Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Mkuu 2000
Ni Battalion mbili hizo.

Na makadirio huenda tulipoteza Battalion 3
 
Mkuu Kunguni kwanza kabisa Pole na stress za corona,

Tangu inchi ipate uhuru ni miaka takribani 17 pekee ilikuwa imepita, ndio tukakutana na janga la vita nchii ilikuwa haijakomaa na sidhani hata kama ilikuwa na akiba hata ya asilimia 40% ya kifedha.
Vita inahitaji fedha,

Na nchi yetu haikuwa na uchumi ya vyema ilikuwa ni nchi changa.

Na kwa wakati huo mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akihitaji watu wajitolee na ndio maana kuna watu walikuwa wanatoa ng'ombe, fedha, kusafirisha watu walio jitolea kwenda vitani, magari, na vitu vingine vingi.

Russia pia na Cuba zina mchango kwetu wakati wa hii vita,
Hivyo ilikuwa ni kweli uchumi ulishuka sababu tulitumia chakula kingi wakati wa vita na kama ujuvyo uzalishaji ulipungua,

sasa wewe kichwa maji unakuja hapa jukwaani kama kumtuhumu mwl, Utadhani yeye ndie aliesababisha hiyo vita.
 
Kiuhalisia ile vita haikuwa na Ulazima

Watanzania walikufa wengi sana kuliko Waganda.
Watoto wa 2000 wanapojaribu kuzaliwa 1960

Mdogo wangu vita haikuwa ya ulazima wakati Nduli Iddi Amini Dada alivamia Mkoa wa Kagera kwa madai ya kwamba ile ni sehemu ya uganda lazima aichukue.

Kwa hiyo mwl. JKN angewaachia..!?
 
Wanajeshi wengi wa Amini walitokea Sudan wakati huo Sudan ni moja walikuwa wanubi pia kabila lake la kakwa lilikuwa karibu na Sudan mpakani inawezekana base yao ilikuwa huko

Kuhusu uchumi kushuka hivi unaelewa kwanini Marekani baada ya vita huwa anaingia mikataba ama ya kuchukua mafuta au vitu vingine kulipia gharama? Vita yoyote ina gharama na sisi baada ya vita Uganda alitakiwa kutulipa sijui malipo yalifikia wapi ila kuna kipindi museveni aliomba yasamehewe
 
Mkuu 2000
Ni Battalion mbili hizo.

Na makadirio huenda tulipoteza Battalion 3
Ni kweli inawezekana sana kwani sina mahesabu kamili haraka haraka kichwani, ila wakati ule batalian moja ilikuwa na kombania saba pamoja na hedikwota COY, na kila kombania ilikuwa na platuni tatu pamoja na ile ya hedikwota zote kwa pamoja zikiwa na kama askari kama 120 mpaka 130 hivi-sitaki kwenda kwa kina zaidi juu ya Organization ya wakati huo. Sasa ukipiga hseabu hiyo mara saba kwenye Battalion moja ni kama askari 910 ambao ukijumulisha na na HQ COY unapata kamaaskari kama 1260. Ila sasa Batallion za kivita wakati huo zilikuwa ni kubwa zaidi ya orgaization hiyo kwa sababu ya Mgambo, magereza, JKT na Polis waliunganishwa katika Batallions hizo.

Jamaa wa Wikipedia wanatoa namba za vifo kama ifuatavyo kwa hiyo hawakufika 2000 wala Batallion moja ya kawaida. Ila majeruhi walikuwa wengi zaidi.

 
Pumba kabisa wewe kwani kumbe unaongea mambo usiyoyajua bali ya kuhadithiwa tu. Hata hujui kuwa mahindi ya Yanga yalikuja kutoka wapi halafu unakuja hapa kupiga kelele.

Kwa vile mimi ni mwalimu nitakufundisha ifuatavyo. Mahindi ya Yanga yaliingia Tanzania mwaka 1975 kutokana na ukame uliokuwa umeikumba nchi mwaka 1973 na 1974 ikiwa ni muda mfupi sana baada ya opereshini vijiji ambayo ilivuruga kilimo cha asili na kuacha watu hawana chakula; na ulikuwa ni msaada ulioidhinishwa na Rais Jimmy Carter wa Marekani kupitia USAID.

Ule mchele wa Jasmine kutoka Thailand haukutolewa msaada kwa ajili ya vita, bali ulianza kuagizwa kuingia nchini wakati wa utawala wa rais Mwinyi na wafanya biashara binafsi baada ya Liberalization; hiyo ni pamoja na mafuta yakupikia ya OKI kutoka Singapore, ambayo ilikuwa ni kwa sababu za kibiashara kushindana sokoni tu. Kama unazungumza unga wa Yanga baada ya vita ni kuwa hukuwepo na wala hujui hali halisi ya wakati ule, kwani tuliokula unga ule mpaka mwaka 1977 hatusemi vile.

Vita iliaza mwaka 1978 wakati nchi haina unga wa yanga tena. Kwa upande wa pili; ni kweli kuwa uchumi wa nchi ulivurugika sana kwa sababu Tanzania ililazimika kununua silaha kali za kupambana na Amin kwa muda mfupi ambazo hazikuwa kwenye bajeti ya nchi; na ikatumia hela za kukopa zinazokaribia bajeti ya miaka miwili au mitatu hivi ya nchi ili kupata mitambo ya Balllistic misiles (BM40) mingi kuliko uwezo wake wakati ule kwa sababu amini alikuwa ameuza migodi yote ya Shaba kwa Urusi kusudi apatiwe vifaru vingi; na alikuwa na vifaru vingi sana ambavyo jeshi letu lilivivunjavuvunja kama chungu ambacho hakikupita kwenye tanuru. Kitu ambacho Tanzania tunashukuru tena kwnye vita ile ni kuwa baada ya vita kuanza, Urusi nayo ikaivamia Afghanstani kipindi hicho hicho na hivyo ikawa iko bize kupambana na Mujahedeen, ikaacha kupelea vifaru kwa Uganda tena.
 
Bila shaka unafahamu umri wangu!
Hata kama sijui umri wako; ni wazi kuwa hukuwapo duniani hapa kabla ya mwaka 1986 wakati ambapo mchele wa Jasmin kutoka Thailand unaanza kuingia nchini. Kwa hiyo wakati vita inaaza mwaka 1978 ulikuwa bado unaishi sehemu fulani ya kufikirika tu, ndiyo maana unatoa maneno ya kufikirika tu.
 
Kiuhalisia ile vita haikuwa na Ulazima

Watanzania walikufa wengi sana kuliko Waganda.

Yaani jirani yako akija nyumbani kwako na kumbaka mke wako mbele yako utasema hakuna haja ya kumpigania mke wako? Nachukulia kama wewe ni mtoto wa kiume. Iwapo vita ile haikuwa na ulazima, basi hatuna haja ya kuwa na JWTZ tena
 

Kumbe unakubaliana na maelezo yangu kuwa mchele wa Tailendi umeanza kuingia Bongo baada ya vita ya Uganda.

Halafu, weka jazba pembeni. Kuweka record ni kuwa IDD Amin alivamia mpakani mwa Uganda na TZ (akaingia maeneo ya Kagera)

Unakubali kuwa vita haikua na ulazima?

Kwamba ilikua inatosha kumwondoa adui mpakani arudi kwake, tubaki tukilinda mipaka yetu.

Kulikua na haja gani kwenda mpaka Kampala hadi Sudani huko na kuyaacha majeshi yakilinda usalama huku yakiendelea kutumia rasilimali za Tanzania?

Kwanini baada ya kumkimbiza Amini pale Kagera wasingerudi na kubaki kulinda mipaka tu na kuwaacha Waganda wapambane na uongozi wao?
 
Sasa mkuu wangemuacha Idd Amin kisa washamtoa Kagera si angejipanga akarudi tena?

 
Mzee wangu alishriki hii vita na alikuwa askari polisi
 
Kwataarifa yako mkuu, bado Uganda iko njema kivifaa vya vita
 
Ina semekana kuwa bila mgawanyiko wa majeshi ya Uganda basi jamaa wangetuchapa ile mbaya...tuwashukuru sana akina mseveni
Hii ni mentality ya kutokujiamini tu, kudhani kuwa sisi ni inferior kwa kila kitu. Vile vile ni kutokuelewa historia halisi

Elewa kuwa jeshi la Uganda wakati huo lilikuwa chini ya Amini, siyo kuwa Jeshi lilikuwa limegawanyika. Chanzo kikubwa cha kuelekea Amin kumpindua Obote ni kwa vile alikuwa anasuka jeshi kuwa lake na kuwa ana-sideline wasiokuwa wafuasi wake kwa kutumia hela za serikali, na Obote alipomtaka aeleze matumizi ya hela za jeshi ndipo akaamua kumpindua. Ni kikundi kidogo kilichokuwa kimebaki upande wa Obote ambacho ndicho kilikimbilia Tanzania kikiongozwa na akina Oyite Ojok na Tito Okello ambacho kiliitegemea sana Tanzania kwa miaka yote minane ya utawala wa Amini; kilikuwa hakifiki hata batallion moja. Baada ya kuangushwa kwa Amini na jeshi lote la Uganda kuvunjwa na TPDF, ndipo UPDF ilipoanzishwa na kufundishwa na TPDF, unaweza kuona hata jina lenyewe. Mvutano wa madaraka uliotokea ndani ya Uganda baada ya Amini kuwa amsheaangushwa na jeshi letu kuwa limesharudi nyumbani ndio uliosababisha Museveni aanzishe jeshi lake la msituni NRA ikiwa ni mwaka 1983. Museveni mwenyewe alipandikizwa kutokea Tanzania; wengine ni kama Dani Wadada Nabudere ambaye alikuwa anafundisha UDSM kabla ya vita.

Hata kama unaidharau Tanzania, kubali kuwa TPDF ilikuwa jeshi imara sana wakati huo. Kumbuka lilikuwa limeshapitia mapigano mabalimbali kusini mwa Afrika kwa hivyo lilikuwa na experience kubwa sana kuliko jeshi lolote Afrika ya Mashariki.
 
Mambo haya mazuri sana Unaweza kukubali tukufanyie Mahojiano Tuandike kitabu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…