Kwa sababu hizo ndio maana wakristo walionekana wako juu kielimu kuliko waislamu.
Acheni mada za udini hazijengi zinabomoa.kama mnasema Nyerere alikuwa anajenga ukatoliki mbona alitaifisha mashule yao na hospitali kubwa kama Bugando? achene hizo wengine hapa JF mwaka 1979 walikuwa hawajaja dunia hii

Sorry sijanukuu aya yoyote kutoka biblia wala Quran hapa , naelewa kuna watu ukitoa ukweli kuhusu Nyerere na kanisa huja juu sana kwani wanaelewa Nyerere alipewa cheo gani na kanisa na amefanya nini hapa Nchini kupiga vita imani nyengine
 
Hivi hizi mada za udini mnataka ziwapeleke wapi? Niwaambie kitu tumetawaliwa na waingereza na wajerumani kwa maana hiyo walikuwa kipa umbele chao ni kujenga mashule tofauti na waarabu.Kwa sababu hizo ndio maana wakristo walionekana wako juu kielimu kuliko waislamu.
Acheni mada za udini hazijengi zinabomoa.kama mnasema Nyerere alikuwa anajenga ukatoliki mbona alitaifisha mashule yao na hospitali kubwa kama Bugando? achene hizo wengine hapa JF mwaka 1979 walikuwa hawajaja dunia hii

Agosti 3, 1970 Mwalimu Nyerere, alimwita Ikulu Padri Rweyemamu katika mazungumzo maalum ambapo Nyerere alimuahidi Rweyemamu kuwa, hivi sasa Kanisa ndilo lililoshika hatamu za kuongoza dola naye atahakikisha hali inaendelea kuwa hivyo.

“Tanzania is not Catholic country, but Catholics is strong, I want to give the church a better chance here”. Akiwa na maana kwamba:- japo “Tanzania si nchi ya Kikatoliki, lakini Ukatoliki una nguvu, hivyo nataka kulipa Kanisa nafasi ya pekee hapa nchini” (Msome, Bergen Uk. 335). Na hali hii ya Kanisa kuwa na nafasi kubwa Serikalini iko wazi.

Waandishi wote hawa wanatuthibitishia kuwa, kuna ukweli fulani kwamba yapo mafungamano ya dhati kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Tanzania.

Ni mafungamano hayo hayo ndiyo yameendelea kuwapa uweza viongozi wa Kanisa Katoliki kutoa maelekezo, maagizo na vilio vyao Serikalini na wakasikilizwa pamoja na kutekelezwa yale wanayoyahitaji hata kama yamelenga kuleta maafa kwa Waislamu. Mfano, mwaka 1998, Padri Lwambano, ambaye ni Paroko wa Kanisa Katoliki Mburahati Jijini Dar es Salaam, alisema kuiambia Serikali:-

“Lazima Serikali ichukue hatua kali sana kwa Waislamu wanaoendesha Mihadhara, sababu ni watu wabaya kabisa, nimepita Sinza na Mwembechai, nimekuta Waislamu hao wanamtukana Yesu wanasema Yesu si Mungu”, alisema Paroko huyo na kuongeza;

“ Kama Serikali imeshindwa kuchukua hatua kali kukomesha Mihadhara ya Waislamu na kuendelea kutupaka matope kwa mgongo wa chupa, Serikali hii ijue sisi tutalishughulikia jambo hilo kwa nguvu zetu zote”.

Kauli hii ya Padri Lwambano, ilirushwa hewani na Kituo cha Radio Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa hilo hapa nchini, Februari 13, 1998.

Padri Lwambano bila kujali kuwa imani yake inaamini ‘Yesu ni Mungu’ na Waislamu imani yao inaamini ‘Yesu si Mungu’, aliinyooshea kidole Serikali nayo ilifuata bila kujali yenyewe (Serikali) haina dini na raia wake wana dini, kwa imani tofauti.

Katika utekelezaji wa agizo hilo bila shaka kila mtu anakumbuka kilichotokea.

Ama kwa wale ambao walikuwa ni wadogo kipindi hicho ni kwamba Jeshi la Polisi lilifika Msikiti wa Mwembechai na kuuwa Waislamu kwa risasi na kikumbukumbu ni maarufu kwa ‘Mauaji ya Mwembechai’.

Kufuatia madai hayo ya Padri Lwambano, viongozi kadhaa wa nchi walifikia hatua ya kuliomba radhi Kanisa Katoliki na Wakristo kwa ujumla. Majina na vyeo vya viongozi hao wakuu wa Serikali yanafahamika.

Baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi, kazi ya kukatili maisha ya Waislamu na kubaka haki zao, kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini Polycarp Kadinali Pengo, aliipongeza Serikali kwa upande mmoja na Polisi kwa upande wa pili kufuatia mauaji hayo hayo ya Waislamu, Mwembechai.

Pongezi hizo alizitoa April 12, 1998 wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Dar es Salaam (DTV). Kanisa likionekana kuuchukukia vilivyo Uislamu, liliongeza harakati za siri na za wazi na kwa kutumia nguvu za dola ili kupunguza kwa upande mwingine nguvu ya Uislamu, maana kuuzima kabisa ni jambo lisilowezekana.

Askofu Mkuu Pengo alitoa taarifa ya kuenea Uislamu hapa Tanzania huku akihitaji msaada wa hali na mali katika kuhidhibiti hali hiyo. Na kwa kweli serikali ilitekeleza kudhibiti , Mihadhara na Wahadhiri, ambapo wahadhiri maarufu nchini wakiongozwa na Habib Mazinge, walitiwa mbaroni na kutupwa Magerezani.

Aidha sehemu ya taarifa yake ilisema hivi; “Uislamu umekuwa tishio kubwa sana kwa imani ya Kikristo nchini Tanzania, iwapo mihadhara ya Waislamu itaachwa iendelee, Kanisa litegemee kukimbiwa na waumini wake na kusilimu, kwa hiyo juhudi lazima zifanywe kuzuia Mihadhara hiyo.

“Tunashindwa kujibu hoja zao Waislamu sababu zina ukweli ndani yake”, maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Askofu Pengo kiitwacho Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenye vijilia Sinodi ya Maaskofu wa Afrika kwa ajili ya Afrika.
 
Kwani nikuomba unifundishe kujenga hoja ?? wewe umejenga hiyo hoja na context hutaki kuleta , unanilaumu na kumwaga povu , mara huyo mtu tuna wasiliana naye mara umeleta hicho ulichowasiliana naye ni vichekesho vitupu

umeondoa kitu gani hapa

mara nimefuta link . View attachment 1479329

Kweli umechanganyikiwa au maji ya Dodoma yamekuzidi
Nimeondoa kopi ya email mojawapo ya mawasilino baina yangu na Dr Sivalon, kwa hiyo inawezekana hukuwa umesioma: jambo zuri sana hilo. Hiyo contact ni public information kwa kwa kila mtu kusoma na wala siyo ya kufichwa
 
Kwa taarifa yako majeshi ya Uganda yalikuwa vizuri sana kabla ya uasi.

Vita ilipoanza tulipoteza wanajeshi wengi mno japo taarifa zilifichwa, binamu yangu amepigana na amesimulia mengi mno ambayo serikali haikuweka na haitaweka wazi.

Hivyo unaposema kwani tulizunguka, unafikiri hao jamaa walikuwa dhaifu kiasi hicho?

Vita ina mbinu nyingi, moja wapo ni kumzunguka adui wakati yeye anapambana na wale waliom face... ghafla snashangaa anashambuliwa eneo ambalo asikutegemea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Behind enemy line
 
Hii ni mentality ya kutokujiamini tu, kudhani kuwa sisi ni inferior kwa kila kitu. Vile vile ni kutokuelewa historia halisi

Elewa kuwa jeshi la Uganda wakati huo lilikuwa chini ya Amini, siyo kuwa Jeshi lilikuwa limegawanyika. Chanzo kikubwa cha kuelekea Amin kumpindua Obote ni kwa vile alikuwa anasuka jeshi kuwa lake na kuwa ana-sideline wasiokuwa wafuasi wake kwa kutumia hela za serikali, na Obote alipomtaka aeleze matumizi ya hela za jeshi ndipo akaamua kumpindua. Ni kikundi kidogo kilichokuwa kimebaki upande wa Obote ambacho ndicho kilikimbilia Tanzania kikiongozwa na akina Oyite Ojok na Tito Okello ambacho kiliitegemea sana Tanzania kwa miaka yote minane ya utawala wa Amini; kilikuwa hakifiki hata batallion moja. Baada ya kuangushwa kwa Amini na jeshi lote la Uganda kuvunjwa na TPDF, ndipo UPDF ilipoanzishwa na kufundishwa na TPDF, unaweza kuona hata jina lenyewe. Mvutano wa madaraka uliotokea ndani ya Uganda baada ya Amini kuwa amsheaangushwa na jeshi letu kuwa limesharudi nyumbani ndio uliosababisha Museveni aanzishe jeshi lake la msituni NRA ikiwa ni mwaka 1983. Museveni mwenyewe alipandikizwa kutokea Tanzania; wengine ni kama Dani Wadada Nabudere ambaye alikuwa anafundisha UDSM kabla ya vita.

Hata kama unaidharau Tanzania, kubali kuwa TPDF ilikuwa jeshi imara sana wakati huo. Kumbuka lilikuwa limeshapitia mapigano mabalimbali kusini mwa Afrika kwa hivyo lilikuwa na experience kubwa sana kuliko jeshi lolote Afrika ya Mashariki.
Mkuu unaweza kueleza kifupi kuhusu Lt.Col Nshimanyi kua baada ya vita hii alinyongwa na ilikuaje?
 
Sina habari yake sawasawa ila najua wazi kuwa hakuna kamanda yeyote aliyenyongwa kwa ajili ya vita ile, hata cpl licha ya lt col. inawezekana alifanya makosa ya jinai baada ya vita na akahukumiwa kwa sheria za uraiani wakati na mimi nimeshaondokana na mambo ya kijeshi, lakini makamanda wote wa vita walipewa heshima kubwa sana. karibu wote walipandishwa vyeo
 
What's your point sasa? Kumtoa Idi Amin kulikuwa kulinda nchi au Dini? Au vyote?

Unajua alipopinduliwa Obote , Nyerere alianza chokochoko nyingi dhidi ya Amin. Obote wakati huo yuko Tz . Alipoulizwa Karume atoe maoni yake kutokana na mapinduzi yale , aliuliza kwani waliompindua Obote ni waingereza akaambiwa ni Waganda. Akasema kama ni waganda kwa waganda basi ni wenyewe , waachieni labda hawamtaki Obote.
Majanga yote kaleta Nyerere ,angalijikalia kimya akajenga uchumi wa nchi yake yasingalitokea .
 
Chokochoko ni kawaida kwenye masuala ya mahusiano ya nchi, wiki iliyopita hata hivi sasa tuna chokochoko na Kenya. Kwahiyo Idi Amin baada ya ChokoChoko ndio akaamua kutuvamia?
 
Hawakukatiza mkuu, ni kwamba majeshi ya Tanzania yalitembeza kichapo kwa Idd Amin, wakaingia hadi kaskazini na magharibi mwa nchi ya Uganda, wakafika kwenye mipaka ya Uganda na Zaire(DRC), mipaka ya Uganda na Sudan. Mji wa Arua uliopo kaskazini mwa Uganda ndio kipo kijiji cha Koboko, kijiji alichozaliwa Idd Amin Dada

Waliingia huko wakiwa na mzuka wa mapambano. Amin akasalimu amri, akakimbia Uganda na kuacha majeshi ya Tanzania(Wakombozi) yakiikamata Uganda
Umenikumbusha mbali sana mkuu
 
Chokochoko ni kawaida kwenye masuala ya mahusiano ya nchi, wiki iliyopita hata hivi sasa tuna chokochoko na Kenya. Kwahiyo Idi Amin baada ya ChokoChoko ndio akaamua kutuvamia?

Sijachanganyikiwa kwani Idd Amin hakuzuka tu akavamia. Kosa ni la Nyerere kumkumbatia rafiki yake Obote . Mambo ya Uganda angaliwaachilia Waganda na ghasia zao . Mbona hakuivamia Kenya wala Sudan wala Kongo ??

Niliandika kabla hawa wapinzani wa Uganda walikuwa wakiingia Uganda kutokea Tanzania na kufanya vitendo vya Ugaidi .
 
Hicho unachoita "Kuwachilia Waganda" kwenye GeoPolitics hakipo, nyumba ya jirani ikiwa inawaka moto; na wewe ukajifanya haukuhusu, utakuja kushangaa umehamia kwako. Wewe unadhani hata wao hawajali kuhusu yanaondelea Tanzania? Tatizo ni pale unapoenda kuvamia nchi nyingine.

On point ya Idi Amin kutovamia nchi nyingine, kasome; mwaka 1976 alitishia kuvamia Kenya, na upumbavu huu huu wa kusema kuna kipande cha Kenya ni cha Uganda.
 
Pumba kabisa wewe kwani kumbe unaongea mambo usiyoyajua bali ya kuhadithiwa tu. Hata hujui kuwa mahindi ya Yanga yalikuja kutoka wapi halafu unakuja hapa kupiga kelele.

Kwa vile mimi ni mwalimu nitakufundisha ifuatavyo. Mahindi ya Yanga yaliingia Tanzania mwaka 1975 kutokana na ukame uliokuwa umeikumba nchi mwaka 1973 na 1974 ikiwa ni muda mfupi sana baada ya opereshini vijiji ambayo ilivuruga kilimo cha asili na kuacha watu hawana chakula; na ulikuwa ni msaada ulioidhinishwa na Rais Jimmy Carter wa Marekani kupitia USAID.

Ule mchele wa Jasmine kutoka Thailand haukutolewa msaada kwa ajili ya vita, bali ulianza kuagizwa kuingia nchini wakati wa utawala wa rais Mwinyi na wafanya biashara binafsi baada ya Liberalization; hiyo ni pamoja na mafuta yakupikia ya OKI kutoka Singapore. Kama unazungumza unga wa Yanga baada ya vita ni kuwa hukuwepo na wala hujui hali halisi ya wakati ule, kwani tuliokula unga ule mpaka mwaka 1977 hatusemi vile.

Vita iliaza mwaka 1979 wakati nchi haina unga wa yanga tena. Kwa upande wa pili; ni kweli kuwa uchumi wa nchi ulivurugika sana kwa sababu Tanzania ililazimika kununua silaha kali za kupambana na Amin kwa muda mfupi ambazo hazikuwa kwenye bajeti ya nchi; na ikatumia hela za kukopa zinazokaribia bajeti ya miaka miwili au mitatu hivi ya nchi ili kupata mitambo ya Balllistic misiles (BM40) mingi kuliko uwezo wake wakati ule kwa sababu amini alikuwa ameuza migodi yote ya Shaba kwa Urusi kusudi apatiwe vifaru vingi; na alikuwa na vifaru vingi sana ambavyo jeshi letu lilivivunjavuvunja kama chungu ambacho hakikupita kwenye tanuru. Kitu ambacho Tanzania tunashukuru tena kwnye vita ile ni kuwa baada ya vita kuanza, Urusi nayo ikaivamia Afghanstani kipindi hicho hicho na hivyo ikawa iko bize kupambana na Mujahedeen, ikaacha kupelea vifaru kwa Uganda tena.
Aloo afande Kichuguu unaijua vilivyo hii story mimi nilikuwa jirani na Maj Gen Marwa yule mzee alishawahi kunisimulia Kuhusu hii vita ya Kagera alinipa moral kubwa sana mpaka nikapenda jeshi.Mengine naomba nisieleze nita unlock codes
 
Back
Top Bottom