Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?


Mkuu Kichuguu, habari za masiku kamanda?

Mimi wakti vita yapigika nilikuwa shule ya msingi tayari na mmoja wa wajomba zangu alikuwa huko kwenye vita na alirudi na vitu kibao.

Nikukuja kufahamu kuwa looting inaruhusiwa kwenye mazingira fulani maana alikuwa amerudi ana redio cassete matata sana na nilipomuuliza yauzwa kiasi gani alicheka sana, akisema "usiulize masuali kama hayo jomba".

Nakumbuka nyakati za jioni nikienda likizo kijijini Uncle alikuwa akitupatia story kabambe za wajeda wa JWTZ na yeye ndie alienipa mawazo ya kujiunga huko baada ya JKT.

Nilifuatilia sana magazeti ya Mzalendo, Uhuru, Mfanyakazi na Daily News (nilianza kusoma mwenyewe na kuandika nikiwa na miaka 5) na kwa kweli magazeti yetu yalipiga kampeni kabambe juu ya kumwondoa nduli Iddi Amin.

Nakumbuka picha ya joka kubwa likiwa nyumbani na mchoraji anasema "joka limeingia nyumbani na watoto wamechachamaa joka kulitoa ndani"

Lakini mkuu Kichuguu nikuulize masuali miwili matatu, vipi michango wa vijana wawili kwa Hayati Mwalimu kama Paul Kagame na M7?

Kama PK alitusaidia kwa upande wa Rwanda basi yawezekana pasi na shaka kwamba M7 nae alitusaidia upande wa Kaskazini khasa Mutukula ambapo ndipo ulipo mpaka kati ya Tanzania na Uganda.

Kuhusu Moshi Conference ambayo iliratibiwa na Hayati Mwalimu je, ilikuwa halali kwa Hayati Mwalimu kutaka kuhalalisha waasi wa Obote?

Kwasababu baada ya mikutano huo ndipo kikaanzishwa chama cha UNLF na baadae pia kuanzishwa kwa UNLA.

Tuelezee kidogo juu ya kikosi kazi "Task Force" kilichoongozwa na Meja janerali Silas Mayunga ambacho kiliundwa na brigedia ya Minziro naingine ambayo nimeshahau kama ni brigedia ya 206 au 208.

Mwisho unafikri ni kwanini Hayati Mwalimu alikubali makubaliano ya Mogadishu Agreement halafu baadae akayapinga yalosimamiwa na raisi wa Somalia wakti ule Siad Barre.

Mogadishu Agreement ilifikiwa kwa kila nchi kurudi nyuma kilomita 10 kutoka mpakani.

Hatua hizi za Hayati Mwalimu ndizo zilizopelekea kuanguka kwa Umoja wa Afrika Mashariki kwa vile Kenya nao waliona Hayati Mwalimu ana msimamo wa aina yake juu ya hii Kagera Salient.

Je, bado Uganda wanaweza kuwa bado wanafikiria hii sehemu ya Kagera Salient?

Kwa sababu mpaka huu ulichorwa na wakoloni wa Uingereza na Ujerumani wkati wa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia.
 
Je Machel kichinichini hakumpa askari kadhaa wa Frelimo nyerere kuongeza nguvu?
 
Nyerere huyu mnaemuita mdini amae alikuwa anaratibu mfumo Ukristo(ukatoriki) ndo huyo huyo aliweka kamfumo kasiko rasmi kwenye katiba kwenye kupokezana urais kati ya hizi dini mbili kuu hapa nchini.
WAISLAM WAKATI MWINGINE MJITAHIDI KUFICHA UJINGA WENU ILI JAMII IWAHESHIMU
 
Hapa kuna maswali mengi nitajitahidi kujibu moja moja kama ifuatavy:

(1) Wakati wa mapambano kulijitokeza vikundi vingi vya kumpinga Amini hivyo Mwalimu akawashauri waungane ndipo wakawa na ule Mkutano wa Moshi. PK hakuwa mwanajeshi wakati huobali alikuwa raia wa kawaida mkimbizi huko Uganda. Tanzania ilipita Rwanda wakati wa Hyabarimana, na siyo kuwa walitusaidia bali tulipita mpakani na wala hawakujua kuwa jeshi letu lilikuwa limepita huko; makamanda wetu walitaka usiri wa hali ya juu sana. M7 naye alikuwa na kikundi chake ambavyo vyote viliunganishwa kuwa kundi moja kubwa likiongozwa na Yusuf Lule. Wakati huo M7 naye alikuwa anaishi tanzania kama mkimbizi.
(2) Mkutano wa Moshi haukuwa wa kuhalalisha waasi wa Obote, kama nilivyosema hapo uliunganisha vikundi vyote vilivyojitokeza kumpinga Amini. Wakati huo Nyerere alishaona kuwa Amin ataanguka na hakutaka aache ombwe la uongozi wala Tanzania ndiyo iitawale Uganda, hivyo alikuwa anawaandaa waganda wajitawale wenyewe baada ya Amini kuangushwa.
(3)Ni kweli Nyerere alikuwa anamshabikia Obote kutokana na historia ya kuelewana kwa muda mrefu - walikuwa na Mulungushi Club, kwa bahati mbaya nadhani hakujua kuwa waganda walikuwa hawamtaki kabisa. Kwa hiyo wakati Obote anashinda uchaguzi wa kwanza baada ya vita waganda walipinga vikali matokeo yale, na ndiyo iliyoleteleza M7 aanzishe jeshi lake la msitunii. Ndipo aliaandikisha wanyarwanda wengi wakimbiizi ksms akina Fred Rwigyema an Paulo Kagame.
(4) Makubalino ya Mogadishu yaliratibiwa na Siad Barre na Tanzania ikiwakilishwa na Samwel Malecela wakati akiwa waziri wa mambo ya nje. Makubalinao yalifanyika baada ya kikundi cha Obote kuwa kimejaribu kuingia Uganda muda mfupi baada ya mapinduzi kikitokea Tanzania na kikapigwa vibaya na askari wa Amin ambaye aliamua kuishambulia Tanzania akaangusha mabomu Mwanza akilenga Hospitali ya Bugando na Makao makuu ya Tanu- bahati nzuri mabomu ya;le yote yakaanguka majini. Kwa hiyo makubaliano hayo yakawa yanazuia kushambuliana tena. Makubaliano yale yalikosa thamani tena baada ya Amini kuvamia Tanzania na kuchukua lile eneo la kagera; alikuwa anadai kuwa mpaka halali ulikuwa ni mto Kagera. Alifanya hivyo bila kuchokozwa.
(5) Afrika ya Mashariki ilianguka kutokana na shinikizo la Charles Njonjo kwa Kenyata mwaka 1977 kabla ya vita; hakukuwa na uhusiano kabisa na vita ile wala mfarakano wa Nyerere na Amini haukuwa sabau ingawa unaweza kuwa ulichangia kwa kutokuwepo diplomacy ya kutosha kipindi hicho. Nyerere aliwahi kukutana na Amin mara nyingi sana, siku moja walikutania Mwanza. Mpaka leo ukimsikia Njonjo ana miaka zaidi ya 100 bado hataki shirikisho. Siku moja nilimsikia akihojiwa na Jeff Koinange na bado akasisistiza kuitaka Kenya ijitoe kwenye Jumuia.
 
Alitaifisha shule na hospitali zote za wakristu kusudi watu wa dini zote wasome na wapate matibabu bure. Dini za kikristo zilikuwa na mahosptiali na mashule mengi sana kuliko serikali.
 
Hapana; Machel mwenyewe alikuwa na vita ya akina RENAMO iliyosbabisa kuwa kwa Nkomati Accord
Kuna article nilisoma inasema walikuwepo na walipitishiwa Airport ya mwanza na kuna baadhi walisahau magazeti yao ya kireno sema ilikuwa ni siri kubwa.
 
Kuna article nilisoma inasema walikuwepo na walipitishiwa Airport ya mwanza na kuna baadhi walisahau magazeti yao ya kireno sema ilikuwa ni siri kubwa.View attachment 1479973
Hiyo siyo kweli; ningejua kwa vile nilikuwa mazingira ya jeshi. Labda walileta Batallion kusaidia shughuli za ulinzi wa ndani na logistics lakini siyo kwenda frontline. Hata msumbiji kwenyewe mpaka leo hakuna kumbukumbu au medali yoyote ya vita hiyo ya Kagera. Wangekuwa wameleta Batallion ni lazima watu kadhaa kati yao wangefariki na kungekuwa na kumbukumbu yao somewhere.
 
Shukrani kwa ufafanuzi.
 

Mkuu Kichuguu ahsante kwa ufafanuzi na maelezo mazuri yaloshiba.

Ila zipo habari za Msumbiji kuisaidia Tanzania kwa kutuma batalioni ya wanajeshi kama 800 hivi.

Hawa walipelekwa moja kwa moja hadi Kagera kwa ndege.

Inawezekana hawa walikwenda kuongeza nguvu kwenye operesheni Chakaza.

Jaribu kutafuta hiii madini ipo mahala.

Ila kwa hakika Tanzania ina historia ya majenerali ambao walikesha wakihakikisha nchi iko mikono salama.

Viongozi wa kijeshi wa kukumbukwa vita vya Kagera:

John Butler Walden- Black Mamba

Silas Mayunga -Mti Mkavu

David Msuguri Jenerali -Mtukula

Meja jenerali Ben Msuya,

Colonel Tumbi -Kamanda Radi

Meja jenerali Tumainieli Kiwelu na

Meja jenerali Mwita Marwa - Kambale
 
U Unasalimiwa na mzee mwenzako Echolima
 
Ongezea hapo
Brigedia Generali Kichuguu
Meja General Echolima
 
.

Umewasahahu Imran Kombe, Romwald Makunda na Ramadhani Haji Faki (huyu huwa anasahaulika sana kwenye kumbukumbu lakini aliongoza brigade moja frontline).

Kuhusu askari wa msumbiji kweli sina uhakika labda ilifanywa siri sana sisi maprivate hatukuweza kuijua. Ila ninachouliza ni kuwa mbona hakuna hata medali moja ya kumbukumbu iliyotolewa kwa Msumbiji, na wala hakuna hata kaburi la kumbukumbu labda kama hawakufa, lakini angalau medali zingetolewa. Nina uhakika mkubwa sana waliokuwa frontline ilikuwa ni watanzania tu, ndani ya Brigade na division ambazo zilikuwa zinaongozwa na hao makamanda uliotaja. Wakati mwingine watu walikuwa wanatengeza taarifa kutokea mitaani tu. Inawezekana walitusaidia pesa za kununulia silaha au walitugawia sehemu fulani ya silaha ingawa nao walikuwa bado ni Taifa changa lenye umri wa miaka mitano tu.
 
Kiongozi kuna sehem umeongelea "Bato ya Lukaya"

Kuna sehem inaitwa "umulwekubyo" (Kona)

Hii "bato" wanasema ndo ilimaliza vita...

1. Mapambano ya Lukaya yaliendeleaa kwa muda gani....?

2. Inasemekan hapa Amin alipoteza Askari wengi hadi kufika 300 au 400 wakiwemo walibya zaidi ya 100 na wengne kutekwa
Katika mazingira ya vita nyie mnajickiaje kuona askari zaidi ya 300 wamelala..?

3. Kama ulishiriki hii "bato" unaweza tueleza nn ilkuwa "failure" ya waganda hapa kiasi cha kupotea wengi kiasi ikii....?

4. Vita uwa ina mengi je ni kweli uko frontline kuna makafara na matambiko yalikuwepo msitunii....??

5. Kuna mahali nilisoma kuwa Kamanda Nshimanyi alkula "ambush" ambayo ilimcost askari 25~35, nn ilkuwa tatzo...??

6. Ulikuwa chini ya Kamanda yupi na katika platoon ako au battalion ako...? Unakumbk "great loss" kwen ilkuwa kupoteza askari wangap katika pambano moja

Asantee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna article nilisoma inasema walikuwepo na walipitishiwa Airport ya mwanza na kuna baadhi walisahau magazeti yao ya kireno sema ilikuwa ni siri kubwa.View attachment 1479973
Yaliyodnikwa kwenye article uliyokwoti hapa yana sehemu kubwa kupikwa tu, kwa mfano ni kuwa kati ya jambo ambalo Nyerere aliilaumu sana OAU ni kule kushindwa kumkemea Amin; Nyerere alilalamaika sana kwa nini OAU wasimkemee tu. Halafu hilo la msumbiji kama nilivyosema hapo juu sina uhakika nalo, kwani halikuwa kwenye circles za mimi kujua labda kama Echolima aliyekuwa frontline analijua, mimi sikuwa frontline. Ila vile vile inawezekana ni vivyo hivyo taarifa za kupikwa tu. Baada ya mobilization ya Mgambo, Polisi, Magereza na JKT; jeshi letu lilikuwa kubwa sana karibu mara mbili ya jeshi Uganda ndiyo maana nina wasiwasi sana kuhusu kupata msaada wa Askari kutoka Musumbiji. Labda wanazungumza askari wa Tanzania waliokuwa Musumbiji wakati huo walirudishwa nyumbani; lakini bado niko open. Kuna general mmoja wa Amini wakati huo baada ya vita aliwahi kuhojiwa na kunyesha jinsi Jeshi la Tanzania lilivyopanuka kwa muda mfupi sana kulingana na Intelligene walizokuwa wanapata. Siku nikiipata tena article ya interview hiyo nitaileta hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…