Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Sina habari yake sawasawa ila najua wazi kuwa hakuna kamanda yeyote aliyenyongwa kwa ajili ya vita ile, hata cpl licha ya lt col. inawezekana alifanya makosa ya jinai baada ya vita na akahukumiwa kwa sheria za uraiani wakati na mimi nimeshaondokana na mambo ya kijeshi, lakini makamanda wote wa vita walipewa heshima kubwa sana. karibu wote walipandishwa vyeo
Mkuu Kichuguu, habari za masiku kamanda?
Mimi wakti vita yapigika nilikuwa shule ya msingi tayari na mmoja wa wajomba zangu alikuwa huko kwenye vita na alirudi na vitu kibao.
Nikukuja kufahamu kuwa looting inaruhusiwa kwenye mazingira fulani maana alikuwa amerudi ana redio cassete matata sana na nilipomuuliza yauzwa kiasi gani alicheka sana, akisema "usiulize masuali kama hayo jomba".
Nakumbuka nyakati za jioni nikienda likizo kijijini Uncle alikuwa akitupatia story kabambe za wajeda wa JWTZ na yeye ndie alienipa mawazo ya kujiunga huko baada ya JKT.
Nilifuatilia sana magazeti ya Mzalendo, Uhuru, Mfanyakazi na Daily News (nilianza kusoma mwenyewe na kuandika nikiwa na miaka 5) na kwa kweli magazeti yetu yalipiga kampeni kabambe juu ya kumwondoa nduli Iddi Amin.
Nakumbuka picha ya joka kubwa likiwa nyumbani na mchoraji anasema "joka limeingia nyumbani na watoto wamechachamaa joka kulitoa ndani"
Lakini mkuu Kichuguu nikuulize masuali miwili matatu, vipi michango wa vijana wawili kwa Hayati Mwalimu kama Paul Kagame na M7?
Kama PK alitusaidia kwa upande wa Rwanda basi yawezekana pasi na shaka kwamba M7 nae alitusaidia upande wa Kaskazini khasa Mutukula ambapo ndipo ulipo mpaka kati ya Tanzania na Uganda.
Kuhusu Moshi Conference ambayo iliratibiwa na Hayati Mwalimu je, ilikuwa halali kwa Hayati Mwalimu kutaka kuhalalisha waasi wa Obote?
Kwasababu baada ya mikutano huo ndipo kikaanzishwa chama cha UNLF na baadae pia kuanzishwa kwa UNLA.
Tuelezee kidogo juu ya kikosi kazi "Task Force" kilichoongozwa na Meja janerali Silas Mayunga ambacho kiliundwa na brigedia ya Minziro naingine ambayo nimeshahau kama ni brigedia ya 206 au 208.
Mwisho unafikri ni kwanini Hayati Mwalimu alikubali makubaliano ya Mogadishu Agreement halafu baadae akayapinga yalosimamiwa na raisi wa Somalia wakti ule Siad Barre.
Mogadishu Agreement ilifikiwa kwa kila nchi kurudi nyuma kilomita 10 kutoka mpakani.
Hatua hizi za Hayati Mwalimu ndizo zilizopelekea kuanguka kwa Umoja wa Afrika Mashariki kwa vile Kenya nao waliona Hayati Mwalimu ana msimamo wa aina yake juu ya hii Kagera Salient.
Je, bado Uganda wanaweza kuwa bado wanafikiria hii sehemu ya Kagera Salient?
Kwa sababu mpaka huu ulichorwa na wakoloni wa Uingereza na Ujerumani wkati wa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia.