Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?


Museveni hakumuondoa Obote. Obote alipinduliwa na majeshi yake.
 
Museveni hakumuondoa Obote. Obote alipinduliwa na majeshi yake.
Ni kweli, nashukuru kwa sahihisho hilo. Nalo linazidi kuweka umbali kati ya Lule, Binaisa na Obote. Shukran
 

Zakumi;
Hakufuatilia mtiririko mzima wangu na William nanukuu "Kumpiga Amin mpaka ndani ya nchi yake kumetugharimu na mpaka leo bado tunalipia, ni wajibu wetu wananchi wenye uwezo wa kufikiri kuuliza kuhusu hizi failed policies!, ambazo zingine physically zinatuumiza mpaka leo, ambapo wahusika hawapo!". Nilichojaribu kumuelewesha tu gharama za vita madeni mengi tu yalishamehewa msikwepe ukweli kinachotugharimu ni ufisadi gharama ya ufisadi ni kubwa kuliko vita ya Kagera

Chama
Gongo la Mboto DSM
 

First thing first, hakuna mwananchi asiye na uwezo wa kufikiri. Tukirudi kwenye mada kamili kwa maoni yangu binafsi, ufisadi ni matokeo na sio kiini matatizo yetu.

Kiini cha matatizo mengi ya Tanzania ni kuwa katika miaka ya 60, 70 na 80, Tanzania haikujenga human resource capabilities zake ambazo zingeweza kulisaidia taifa katika mazingira ya kisasa ya kiuchumi.
 

Zakumi
Unaposema ufisadi ni matokeo na sio kiini cha matatizo yetu unamaanisha kitu gani? Je baada ya 1980 hadi 2012 tumeweza kujenga hizo human resource capabilities? Ufisadi umekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwenye maendeleo ya uchumi wetu; badala ya watu kujadili hoja za msingi tunaendesha propaganda ambazo hazina maana yeyote ile; leo serikali imeshindwa kutoa mkopo wa vyuo vya elimu ya juu kutokana na ukosefu fedha hii si aibu rasimali zote tulizokuwa nazo bado tunashindwa kusomesha wanafunzi wetu? Na hili nalo pia tulaumu vita vya Uganda?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 

Chama,
Si busara kukurupuka na kutoa comment....nasisitiza, si busara hata kidogo. Pitia post zangu, zote nimetamka wazi kwamba Nyerere hakufanya kosa hata kidogo kumpa hifadhi Obote...hapa nasisitiza kwa herufi kubwa labda utaelewa: NYERERE HAKUFANYA KOSA KUMPA HIFADHI OBOTE....Pitia post zangu utaona huo msisitizo. Nilichosema na ambacho nitaendelea kukisimamia ni suala la Nyerere kumwacha Obote na supporters wake kuitumia Tanzania kama uwanja wa mafunzo na maandalizi kwa ajili ya kurudi Uganda kum-overthrow Amin. Hilo ndilo ninalopinga mimi. Mwaka mmoja baada ya Obote na wafuasi wake kuingia Tanzania, wafuasi hao walivuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganda na kufanya jaribio lililoshindwa la kumpindua Amin. Baada ya kushindwa, wakakimbia na kurudi tena Tanzania. Hoja yangu hapo ni kwamba huwezi kufanya mapinduzi dhidi ya serikali ya kijeshi kama ya Amin bila kufanya maandalizi ya kutosha; maandalizi hayo ikiwa ni pamoja na maandalizi ya kijeshi. Kama ndivyo, maandalizi ya kijeshi yaliyolenga kwenda kumpindua Amin yalifanyikia wapi ikiwa wana-mapinduzi hao walitokea kwenye ardhi ya Tanzania na waliposhindwa wakakimbilia tena Tanzania?! There's no way kwamba intelligence na serikali kwa ujumla kwamba hawakufahamu.....walifahamu! Sasa kwanini Nyerere aliruhusu jam bo hilo?! Hata kama wewe ungekuwa ndie Amin halafu unagundua nchi jirani inatoa msaada wa kijeshi kwa kikundi kinachbolenga kukuondosha madarakani ungekaa kimya na kupuuza?! Amin, sawa na kiongozi yeyote alikuwa na haki ya kutangaza hali ya hatari dhidi ya Tanzania kwavile ilishathibitika kwamba Tanzania inafadhili harakati dhidi yake. Hakuna kiongozi hata mmoja duniani ambae angekuwa tayari kupuuzia jambo hilo.

Kwa kumalizia, narudia tena na tena.....sioni tatizo kwa Nyerere kumpa hifadhi Obote.
 

Serious Crime ni kama ile ambayo ilifanywa na Nyerere ya kufadhili harakati za kijeshi dhidi ya Amin ndani ya ardhi ya Tanzania. Hakuna ,kiongozi yeyote duniani ambae angepuuzia ambacho kilifanywa na Nyerere.
 

NasDaz
Sijakurupuka narudia tena upeo kwenye medani ya siasa bado kidogo itachukua muda; Idd Amin alikuwa ni dikteta mwenye kuuwa raia wake kama kuku; halikuwa kosa kuwapatia hifadhi raia ambao walikuwa wanakimbia mauaji; majaribio yaliyofanyika kumuua Idd Amin yalifanyika ndani ya Uganda ni lazima ukubali Amin hakuwa kipenzi cha waganda hasa alipoanza kuua raia ovyo. Kwa raia hao kukimbilia Tanzania sidhani kama kulijustify kitendo chake cha kuvamia Tanzania na kuua watanzania wasio na hatia; hivi sasa tunahifadhi wakimbizi wa Rwanda na Burundi sidhani kama Kagame akiamua kutushambulia kwa vigezo vya wakimbizi tutamwacha;Amin alijiamini baada ya ahadi za silaha na Ghadaf kitu ambacho alipatiwa; kumwondoa ilikuwa sawa kabisa tungemwacha angeendela kabla ya vita vya Kagera majeshi yake yalishawahi kuvuka mpaka na kurudi sasa sielewi mganda wewe unachohoji.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Kuna mahali ukisoma unajiuliza huyu aliyeandika amelipwa kiasi gani! Yaani ufisadi huu wa kutisha bado mtu anapata ujasiri wa kusema si kiini cha matatizo, na anataka kutuaminisha kuwa ni matokeo ya utawala wa awamu ya kwanza. Hivi kipindi cha utawala ule kulikuwa na ufisadi wa kiwango hiki? Hizi chuki mbona hatari sana.
 

Sidhani kama tungemtimua tu ingetosha kwani lazima angejipanga na angerudi na pia alikuwa akiwatesa wananchi wa uganda nadhali ilikuwa sahihi kumwondoa kabisa
 

sasa kama unakubali kuwa Idi Amin alikuwa mwendawazimu unashindwaje kuamini ukweli kuwa Amini ndiye aliyeanza uchokozi au hujui tabia za kiwendawazimu? asiyejua tabia za kiwendawazimu hawezi akawa sio mwendawazimu!
Mtu alieweza kupora mali za waasia walizochuma kwa jasho lao kisha kuwafukuza na kugawa mali hizo kwa rafiki zake unamchukuliaje? ukitaka ukweli waulize waganda waliokuwepo enzi za Amin watakupasha ukweli, na jiulize kwanini waganda waliyaunga mkono majeshi ya TZ na kuwashangilia na kuwaita wakombozi wao? wewe unadhani walikuwa wamekombolewa kutoka kwenye nini?
Acheni kuja na historia za kutunga zisizo na mashiko!
Kama Nyerere alikuwa mchokozi kwanini OAU au UNO hazikumlaani!? acheni hoja za kipuuzi ambazo ambazo zinaweka bayana ufinyu na umbumbumbu wa tafakari zenu.
 

Una umri gani?
 
unapoamua kuja na negative criticism dhidi ya Nyerere na maamuzi yake lazima uje hapa na parallel justification ya kufanya hivyo kwa kuitizama status quo...kwamba ni yapi mazuri yanayofanywa na watawala wa sasa TZ ambayo yanayokufanya uje na hizi on and off negative critiques dhidi ya Nyerere...Kwangu mimi...kwa kifupi sana nina support maamuzi ya Nyerere kumuondoa Idd Amin Tz na uganda..kwani tayari alikuwa ni threat tosha kwa security ya TZ kwa wakati huo...Labda swali la msingi kwako mleta mada....ni logic gani ilitumiwa na JK alipoivamia Comoro na kuwaondoa waasi kwa kutumia majeshi ya TZ????.......labda ukijibu swali hili utakuwa umejijibu mwenyewe hoja yako.......
 
Hivi ilikuwa inahusu nini sisi raia wa Tanzania kulazimishwa kuvaa T-Shirts za Uganda People's Congress (UPC).
 

Mkuu wangu Chama,
Mbona nimeongea lugha nyepesi sana kuweza kueleweka na yeyote aliye mtumiaji wa Kiswahili?! Mbona ung'ang'ania sana suala kwamba haikuwa kosa Nyerere kuwapokea wakimbizi toka Uganda wakati nami nimeshaweka wazi kwamba Nyerere hakufanya kosa kumkaribisha Obote?! Unaona taabu gani kupitia post zangu za nyuma?! Ina maana ni mahaba yako kwa Nyerere ndiyo yanayokufanya ushindwe hata kuyaona mambo madogo kama haya?! Narudia, haikuwa kosa kwa Nyerere kumpokea Obote na wafuasi wake; kosa ilikuwa Nyerere kumruhusu Obote kuendesha harakati za kijeshi ndani ya ardhi ya Tanzania huku harakati hizo zikiwa pia zinafadhiliwa na serikali....ugumu wako katika kuelewa hapo upo wapi?! As far as ilishathibitika kwamba Obote alikuwa anaendesha harakati za kijeshi dhidi ya Amin kutokea Tanzania; Amin sawa na kiongozi yeyote yule ange-react tu. Umetoa mfano wa wakimbizi wa Rwanda na Burundi, am sorry to say tht huo ni mfano mfu kwavile hakuna kikundi chochote ama kutoka Rwanda au Burundi ambacho kinaendesha harakati za kijeshi kutokea Tanzania huku wakipata msaada huo kutoka Tanzania. Kwahiyo halitakuwa jambo linalokubalika endapo ama Rwanda au Burundi wakiishambulia Tanzania. Lakini endapo itadhihirika kwamba kuna harakati za kijeshi dhidi ya Rwanda au Burundi; harakati ambaz zinapata support kutoka Tanzania; then ama Rwanda au Burundi watakuwa na haki kutushambulia.

Sheria za kimataifa juu ya vita zinatamka wazi kwamba, unaweza kuanza kushambulia endapo imedhihirika kwamba adui yako anaonesha dalili za kutaka kukushambulia. Obote baada ya kuingia Tanzania na kufuatiwa na wafuasi wake; hapo hapo kwa msaada wa Nyerere wakapanga kwenda kuivamia Uganda. Hapo ndipo linapoanzia kosa la Nyerere. Alitakiwa kumpokea Obote na wafuasi wake kama wakimbizi tu na si vinginevyo. Tatizo lenu supporters mnaanzia pale Amin alipoingiza majeshi Tanzania na kwa makusudi mnaacha kuzingatia harakati za Obote mara baada kupinduliwa.
 
Hivi ilikuwa inahusu nini sisi raia wa Tanzania kulazimishwa kuvaa T-Shirts za Uganda People's Congress (UPC).

Mkuu ritz,
Upo serious au unatania?! Ina maana ni kweli watu walikuwa wanalazimishwa kuvaa t-shirt za UPC?! Tell me u're kidding!
 
@Zakumi, nchi ambayo ufisadi umekithiri to the extent umekuwa kama a way of life, yani kila kitu ni rushwa utajenga vipi human resources capabilities?Please tell me its a joke!
chama, a very good question...
 


- Mkuu hlod on a second, hapa tunakata ishus za policies za Mwalimu na effect yake to this Nation, hapa tunakata ishu ya kumpiga Amin na wewe unaweza kufungua ya mazuri ya MWalimu, otherwise ni vyema ukasema uzuri wa kumsambulia Amin mpaka ndani ya nchi yake, kuliko kuwaamulia wengine what to say na what to writte, that is never the JF's Mission!

William.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…