Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Kabudi anahusikaje?Na ndipo kifimbo alipofikiria kung'atuka. Ile vita kina Kabudi waliandika propaganda sana kuonyesha ushindi wakati kiuhalisia we lost
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabudi anahusikaje?Na ndipo kifimbo alipofikiria kung'atuka. Ile vita kina Kabudi waliandika propaganda sana kuonyesha ushindi wakati kiuhalisia we lost
MkuuPumba kabisa wewe kwani kumbe unaongea mambo usiyoyajua bali ya kuhadithiwa tu. Hata hujui kuwa mahindi ya Yanga yalikuja kutoka wapi halafu unakuja hapa kupiga kelele.
Kwa vile mimi ni mwalimu nitakufundisha ifuatavyo. Mahindi ya Yanga yaliingia Tanzania mwaka 1975 kutokana na ukame uliokuwa umeikumba nchi mwaka 1973 na 1974 ikiwa ni muda mfupi sana baada ya opereshini vijiji ambayo ilivuruga kilimo cha asili na kuacha watu hawana chakula; na ulikuwa ni msaada ulioidhinishwa na Rais Jimmy Carter wa Marekani kupitia USAID.
Ule mchele wa Jasmine kutoka Thailand haukutolewa msaada kwa ajili ya vita, bali ulianza kuagizwa kuingia nchini wakati wa utawala wa rais Mwinyi na wafanya biashara binafsi baada ya Liberalization; hiyo ni pamoja na mafuta yakupikia ya OKI kutoka Singapore, ambayo ilikuwa ni kwa sababu za kibiashara kushindana sokoni tu. Kama unazungumza unga wa Yanga baada ya vita ni kuwa hukuwepo na wala hujui hali halisi ya wakati ule, kwani tuliokula unga ule mpaka mwaka 1977 hatusemi vile.
Vita iliaza mwaka 1978 wakati nchi haina unga wa yanga tena. Kwa upande wa pili; ni kweli kuwa uchumi wa nchi ulivurugika sana kwa sababu Tanzania ililazimika kununua silaha kali za kupambana na Amin kwa muda mfupi ambazo hazikuwa kwenye bajeti ya nchi; na ikatumia hela za kukopa zinazokaribia bajeti ya miaka miwili au mitatu hivi ya nchi ili kupata mitambo ya Balllistic misiles (BM40) mingi kuliko uwezo wake wakati ule kwa sababu amini alikuwa ameuza migodi yote ya Shaba kwa Urusi kusudi apatiwe vifaru vingi; na alikuwa na vifaru vingi sana ambavyo jeshi letu lilivivunjavuvunja kama chungu ambacho hakikupita kwenye tanuru. Kitu ambacho Tanzania tunashukuru tena kwnye vita ile ni kuwa baada ya vita kuanza, Urusi nayo ikaivamia Afghanstani kipindi hicho hicho na hivyo ikawa iko bize kupambana na Mujahedeen, ikaacha kupelea vifaru kwa Uganda tena.
We nae huwezi kufikiri vzr.Kumbe unakubaliana na maelezo yangu kuwa mchele wa Tailendi umeanza kuingia Bongo baada ya vita ya Uganda.
Halafu, weka jazba pembeni. Kuweka record ni kuwa IDD Amin alivamia mpakani mwa Uganda na TZ (akaingia maeneo ya Kagera)
Unakubali kuwa vita haikua na ulazima?
Kwamba ilikua inatosha kumwondoa adui mpakani arudi kwake, tubaki tukilinda mipaka yetu.
Kulikua na haja gani kwenda mpaka Kampala hadi Sudani huko na kuyaacha majeshi yakilinda usalama huku yakiendelea kutumia rasilimali za Tanzania?
Kwanini baada ya kumkimbiza Amini pale Kagera wasingerudi na kubaki kulinda mipaka tu na kuwaacha Waganda wapambane na uongozi wao?
Na wewe ni Mkatoliki?We nae huwezi kufikiri vzr.
Kwa akili za amini unadhani asingerudi tena.
Fikiri tena na tena, labda hujui kwa nini tulilazimika kuingia vitani
Hivi tulikuwa na haki kuitwa jeshi la ukombozi?Hawakukatiza mkuu, ni kwamba majeshi ya Tanzania yalitembeza kichapo kwa Idd Amin, wakaingia hadi kaskazini na magharibi mwa nchi ya Uganda, wakafika kwenye mipaka ya Uganda na Zaire(DRC), mipaka ya Uganda na Sudan. Mji wa Arua uliopo kaskazini mwa Uganda ndio kipo kijiji cha Koboko, kijiji alichozaliwa Idd Amin Dada.
Waliingia huko wakiwa na mzuka wa mapambano. Amin akasalimu amri, akakimbia Uganda na kuacha majeshi ya Tanzania (Wakombozi) yakiikamata Uganda.
Nikuulize swali mkuu. Uliona wapi nchi inapigana vita, alafu uchumi wake unapanda au unabaki vile vile bila kutikisika. Hata America is better off baada ya kujitoa Afghanistan.Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)
Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita. Wanajeshi walikua hawatoshi?
Ahsante. 1979 ulikua una umri gani kaka?
Waafrika wapi hao? Unatuchanganya na Upuuzi wa watu kadhaa ....Allah amlaze mahala pema peponi ndugu yetu Idi amin, bila kumsahau Ndugu yetu na kipenzi cha waafrika kwa ujumla Muammar Gaddafi, Allah amlaze mahala pema peponi!
Vyanzo vya kimataifa vinasema tulipoteza 5000Walipotea wapi; si ajabu unasikia hadithi tu; ni kweli tulipoteza wanajeshi karibu 500 ( siyo 2000 ingawa sina namba kamili) ambayo ni karibu batallion moja, na nimekuambia kuwa katika hatua za kwanza za vita kuna karibu Batallion nzima iliyopotea kwa sababu ya uamuzi mbovu wa kamanda mmoja.
Vile vile vita ya Lukaya iliua waganda na walibya wengi sana lakini pia watanzania walikufa. Mimi nilikuwa karibu sana na taarifa za mapambano yale kuanzia mwezi Octoba mwaka 1978 (siyo 1979) kabla hata Rais hajatangaza vita yenyewe kwa vile nilikuwa kwenye Brigedi ya Magharibi ambayo ndiyo iliingia vitani kwanza.
Vita iliendelea kwa miezi saba katika mazingira magumu kama niliyosema hapo, hivyo ni kweli watu walikufa. Huwezi kupigana vita ya ardhini bila askari wako kufa. Jeshi la Uganda halikuasi bali lilielemewa nguvu na jeshi la Tanzania licha ya kuwa walikuwa wanasaidiwa na askari wengi sana kutoka Libya.
Unaposema kuwa watu wetu walielemewa sana ila baada ya hapo jeshi la Uganda likaasi ndipo tukapata unafuu- ni wazi hujui vita nini- ile siyo ngoma ya mdundiko ndugu yangu, ni kazi ya kurushiana risasi za moto, sema pia ni askari wangapi wa Uganda waliokufa kama hutapatwa na ugonjwa wa moyo iwapo unaliangalia jeshi la Tanzania wakati huo katika negative lens;
Jeshi la Uganda lilikuwa kubwa sana, Amini alikuwa anawekeza sana katika jeshi kuliko sehemu nyingine yoyote, ila sasa JWTZ ilikuwa inawafuta kama sisimizi ndipo wakafikia kukata tamaa ya kuendelea na vita ile.
Kwani vyanzo hivyo vilikuwapo vitani? Unajua askari 5000 ni sawa na Brigade ngapi za wakati huo?Vyanzo vya kimataifa vinasema tulipoteza 5000
Inakushangaza!!?..kipindi hicho watu wakibebwa mitaani kupelekwa jeshiniKwani vyanzo hivyo vilikuwapo vitani? Unajua askari 5000 ni sawa na Brigade ngapi za wakati huo?
Wacha hadithi za kusimuliwa na watu waliosimuliwa pia. Nimeshaandika humu kwa kirefu sana kuhusu vita hiyo hivyo hakuna haja ya kuanza kujibizana na mtu anayekuja hapa na hadithi za kusimuliwa wakati mimi mwenyewe nilikuwamo ndani. Eti watu wakibwebwa mitaani kwenda jeshini? Unazungumuza kwa akili timamu kweli na kwa nia ya kufahamishana ukweli au unataka na wewe uchangie?Inakushangaza!!?..kipindi hicho watu wakibebwa mitaani kupelekwa jeshini
Soma vizuri historia ya Vita ya Kagera.Tulizunguka sana. Arua, Kasese, portfot na kwingine kabla ya kufika Kampala. Swali ni kwanini tulizunguka sana badala ya kukatisha tu na kufika hapo kampala na kumtimua huyu nduli?
Mkuu vingine humu ni vitoto vinavyonuka mikojo.Wacha hadithi za kusimuliwa na watu waliosimuliwa pia. Nimeshaandika humu kwa kirefu sana kuhusu vita hiyo hivyo hakuna haja ya kuanza kujibizana na mtu anayekuja hapa na hadithi za kusimuliwa wakati mimi mwenyewe nilikuwamo ndani. Eti watu wakibwebwa mitaani kwenda jeshini? Unazungumuza kwa akili timamu kweli na kwa nia ya kufahamishana ukweli au unataka na wewe uchangie?
Eti binamu yako alikuwepo, je akija mwingine akatoa maelezo mengine, akasema Babayake alikuwepo, utabafilisha unachoamini sasa hivi, maana Baba ni mtu wa karibu kuliko binamu.Kwa taarifa yako majeshi ya Uganda yalikuwa vizuri sana kabla ya uasi.
Vita ilipoanza tulipoteza wanajeshi wengi mno japo taarifa zilifichwa, binamu yangu amepigana na amesimulia mengi mno ambayo serikali haikuweka na haitaweka wazi.
Hivyo unaposema kwani tulizunguka, unafikiri hao jamaa walikuwa dhaifu kiasi hicho?
Vita ina mbinu nyingi, moja wapo ni kumzunguka adui wakati yeye anapambana na wale waliom face... ghafla anashangaa anashambuliwa eneo ambalo hakutegemea.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ashakum si matusi; ila wazungu walisema "an empty container/debe makes the most noise"Wewe mwenye bundle
Kwa nini wewe ushindwe kumuandikia na kumpigia simu akupe hiyo context uliyoitaja ???au huna context unafoka na kumwaga povu tu ??